Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Yeah Gari yenye sensor Kila mahali huwezi kuikagua kila siku, kama Tyre ikidungwa tu na msumari Taa inawaka ya nini Sasa kuanza kukagua matari Kila siku, labda kama ni mabovu kwamba unahofia yatabasti njiani
 

Yaani BMW engine Oil service ufanye baada ya 3000Km.


Kweli wajapani wa Bongo mmefanya kazi kubwa sana kuturn hizi German mashines kuwa japanese motors.
 
Mkuu Oil Gani ni recommended kwa BMW X3 ya 2008 kwa hali ya hewa ya Dar ambayo inaweza kutoboa hizo Kilometers 5,000
 
Yaani BMW engine Oil service ufanye baada ya 3000Km.


Kweli wajapani wa Bongo mmefanya kazi kubwa sana kuturn hizi German mashines kuwa japanese motors.
Mkuu kama unaendesha Gari ya Ujerumani huko huko Ujerumani ni sawa unaweza badilisha baada ya kilometers 5,000 lakini kama unaendesha Gari ya German hapa Bongo basi ni vizuri kuchange oil Kila baada ya kilometers 3,000 kwasababu kuna factors nyingi zitakazosababisha usitoboe hizo Kilometers elfu 5
 
Kama hakuna leakage huhitaji kuongeza oil hapo kati
Taa ya njano kuwaka ni 'normal warning ' na sometimes mfumo unachanganyikiwa kidogo
Nilichoona hapo ni bei ya oil, naona kama wamepiga ndefu.. Labda kama ni ile oil ya km 10,000 hapo sawa
 
Ipo siku utaliuza hapa hapa
 
Hata mimi najua BMW ni 10k ndio service, sijui gari yake imeandikwaje au amefata wafundi wa mtaani!!
Google Atlantic ipo Mikocheni Coca-cola karibu na GSM iliyoungua, halafu Rudi hapa uniambie kama ni wa mtaani, Picha linaanza nilivyoenda kwa mara ya kwanza nimekabidhi funguo reception naona mzungu ndio anakabidhiwa funguo akaishughulikie gari maana ndio ilikuwa imetua Bongo

Niliacha milion 1 na laki 2 kuchekiwa tu Kila Kitu kama Kiko sawa na vilivyo badilishwa ni oil filter na Air filter basi
 
Wajinga ndo waliwao ,kubadili oil kwa kilometa ipo siku utalia ,Cha msingi angalia gari umelitumiaje

Eg kilometa 5000 Ni sawa utembee km 1000 kwa siku tano unaweza ua gari
 
Mzungu Ni asili tu

Gari langu lilivopata ajali , garage Ni ya mchina, ofisini Yuko mchina Bei tumepatana na mchina ila gari imenyooshwa na wabongo kwa vifaa vyamchina
 

Kwa hio kuchekiwa ukapewa mkeka wa milion kwamba ndo ukaona wako vizuri ,, je ningekupeleka sehemu likachekiwa wakakwambia au kukupa mkeka wa Bei ghali zaidi means ungeona huko pa Bei ghali ndo mafundi😁 we bado mshamba na utapigwa sana

Ushamba wa watu wengine wenye pesa na akili zipo down ndo inafanya wajanja tuishi mjini just kwa kujua ongea tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…