Habari ya Jumapili wadau,
Mimi kijana wa miaka 25 ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea kuna kazi naifanya ambayo kwa mwenzi huwa inaniingizia kipato cha laki tatu(300000). Sasa nilikuwa nahitaji mpangilio mzuri wa matumizi wa haka kamshahara kangu ili nipate kubaki na akiba hata wazazi siku wakihitaji msaada wa kifedha nipate kuwasaidia.
Naombeni ushauri wenu mlionitangulia katika maisha ya kujitegemea.
Ngoja nitoe ushauri kwa mtizamo wangu. Binafsi naamini kuwa kipato chochote kile mtu anaweza kufanya jitihada na kufika pale anapotaka kufika.
Unapokuwa na kipato chochote kile iwe kikubwa au kidogo ni vyema ukikitumia kwa mgawanyo wa asilimia.
Kuna makundi tofauti kwenye matumizi ya pesa baadhi yake ni:-
1. Matumizi ya kawaida, hapa najumuisha chakula, nauli, vocha, kuhonga, umeme, maji na kadhalika. Kwa kipato chako unaweza ukaelekeza 60% ambayo ni 180,000
2. Matumizi ya ununuzi wa mali binafsi kama kiwanja, gari, simu, furniture na kadhalika. Unaweza ukaelekeza 15% ambayo ni 60,000. Unakuwa unakusanya taratibu taratibu unanunua assets taratibu taratibu.
3. Matumizi ya uwekezaji, hapa ni kama unaanzisha biashara, au unanunua hisa za makampun ili kipato chako kizalishe mara dufu na kadhalika. Unaweza pia ukaelekeza 15% unakusanya huku unafikiria biashara ambayo unaweza ukawekeza.
4. Mfuko wa dharula, hii ni kwaajili ya mambo ambayo haukutarajia kama kuibiwa vitu vya muhim kama simu, matatizo mengne mengine na kadhalika. Unaweza ukaelekeza 10% ambayo ni elfu 30, hii hela hakikisha hauigusi iache ikue hivyo hivyo taratibu ni kwaajil ya dharula tu.
Wakati huo unapambana kuhakikisha unaongeza kipato chako, usiridhike na kipato cha 300,000. Jitahidi kuwa mbahiri kadri uwezavyo zaidi ya mchaga, tupo tulioanza kwa kipato cha 150,000 kwa mwezi na tukaweza.
Kipato kikikua unaweza ukaadjust asilimia zako na ukaongeza fungu lingine ambalo ni matumizi ya starehe na kujifurahisha unayoweza kuiwekea hata asilimia 5% ila kwasasa si vyema ukawa ni hicho kipengele.