Ushauri namna ya kupata tractor lenye uwezo wa kung'oa miti/visiki na kulima

malewa

Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
15
Reaction score
4
Wadau naombeni ushauri ni tractor aina gani yenye uwezo wa kung'oa miti/visiki na kulima pia. Je inapatika hapa nchini?
 
Kung'oa visiki na miti hufanywa na bulldozer kama hili hapa chini, kwa mbele husukuma mti na kuanguka, nyuma kuna mavyuma huingia chini ya ardhi na kung'oa visiki hadi mizizi.

 
Ndugu Asante nakushukuru sana kwa kupanua uelewa wangu katika hili.
 
Ndugu Asante nakushukuru sana kwa kupanua uelewa wangu katika hili.

Ulitaka kuelewa tu au kukodi/kulitumia hilo burdoza? gharama ya kukodi huo mtambo ni iko juu sana ndugu wala usipoteze muda wako kwenda kuulizia. Nakushauri tafuta vijana shupavu wakung'olee hiyo miti ni nafuu zaidi.
 
Nina shamba, lengo langu ni kuona kama ningeweza hata kununua used ama kukodisha. Lakini kutokana na maelezo nikiyopata kutoka ndugu Asante, nimeona ni ngumu kuupata mtambo kama huo na pia kukodi si rahisi pia. Nitatumia ushauri wako ndugu Kisima wa kutumia vibarua. Nashukuru sana.
 
Nenda pale KINONDONI MAKABURINI kuna wale wachimba makaburi ndo wataalamu wa kung'' oa visiki mashambani na bei poa
 

Kama shamba lako ni kubwa ni rahisi na nafuu ukikodisha bulldozer, kwa siku moja lina uwezo wa kusafisha ekari 10 au zaidi kung'oa miti na visiki na kusawazisha vichuguu.
 
Tree Mover ni mtambo pekee si tu kung'oa miti unaweza hata kuibeba na kuisafirisha kwenda kuipanda sehemu nyingine. Jaribu kuingia kwenye youtube ucheki inavyofanya kazi.
 
Kama shamba lako ni kubwa ni rahisi na nafuu ukikodisha bulldozer, kwa siku moja lina uwezo wa kusafisha ekari 10 au zaidi kung'oa miti na visiki na kusawazisha vichuguu.

Kweli linaweza kufanya kazi haraka sana ila issue ni hiyo bei ya kukodisha na sizani km linaweza kung'oa ekari10 kwa siku labda hilo pori liwe halijashona miti. Usije ukaambiwa hiyo ekari10 linang'oa kwa sh10M hapo ndo baraa linapoanzia.
Wakati vijana wa kazi kung'oa na kusafisha ikizidi sana ni sh300k kwa ekari1.
 

Naona unatishika ulipoona picha ya ukubwa wa bulldozer;

Kwa siku unakodisha kwa masaa 8 kwa gharama ya sh. 800,000.00
Mafuta ni juu yako kwa masaa 8 itatumika diseli ya 200,000.00
Utamlipa operator shilingi 50,000.00 kwa siku

Jumla kuu ni shilingi 1,050,000.00 kwa siku kusafisha eka 10

Kuna gharama ya kulichukuwa kwa lori kutoka mjini kupeleka shamba na kulirudisha gharama zake inategemea umbali lakini kama ni mkoa wa Pwani gharama ni wastani wa shilingi 1,000,000.00

Kung'oa kwa mikono

Bei ya shilingi 300,000 x 10 = 3,000,000.00

Utanunua mashoka, sururu, mapanga, tupa. Utagharamia kambi ya vijana

Kusafisha ekari 10 itachukua zaidi ya siku saba inategemea idadi ya watenda kazi, na ukubwa wa miti na visiki
 

Nashukuru kwa ufafanuzi murua mkuu Asante. Ila wasiwasi wangu bado upo kwenye uharisia wa kung'oa ekari10 kwa siku. Lakini pia utalazimika kununua chainsaw ya kukatia hiyo miti iliyoangushwa ili shamba libaki kweupe zaidi. Hivyo nashauri uongezee na gharama ya chainsaw sh2000000, petrol&oilchafu,oparetor na utachoma mkaa masalia ya hiyo miti ili angalau kufidia gharama za usafishaji.
 
Last edited by a moderator:

kaka ukitaka dozer lipo kwa milioni 30 mpaka 25 ni email kama utataka
 
kaka ukitaka dozer lipo kwa milioni 30 mpaka 25 ni email kama utataka

Kwa bei hiyo, ubora wa doser husika ni wa mashaka. Pia si rahisi kusafisha ekari 10 kwa siku hata kama ni vichaka.
 
Wakuu nashukuru kwa maelezo mazuri na ya kuelimshana kuhusu suala hili. Nilikuwa sijapitia humu kwa muda kidogo, nimejifunza kupitia angalau kila wiki. Nitafuatilia ushauri kadhaa mlioutoa ili hatimaye niweze kuamua cha kufanya.
 
hilo doza la kuuzwa milion 25 - 30, chini ya bei ya trekta!!! mmmh!!!!!!! akili za kuambiwa unachanganya na za kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…