Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu Asante nakushukuru sana kwa kupanua uelewa wangu katika hili.
Nina shamba, lengo langu ni kuona kama ningeweza hata kununua used ama kukodisha. Lakini kutokana na maelezo nikiyopata kutoka ndugu Asante, nimeona ni ngumu kuupata mtambo kama huo na pia kukodi si rahisi pia. Nitatumia ushauri wako ndugu Kisima wa kutumia vibarua. Nashukuru sana.
Kama shamba lako ni kubwa ni rahisi na nafuu ukikodisha bulldozer, kwa siku moja lina uwezo wa kusafisha ekari 10 au zaidi kung'oa miti na visiki na kusawazisha vichuguu.
Kweli linaweza kufanya kazi haraka sana ila issue ni hiyo bei ya kukodisha na sizani km linaweza kung'oa ekari10 kwa siku labda hilo pori liwe halijashona miti. Usije ukaambiwa hiyo ekari10 linang'oa kwa sh10M hapo ndo baraa linapoanzia.
Wakati vijana wa kazi kung'oa na kusafisha ikizidi sana ni sh300k kwa ekari1.
Naona unatishika ulipoona picha ya ukubwa wa bulldozer;
Kwa siku unakodisha kwa masaa 8 kwa gharama ya sh. 800,000.00
Mafuta ni juu yako kwa masaa 8 itatumika diseli ya 200,000.00
Utamlipa operator shilingi 50,000.00 kwa siku
Jumla kuu ni shilingi 1,050,000.00 kwa siku kusafisha eka 10
Kuna gharama ya kulichukuwa kwa lori kutoka mjini kupeleka shamba na kulirudisha gharama zake inategemea umbali lakini kama ni mkoa wa Pwani gharama ni wastani wa shilingi 1,000,000.00
Kung'oa kwa mikono
Bei ya shilingi 300,000 x 10 = 3,000,000.00
Utanunua mashoka, sururu, mapanga, tupa. Utagharamia kambi ya vijana
Kusafisha ekari 10 itachukua zaidi ya siku saba inategemea idadi ya watenda kazi, na ukubwa wa miti na visiki
Nina shamba, lengo langu ni kuona kama ningeweza hata kununua used ama kukodisha. Lakini kutokana na maelezo nikiyopata kutoka ndugu Asante, nimeona ni ngumu kuupata mtambo kama huo na pia kukodi si rahisi pia. Nitatumia ushauri wako ndugu Kisima wa kutumia vibarua. Nashukuru sana.
kaka ukitaka dozer lipo kwa milioni 30 mpaka 25 ni email kama utataka
kaka ukitaka dozer lipo kwa milioni 30 mpaka 25 ni email kama utataka