Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Expectation is the mother of all disappointment!
Nitaisoma zaidi hii thread, nimeishia katikakati.
Asa MNDEE mbona hujatupa mlango wa hiyo sehemu? atashareje hii experiece huko?
Wakuu hii social group ni ya hapa hapa JF, karibuni mjiunge. Path ni hii
JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Social Groups > JF Blogs
Infertility and Adoption Support Group
Kwa wale wenye interest na IVF process nitapost my own personal experience in two months so stay tuned!
Kaka Mbu thanks,
Sijapitia posts zote kusoma ila i think ni mutual understanding between the two .. sisi especially in african society neno mtoto ni la familia yote nasi la wanandooa peke.. its an open table discussion na kila mwanandugu ana right ya kuulizia 'whats is happening?' sasa wanandoa cant elude this business ya kuwa na mtoto .. they are haunted from all corners hata marafiki wataulizia pia coz ndo jamii yetu ilivyo. mm nasecond adoption .. coz in our african traditional society theres no way utamkataza mwanaume kuoa, kwani jamii nzima itamsuport kwa hili .. kama kaoa kanisani watamlazimisha hata afanye traditional ama secret wedding.. ilimradi tu apate mtoto ..mke wake akitaka asitake .. kwani itakua right yake.. dini pia kama ss waislamu kama mke ambaye anamatatizo ameridhia mume anaweza akaoa .. na mwanamke pia asirule out the fact kwamba mwanaume kwa kigezo hiki bila ridha yake atalazimisha tu kuoa.
adoption ambae na advocate for ni within the family .. unachukua mtoto wa ndugu yako na anakua wa kwako ... which is not bad .. rights zote zinahama kwako .. some even do it well .. kama binti yoyote hapo nyumbani amebeba mimba bila mpango na baba wa mtoto kamkimbia .. huyu mtoto anakuwa wa familia na kumpa nafasi zaidi anapewa one of the victims of such circumstances kumlea ...ama hata mwengine ambaye amefiwa na wazazi ama hata mmoja tu anajitolea kumpa mwenzie mtoto .. especially wanawake between dada's this is very possible. In my family this has happened, kuna cousin wangu mmoja has the same problem, mdogo wake akaamua na mumewe kwamba they had enough kids .. 3 ila they should try the fourth time na wakifanikisha .. that kid atakua wa sistaake .. alhamdulillah it happened so ... kila kitu cha huyo mtoto kikawa kinatoka kwa huyo mamaake mpya.. till alivyoacha kunyonya ..like mwaka mmoja mtoto akapelekwa kwa mamaake ... mpaka leo shes 18 na anatambua ukweli ila mama mwengine hamjui anamtambua mamaake huyo alomlea ..
This issue tackled kifamilia ina very excellent results .. coz we cant elude this .. all the family is concerned coz hata kama umezaa the whole family will participate kuwalea hawa watoto wako ... you cant close doors to all.
To sum it up .. si dhani kama couples should pretend kama hakuna ufa ...upo .. swala la watoto ni lazima kwa mtu yoyote .. atatamani tu kwani ni vitu ambavyo mtu anafeel vitakamilisha maisha yake .. kuavoid affairs za siri .. mtu kuja kushtukia kwamba mume wake anamke njee na watoto, i would second adoption lakini within the family bounds .. naona ina hadhi zaidi .. otherwise any other type of adoption is also good ila hapa mtoto baadae akikukua theres a possibility akaanza kudadisi ametoka wapi .. na mambo identity yake itaweza kumsumbua kisaikologia akiwa mkubwa.
To sum it up .. si dhani kama couples should pretend kama hakuna ufa ...upo .. swala la watoto ni lazima kwa mtu yoyote .. atatamani tu kwani ni vitu ambavyo mtu anafeel vitakamilisha maisha yake
Kaka Mbu, kwani uhusiana kati ya bi mdogo na bi mkubwa upo vipi ? maana mara nyingi huwa kuna mvutano wivu vinyongo na ushindani mkubwa kati ya Mke aliyetangulia na Bi mdogo, hasa kama Bi mdogo kwa namna moja au nyingine alikuwa kwenye picha kabla ya bi mkubwa kutalikiwa (situation ambayo hutokea mara nyingi), mshauri bwana mkubwa asi underestimate hilo, kama kuna tatizo liwekwe wazi lijadiliwe, inaweza ikasaidia kujua mzizi wa tatizo zima
Wengi ambao shida pekee ni kukosa mtoto, baada ya kujaribu njia mbalimbali bila mafanikio wanaweza kupokea ushauri na kufarijika kwa kulea watoto wa wenzao, kuadopt, kulea yatima etc, hali ambayo haiwezi kumfariji anayeshindana na mwenzie kwa sababu hata akiadopt bado atakuwa inferior kwa mwenzie kwa sababu hajazaa mwenyewe, ndio maana wengine huwa wanakataa kabisa adoptions au kulea watoto wa wenzao kwa sababu wanajua hiyo haiwezi kuwa sulution ya matatizo yao
Kuna mambo yanayo leta hisia kwamba inawezekana machungu yake bi mdogo yanasababishwa na ushindani kati yake na bi mkubwa kama vile
 bi mdogo kusema ananyanyasika kwa vile hazai
 watoto wa bi mkubwa aliowalea toka utotoni kuhamia kwa mama yao na bi mdogo kutokuelewana na watoto hao baada ya wao kuhamia kwa mama yao
 bi mdogo anataka kupata mtoto wa kuzaa mwenyewe na si vinginevyo
 bi mdogo kutafuta mtoto kwa waganga wa kienyeji _ inawezekana kuna mganga aliye mpoint bi mkubwa kama ndio mbaya wake maana tunasikia waganga wengi ndivyo walivyo
Japo watoto ni sehemu kubwa sana ya ndoa na raha zake mimi naamini kabisa kama mnapendana mnaweza kuoana hata kama mnajua hamtaweza kuzaa. Na pia kabla ya kuoana wapendanao waongelee vitu kama hivi na waulizane kabisa ikiwa hivi bado uta nipenda au la?
Hili ni neno ndugu yangu Pretty... kweli kabisa wanandoa hiki ni kitu wanapaswa kujua ila wengi wanakuwa wakiweka mbele tegemeo la watoto wakisahau kuwa Muumba wetu anakuwa na mpango na kila kiumbe wake.Kuna watu wameumbwa bila uzazi kwa sababu huenda kazi yao ni nyingine kabisa...huenda wao wameumbwa waje kusaidia wengine wenye mahitaji mfano kutunza mayatima au kwenda kutoa huduma nyingine zenye kuhitaji mtu mwenye muda wa kutosha.Lakini hili linahitaji mtu mwenye imani ... na bahati mbaya hatuwezi kujua kiwango cha imani cha Bi Mdogo huyu.Ukizingatia pia kama aliwahi kuharibu mimba huko nyuma basi itakuwa ngumu kwake kukubali ushauri kama huu.Mtoto ni majaaliwa ya ndoa/matunda ya ndoa, hivyo inawezekana mkapata au mkakosa.
.
...ngoja nikupe kisa hiki;
"Bwana mkubwa yeye kutokana na umri wake na huyo mkewe, kaamua kumshukuru mungu kwa majaaliwa hayo. Anampenda mkewe na amekubaliana na hali japo alitarajia Bi mdogo angemzalia mtoto wa Kiume, aje kuwa mrithi na Walii kwa dada zake.
Sasa, Bi mdogo yeye kila siku ni vilio na malalamiko kwamba bila uzazi hajakamilika. Mbaya zaidi ni upande wake yeye Mke ndio unaoshurutisha Mke ajaribu kila namna almuradi amzalie huyo baba Mtoto, wakati upande wa mume wao walaaa...wanamchukulia wifi yao kuwa mkamilifu."
Ushauri wako/ wenu vipi kwenye case ya namna hii, maana hayo malalamiko, na vilio vya bi mdogo vinaletesha mgongano mkubwa kwenye maisha ya wana ndoa hawa.
Nionavyo mimi huyu bibie anasumbuliwa zaidi na mawazo (sio ya kukosa kizazi) bali ya maisha yake ya baadae pindi huyu bwana akifa?
!
...
Unajua, bi mdogo alipoolewa hawa mabinti walikuwa wadogo sana. Mabinti hawa walikuwa wanampenda sana mama yao mpya, na mpaka sasa wanamchukulia kuwa confidant wao muhimu.
Tatizo ni bi mdogo huyo katika siku za karibuni amekuwa ama kwa bahati mbaya/makusudi, analetesha chokochoko kwa hao mabinti. I mean kujibishana nao kishari shari, na kukata mawasiliano nao, wakati awali alikuwa mstari wa mbele 'kuwadekeza'.
Hili limekuja hasa pale mabinti hao walipohamia rasmi kwa mama yao mzazi, kuishi nae, na hivyo kuja kwa mama wa 'kambo' na Bw' mkubwa wakati wa likizo, au kusalimia tu.
...
Inafikia wakati inabidi papigwe msitari chini kama ilivyoshauriwa hapo awali...kuitisha kikao cha wazazi pande mbili na Mume akiwa ndiye mwenye mamlaka ya nyumba kutoa msimamo wa mwisho. Kinyume na hapo mvutano hautokwisha kwani kila mtu atakuwa anavutia kwake.
Mheshimiwa asipojiangalia atakuja lea wajukuu badala ya watoto,...haipendezi mwanaume kesha retire ilhali bado anahangaikia ada za shule za watoto... ndio kuwatwika mzigo mabinti zake (wakubwa) bureee...
...
...uhusiano wao mbaya sana. Bi mkubwa anaona kama si bi mdogo, huenda huyo bwana mkubwa angerudiana nae. Na bi mdogo anaona asipozaa mtoto, huenda Bw'mkubwa akarudiana na mama watoto wake. Wakati huo huo, huyo mheshimiwa keshaapa heri aoe mke mwingine kuliko kurudiana na huyo ex-wife wake, kwa jinsi alivyomtenda...