Mh Mbu,
Kwa heshima zote naomba nami niweke neno kwenye hii mada nyeti.
Mwanzo wa mapenzi na hata ndoa ni raha tupu na focus huwa ni kwa wawili wapendanao.Kipindi hiki ni vigumu kuuona ukweli na hata kama wawili hao wangeambiana watathmini katika ndoa yao itakuwaje kama hakuna watoto, bila shaka kila mmoja kwa wepesi sana angesema kuwa hiyo haitakuwa hoja.Mapenzi yangekuwa yamewapofusha wasiweze kuuona ukweli, hivyo basi naomba nitofuatiane kidogo na Mwana F1 hapa chini:
Japo watoto ni sehemu kubwa sana ya ndoa na raha zake mimi naamini kabisa kama mnapendana mnaweza kuoana hata kama mnajua hamtaweza kuzaa. Na pia kabla ya kuoana wapendanao waongelee vitu kama hivi na waulizane kabisa ikiwa hivi bado uta nipenda au la?
Mtoto ni majaaliwa ya ndoa/matunda ya ndoa, hivyo inawezekana mkapata au mkakosa.
.
Hili ni neno ndugu yangu Pretty... kweli kabisa wanandoa hiki ni kitu wanapaswa kujua ila wengi wanakuwa wakiweka mbele tegemeo la watoto wakisahau kuwa Muumba wetu anakuwa na mpango na kila kiumbe wake.Kuna watu wameumbwa bila uzazi kwa sababu huenda kazi yao ni nyingine kabisa...huenda wao wameumbwa waje kusaidia wengine wenye mahitaji mfano kutunza mayatima au kwenda kutoa huduma nyingine zenye kuhitaji mtu mwenye muda wa kutosha.Lakini hili linahitaji mtu mwenye imani ... na bahati mbaya hatuwezi kujua kiwango cha imani cha Bi Mdogo huyu.Ukizingatia pia kama aliwahi kuharibu mimba huko nyuma basi itakuwa ngumu kwake kukubali ushauri kama huu.
...ngoja nikupe kisa hiki;
"Bwana mkubwa yeye kutokana na umri wake na huyo mkewe, kaamua kumshukuru mungu kwa majaaliwa hayo. Anampenda mkewe na amekubaliana na hali japo alitarajia Bi mdogo angemzalia mtoto wa Kiume, aje kuwa mrithi na Walii kwa dada zake.
Sasa, Bi mdogo yeye kila siku ni vilio na malalamiko kwamba bila uzazi hajakamilika. Mbaya zaidi ni upande wake yeye Mke ndio unaoshurutisha Mke ajaribu kila namna almuradi amzalie huyo baba Mtoto, wakati upande wa mume wao walaaa...wanamchukulia wifi yao kuwa mkamilifu."
Ushauri wako/ wenu vipi kwenye case ya namna hii, maana hayo malalamiko, na vilio vya bi mdogo vinaletesha mgongano mkubwa kwenye maisha ya wana ndoa hawa.
Ushauri kwenye hili ndugu yangu nitasema hivi:
Wanawake wengi wanaamini kuwa bila kuzaa basi hawajamilisha uanawake wao...ndio utawakuta mara waende kwa waganga mara watumie hata hila za kujaribu kupata mimba kutoka kwa wanaume wengine alimuradi basi wathibitishe wako kamili;
Kuna swala la security siku za usoni kama livyosema
Kweli hapa chini.Watu wengi hili hawalioni na hasa kama bado ni vijana.Angalia hata kwa wazazi wetu wanavyojisikia fahari kutambulisha wajukuu zao ndio tutaelewa kwanini bi Mdogo anang'ang;ania kuzaa.Uzeeni kuna upweke sana.Focus ya wazee mara nyingi ni kuangalia watoto wa watoto wao.Sasa Bi mdogo hili linampa shida sana.Ila anaweza kushauriwa kuwa hata kama hataki kuasili ( adoption) bado kuna watoto wa ndugu wa upande wake hata kama wale watoto wa bi Mkubwa maelewano yametetereka.Cha muhimu ni yeye kujenga ukaribu hasa na watoto wa nduguzake ili waje wawe nguvu yake huko mbeleni.Hii nimeiona hata kwa baadhi ya ndugu zangu mimi mwenyewe na inafanya kazi vizuri tu.
Nionavyo mimi huyu bibie anasumbuliwa zaidi na mawazo (sio ya kukosa kizazi) bali ya maisha yake ya baadae pindi huyu bwana akifa?
!
Wakati mwingine watoto wa kufikia hujakubadilika hata kama unawalea vema kama Mbu ulivyoonyesha hapa chini.Cha msingi ni huyu Bi Mdogo ashauriwe kuwa pamoja na yote, ajiepushe kujibishana nao na aendelee kuwaonyesha upendo tu maana huenda hawa watakuja kumfaa huko mbeleni.Kuendelea kujenga chuki ni kwa hasara yake mwenyewe maana Bw Mkubwa akiondoka duniani, basi ajue hatakuwa na mtetezi.
...
Unajua, bi mdogo alipoolewa hawa mabinti walikuwa wadogo sana. Mabinti hawa walikuwa wanampenda sana mama yao mpya, na mpaka sasa wanamchukulia kuwa confidant wao muhimu.
Tatizo ni bi mdogo huyo katika siku za karibuni amekuwa ama kwa bahati mbaya/makusudi, analetesha chokochoko kwa hao mabinti. I mean kujibishana nao kishari shari, na kukata mawasiliano nao, wakati awali alikuwa mstari wa mbele 'kuwadekeza'.
Hili limekuja hasa pale mabinti hao walipohamia rasmi kwa mama yao mzazi, kuishi nae, na hivyo kuja kwa mama wa 'kambo' na Bw' mkubwa wakati wa likizo, au kusalimia tu.
Huyo bwana naye inabidi aonyeshe msimamo wake katika suala hili... ama ampe uhuru aende kuolewa kwengine ama mwanamke akubali matokeo atulie.Isitoshe huyo bi Mdogo hatujaelezwa kama yuko katika nafasi gani kuja kulea watoto wadogo wakati mume umri ushaenda.Ashauriwe aangalie hilo nalo maana kuzaa kunaendena na majukumu.Je atakuwa tayari kuja kulea "wajukuu" na "babu yao" pia?Kulea watoto wadogo ni shughuli achilia mbali kumlea mume anayezeeka.
...
Inafikia wakati inabidi papigwe msitari chini kama ilivyoshauriwa hapo awali...kuitisha kikao cha wazazi pande mbili na Mume akiwa ndiye mwenye mamlaka ya nyumba kutoa msimamo wa mwisho. Kinyume na hapo mvutano hautokwisha kwani kila mtu atakuwa anavutia kwake.
Mheshimiwa asipojiangalia atakuja lea wajukuu badala ya watoto,...haipendezi mwanaume kesha retire ilhali bado anahangaikia ada za shule za watoto... ndio kuwatwika mzigo mabinti zake (wakubwa) bureee...
...
...uhusiano wao mbaya sana. Bi mkubwa anaona kama si bi mdogo, huenda huyo bwana mkubwa angerudiana nae. Na bi mdogo anaona asipozaa mtoto, huenda Bw'mkubwa akarudiana na mama watoto wake. Wakati huo huo, huyo mheshimiwa keshaapa heri aoe mke mwingine kuliko kurudiana na huyo ex-wife wake, kwa jinsi alivyomtenda...
Kwa vyovyote ushindani wa wanawake hawa utaendelea kuwepo na hata kama bi mdogo atazaa asifikirie ndio mwisho wa matatizo.Hivyo Bi Mdogo ashauriwe ajitahidi kutokuongeza chumvi kwenye kidonda.Amheshimu Bi Mkubwa kwa vile alimtangulia na pia ajifikirie hali yake na matatizo aliyo nayo.Huenda hata haya matatizo ya kutaka kuzaa yanaongeza stress kwa bw. Mkubwa kiasi akajaona bora kujipumzisha kwa Bi Mkubwa kuepuka presha za bi mdogo.
Mbu naona umekuwa mstaarabu ukaacha kutuhabarisha jinsi bw. Mkubwa anavyowekwa kwenye wakati mgumu wa kuhakikisha mtoto anapatikana kwa bi Mdogo maana sidhani kama bwana huyo ana raha na hata anaweza kuhimili mikikimiki ya mradi huo wa kumzalisha bi mdogo.