Ushauri: Nataka kuanzisha kiwanda kidogo cha kukoboa nafaka

ludaga mdawagala

New Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
3
Reaction score
3
Habari Mimi ni kijana nataka mjasiliamali nataka kuanzisha kiwanda kidogo cha kukoboa nafaka kwa garama nafuu sana naomba ushauri bei ya mota pamoja bei ya kinu cha kukoboa na kusaga na kifaa vingine tafadhari
 
Habari Mimi ni kijana nataka mjasiliamali nataka kuanzisha kiwanda kidogo cha kukoboa nafaka kwa garama nafuu sana naomba ushauri bei ya mota pamoja bei ya kinu cha kukoboa na kusaga na kifaa vingine tafadhari
Unataka kufanyia wapi Biashara Yako, Hizi mashine zipo za mahitaji tofauti, zipo mashine za kusaga na kukubo mizigo midogo midogo. Pia zipo mashine ambazo zinasaga unga wa Biashara ule wa kupack sasa wewe unataka kufanya nini katika hivyo viwili?
Kwa kuongezea mashine zizosaga mizigo midogo hazina nguvu ya kusaga Unga wa kupack zitakuchelewesha, Ila mashine zinazoweza kusaga unga wa kupack zinaweza kusaga mizigo midogo midogo pia hapo sasa wewe umelenga kufanya nini zaidi
 
Asante mkuu Mimi nataka kufungua machine ya kusaga na kukoboa kwa kutumia umeme pia nataka nifungulie tabora hivyo naomba ufafanuzi jinsi ya kupata:-
1.mota kwa bei nafuu
2.kinu cha kukoboa NA kusaga
Ningependa xn kama ukinitajia na bei zake pia naomba kujua vinu vya sido na vinu vya dukani vipi ni imara na bei yake nafuu
 
Mashine za Sido ndio nzuri zukani zitakusumbua, Sema Upo mbali, mimi nipo Dar es salaam, Namiliki mashine ya Kukoboa na kusaga mizigo midogo midogo na Mikubwa pia zinasaga Pia, mashine yangu ya kusaga Nilitengenezea Dodoma Karibu na Soko La mahindi kibaigwa, na ya Kukoboa nilitengenezea hapa hapa Dar, kwanini ya Kusaga nilitengenezea Dodoma Ni kwasabau Jamaa anatengeneza mashine imara sana, chuma kabisa mpaka Leo mashine sijawahi kuichomelea tofauti na zile mashine za mabati,
 
Nataka kufungua mashine za kusaga mizigo midogomidogo ya kuhudumia
Sido na baadhi ya watu mtaani wanazitengeneza. Niliwahi kufuatilia wakantajia namba 75 inasaga kilo 750 sikumbuki kwa saa au kwa siku mtambo kamili inafika million 3.5 na namba 100 inasaga Tani 1 inafika million 4.5.
 
Hao wa kibaigwa naweza pata namba zao.mm nipo mbeya nahtaji mashine ngumu
 
Mkuu Milling naomba namba yako tuwasiliane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…