Ushauri: Nataka kununua gari hii

Ushauri: Nataka kununua gari hii

kinjumbi one

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
1,695
Reaction score
2,144
IMG-20170908-WA0004.jpg
habari za weekend
Wataalam wa magari, na wazoefu wa matumizi ya magari, naomba ushauri, nimeona gari ya ubalozi inauzwa aina ya vitz new model, CC 1290. ya 2007. Imeingia nchini 2014.

Mimi itakua ndo gari yangu ya kwanza. Je ipo vizuri? Au huwa inasumbua sumbua, na vp ulaji wa mafuta, vp service yake, vp uimara, na vp kuhusu ushuru, na usajili, inaweza kuwa km sh ngapi? Maana kadi naona imeandikwa diplomatic. Bei anataka usd 2800.
 
Sawa wakuu naendelea kusibiri, na siku zote wanasema subira inavuta heri
 
View attachment 589513 habari za weekend
Wataalam wa magari, na wazoefu wa matumizi ya magari, naomba ushauri, nimeona gari ya ubalozi inauzwa aina ya vitz new model, CC 1290. ya 2007. Imeingia nchini 2014. Mimi itakua ndo gari yangu ya kwanza. Je ipo vizuri? Au huwa inasumbua sumbua, na vp ulaji wa mafuta, vp service yake, vp uimara, na vp kuhusu ushuru, na usajili, inaweza kuwa km sh ngapi? Maana kadi naona imeandikwa diplomatic. Bei anataka usd 2800.
Cc 1270 unauliza ulaji wa mafuta basi nunua t-better motorcycle itakufaa
 
Mkuu, kwanza hiyo sio New Model. Hiyo ni 2nd Generation Vitz.

1st Generation ilikua 1999 hadi 2005.

2nd Generation ilikua 2005 hadi 2010.

3rd Generation ni 2010 hadi sasa.

Yako ni 2nd Generation. XP90. Inaitwa pia Toyota Yaris kwa Nchi za America.
Zipo za FWD na 4WD sijui yako ni ipi maana hujaweka maelezo yankutosha hapo.

Na pia zenye engine ya 1.3L zipo zenye engine ya 1NR-FE, 2NZ-FE na 2SZ-FE zote ni i4 na zina technology ya VVTi.

Hii gari inafanana na Belta sema Belta ni Sedan na Platz some how. Ila sana sana na Belta.

Kwa Milion 6.5 chukua tu mkuu. Bei nzuri. Ingawa body yake ni laini sana ila kwani unaenda kufanya mashindano ya kugongana? Kuhusu Maintanance kuanzia Engine ma Body, unapata spare na body parts kila mahali kwani mafundi wa Toyota na vifaa vyake wamejazana kila mahali.

Kuhusu mafuta na ulaji iko vizuri kwa hiyo engine size na performance yake sio ndogo ina range kwenye 90hp hivi. So itasua sua kidogo ukibeba watu wanne wanene katika mlima ila katika day to day activities iko vizuri.

Bado Narudia kwa hiyo bei, angalia tu accident history, hali ya gari na vitu vingine.
 
Mkuu, kwanza hiyo sio New Model. Hiyo ni 2nd Generation Vitz.

1st Generation ilikua 1999 hadi 2005.

2nd Generation ilikua 2005 hadi 2010...
Asante mkuu, kwa ushauri murua kabisa, sasa je vp kuhusu magari ya ubalozi pale tra, hakuna longolongo ktk kubadilisha umiliki? Na vp kwa bei hiyo ukijumlisha ushuru nitakaopigwa t.r.a maana si ina msamaha wa kodi, nini ushauri wako, nichukue tu?
 
Kwa ili swali naomba waje wataalamu wa kuimport. Sipo vizuri hapa kaka.
 
Kaka hiyo gari wakati ananunua alinunua second hand au mpya? Na Km ngapi imetembea?
Mbona ghali sana wakati Japan gari hiyo unapata kwa $2500 mpaka dar.

Used TOYOTA VITZ for sale | 834 Stock Items | tradecarview
Mileage 26 km, mkuu, afu hiyo ya USD 2500 including cif hadi dar, nyingi zina mileage kuanzia 60,000 huko. Alafu kuna ushuru hadi Jana, ilikua 4,800,000. Plus muda. Kumbuka hiyo gari ni ya afisa ubalozi, anakaa akiba kazini posta. Ni kweli alinunua second hand ikiwa ina mileage, 10,000, kumbuka hawa hawana ndg mikoani kusema kila desembar kiguu na njia
Ni hayo tu.
 
Asante mkuu, kwa ushauri murua kabisa, sasa je vp kuhusu magari ya ubalozi pale tra, hakuna longolongo ktk kubadilisha umiliki? Na vp kwa bei hiyo ukijumlisha ushuru nitakaopigwa t.r.a maana si ina msamaha wa kodi, nini ushauri wako, nichukue tu?

Kuhusu suala la kodi TRA, umesema hiyo gari kwa sasa inamilikiwa na afisa ubalozi; swali langu je hiyo gari ina namba za ubalozi? (zile za bluu mf T...CD...) au namba za kawaida? Tuanzie hapo
 
Kuhusu suala la kodi TRA, umesema hiyo gari kwa sasa inamilikiwa na afisa ubalozi; swali langu je hiyo gari ina namba za ubalozi? (zile za bluu mf T...CD...) au namba za kawaida? Tuanzie hapo
Ina namba za ubalozi zile za bluu.
 
Mileage 26 km, mkuu, afu hiyo ya USD 2500 including cif hadi dar, nyingi zina mileage kuanzia 60,000 huko. Alafu kuna ushuru hadi Jana, ilikua 4,800,000. Plus muda. Kumbuka hiyo gari ni ya afisa ubalozi, anakaa akiba kazini posta. Ni kweli alinunua second hand ikiwa ina mileage, 10,000, kumbuka hawa hawana ndg mikoani kusema kila desembar kiguu na njia
Ni hayo tu.
Sina uhakika saana na matumizi ya gari kwa huyo ndugu, ila kwa gari ya maika 10 kutembea km 26,000 pekee inatia wasiwasi kidogo. Maana engine imetengenezwa ili itumike. Tofauti na watu wengi wanavyofikiri, engine inayotumika ni bora zaidi kuliko engine iliyotunzwa ndani. Kuna msemo Kiingereza kwamba, If you don't use it, you lose it.
 
View attachment 589513 habari za weekend
Wataalam wa magari, na wazoefu wa matumizi ya magari, naomba ushauri, nimeona gari ya ubalozi inauzwa aina ya vitz new model, CC 1290. ya 2007. Imeingia nchini 2014. Mimi itakua ndo gari yangu ya kwanza. Je ipo vizuri? Au huwa inasumbua sumbua, na vp ulaji wa mafuta, vp service yake, vp uimara, na vp kuhusu ushuru, na usajili, inaweza kuwa km sh ngapi? Maana kadi naona imeandikwa diplomatic. Bei anataka usd 2800.
Mnada sio wa wazi? PPRA wanajua?
 
Back
Top Bottom