Ushauri: Nataka nifanye biashara hii

Ushauri: Nataka nifanye biashara hii

Zacht

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2020
Posts
1,026
Reaction score
2,266
Heri ya mwaka mpya .

Kuna kitu nimewaza kufanya lakini sijui kama nipo sawa kimahesabu kwa Sababu sio uzoefu nayo, iko hivi nimewaza nianzishe biashra ya chakula (wali) kwa kufanya partnership na mtu. Yaani namtafuta m-mama au mdada nampa mchele 90-100 kg auze. Then mimi Nitakuwa nachukua Kila siku 10k kwake kwa mwezi mmoja.

Nimepanga nifanye hivi at least kwa watu watatu niwe napokea 30k, kuhusu mchele napata wapi Mimi mwenyewe mkulima mzuri tu nalima mpunga kutoa kilo 90-100 kwa mwezi inawezekana kwahiyo nikaona badala ya kuuza mchele nifanye hivi .

Mnaonaje wadau wenye uzoefu nimewaza sawa kweli hapa?
 
Wazo sio baya ila kwa upande wa mtu utakayefanya nae iyo biashara ndo huwenda kukawa na mgogoro
 
Hapo unaenda kupigwa sema nakupa wazo la mkinga mmoja pale Mbeya , yeye alichofanya alienda kuongea na mama ntilie kama 30 , kila mama ntilie anasema oda yake yaani anaetaka kilo mbili sawa au kilo tatu sawa, mwamkinga alichofanya kila siku anawapigia simu asubuhi ajue oda zao halafu anavijana saa moja asubuhi walishapata mzigo kwa bei ya punguzo na akawa mchele anawauzia msafi kabisa, anawapa mchele asubuhi jioni anapita kukusanya pesa kwa sasa kanunua gari ya delivery na muuzani wa nyama anawapekea pia nyama kwa bei ndogo maana anachukua machinjioni direct na kusupply kwa uaminifu na kwa sasa anafanya vizuri kuliko kawaida,
 
Namtafuta mtu ninaye mfahamu kwa usalama wa biashara na Kila kitu Kinafanyika kwenye maandishi
 
Alikuwa anawauzia kwa bei ya punguzo ?
 
Kwa mfano mchele 1500 dukani yeye anawapelekea kwa 1490 ,
Ok , kwahiyo mkuu unanishauri babala ya kuwapa mchele nifanye kama huyo mkinga
 
Namtafuta mtu ninaye mfahamu kwa usalama wa biashara na Kila kitu Kinafanyika kwenye maandishi
[emoji23][emoji23][emoji23] mama ntilie ukamletee maandishi wakati anamarejesho ana michezo kama yote atakutema maana anajua wapo watakao muuzia vizur zaidi yako ww uko na shida ya pesa ndio maana unahisi ni rahisi kufanya hivyo ila tafatari zaidi
 
Ok , kwahiyo mkuu unanishauri babala ya kuwapa mchele nifanye kama huyo mkinga

Nimekupa idea yake wewe unaweza kuboresha, yaani unaposikia creative ni pamoja na kuboresha wazo la mtu mwingine lako linakua bora zaidi unapenya kwa mfano mnauza karanga za kukaanga watu wawili mwenzako kwenye karanga anapata product nyingi anauza wewe na sinia moja uliyokaanga mwenzako ana sinia tatu hadi nne moja anakaanga na maganda, nyingine anafunga mbichi, nyingine anaikaanga kawaida na nyingine akishakaanga anatoa ile cover nyekundu inabaki karanga nyeupe tu, akikua zaidi karanga ile ile anaiandaa anasaga unga anapeleka kuuza kama kiungo cha mboga hapo anapeleka sokoni huko, hivo usikopi wazo hilo hilo wewe boresha zaidi,
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mama ntilie ukamletee maandishi wakati anamarejesho ana michezo kama yote atakutema maana anajua wapo watakao muuzia vizur zaidi yako ww uko na shida ya pesa ndio maana unahisi ni rahisi kufanya hivyo ila tafatari zaidi

Kwenye biashara afanye tafiti lakini suala la kupoteza hilo hawezi kulikwepa hasa kwa biashara mpya kikubwa awe na tahadhari wakati anagawa mzigo mwanzo asigawe mzigo wa mtaji wote anawapa kidogo kidogo hadi baadae wakishaanza kuongea lugha moja anaweza sasa kuongeza ni kwenda kwa tahadhari
 
Akili kubwa
Hapo unaenda kupigwa sema nakupa wazo la mkinga mmoja pale Mbeya , yeye alichofanya alienda kuongea na mama ntilie kama 30 , kila mama ntilie anasema oda yake yaani anaetaka kilo mbili sawa au kilo tatu sawa, mwamkinga alichofanya kila siku anawapigia simu asubuhi ajue oda zao halafu anavijana saa moja asubuhi walishapata mzigo kwa bei ya punguzo na akawa mchele anawauzia msafi kabisa, anawapa mchele asubuhi jioni anapita kukusanya pesa kwa sasa kanunua gari ya delivery na muuzani wa nyama anawapekea pia nyama kwa bei ndogo maana anachukua machinjioni direct na kusupply kwa uaminifu na kwa sasa anafanya vizuri kuliko kawaida,
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mama ntilie ukamletee maandishi wakati anamarejesho ana michezo kama yote atakutema maana anajua wapo watakao muuzia vizur zaidi yako ww uko na shida ya pesa ndio maana unahisi ni rahisi kufanya hivyo ila tafatari zaidi
Nimekupa idea yake wewe unaweza kuboresha, yaani unaposikia creative ni pamoja na kuboresha wazo la mtu mwingine lako linakua bora zaidi unapenya kwa mfano mnauza karanga za kukaanga watu wawili mwenzako kwenye karanga anapata product nyingi anauza wewe na sinia moja uliyokaanga mwenzako ana sinia tatu hadi nne moja anakaanga na maganda, nyingine anafunga mbichi, nyingine anaikaanga kawaida na nyingine akishakaanga anatoa ile cover nyekundu inabaki karanga nyeupe tu, akikua zaidi karanga ile ile anaiandaa anasaga unga anapeleka kuuza kama kiungo cha mboga hapo anapeleka sokoni huko, hivo usikopi wazo hilo hilo wewe boresha zaidi,
Kwenye biashara afanye tafiti lakini suala la kupoteza hilo hawezi kulikwepa hasa kwa biashara mpya kikubwa awe na tahadhari wakati anagawa mzigo mwanzo asigawe mzigo wa mtaji wote anawapa kidogo kidogo hadi baadae wakishaanza kuongea lugha moja anaweza sasa kuongeza ni kwenda kwa tahadhari
I thought it would be a simple idea.... kweli nimeamini kitu kinakuwa rahisi na kinaoneka kinawezekana ukijadiri kichwani kwako😆 .

Ngoja niumize fuvu kufikiria vizuri inaweza kuwa idea nzuri
 
Back
Top Bottom