Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Ni wazo zuri kama pesa ungekuwa umesave mwenyewe lakini ya kukopa ndugu yangu kwenda kuanzisha biashara mpya, bila kujua changamoto zake sikushauri uache kazi, badala yake, tafuta kimtaji chako kidogo jaribu kufanya hiyo biashara ambayo unataka kufanya jaribu hata kwa mwaka hivi utakuwa umejifunza, hapo unaweza kukopa kuongezea kwenye biashara na kuacha kazi.

Mimi nilifikia hatua ya kuacha kazi baada ya miaka 6 kazini, sikuona mabadiliko yoyote kwenye maisha yangu, mwisho niliamua kuacha kazi, wakati nimeacha nilikuwa nimesave kama milion 3 zangu peke yangu, nikauza mpaka vitu vya ndani kuongezea mtaji, nilijitesa ndani ya miezi 6 mambo yakaanza kunyooka. Toka nimeacha kazi nina miaka 2 niliacha sina hata kiwanja, lakini sasa ni nyumba 1 na viwanja 3, watoto wanakula, shule wanakwenda, biashara imesimama, account inasoma, Natembelea miguu minne, nina muda wa kutosha kufanya mambo yangu, nimetengeneza ajira zaidi ya watu 15. Ninatoa amri mimi wala hakuna wa kunipangia. Maisha ya kitumwa nilishatoka. Karibu sana ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kukopa hapo me ndiyo naona tatizo labda sababu ni mwoga mikopo... ni hivi biashara unayoenda kuanza kuna changamoto zipo hasa kwa mnao anza ila kama umeshajua namna ya kuziepuka jilipue na mkopo
 
Kwa uwelewa wangu nihivi usikope mkopo kwa ajili ya kuanzisha biashara ila kopa mkopo kwaajili ya kuendeleza biashara,,mkuu usiache kazi mpaka uhakikishe umeanzisha biashara na kumudu changamoto zake kisha ukiona hapa sasa sinashaka na hich nnachokifanya ilikutafuta mianya zaidi yakibiashara ndo ujilipue na uingie kusimamia biashara zako.Sababu hiyo milion 10 unaweza ukaiona kubwa ukaacha kazi kutokana na bado huna na hujapata changamoto za kibiashara ukaiona ikiteketea bila kujua,na nyumban pesa hakuna aisee utamtafuta mchawi nani wakati ni wewe mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujiajiri ni wazo zuri sana, siyo rahisi kufanikiwa maishani kwa kutegemea ajira.

Siwezi kusema idea yako kama ni nzuri au laa, watu huwa wana suggest kukopa kuendeleza biashara na siyo kuanzisha biashara.
Ila sometimes mtu huna option hiyo. Hatujui ni biashara gani unataka kuanzisha, au hata wewe una nidhamu kiasi gani kwenye hela, maisha na biashara, so kukwambia ufanye au usifanye ni kubahatisha.

Mimi niliacha kazi mwaka jana mwezi 7 na kuanzisha kampuni yangu. Mwanzo huwa ni mgumu, hasa kwa sababu ya expectations.
Ukiwa una plan biashara huwa tuna assume baada ya muda flani itaanza rudisha hela, mara nyingi haiwi hivyo.
So ushauri wangu, kuwa realistic kwenye expectations na pia like me nilinunua bodaboda kuingiza hela za kula nikiwa napambana na kampuni (ingawa bodaboda nayo inataka dereva mzuri, luck for me, wangu azingui)
All in all, panga, pangua, panga tena, kuwa na plan B na tafuta muda kwa namna yoyoye ile do research. Jifanye mwehu tu, zunguka uliza watu depending na biashara unayotaka kufungua.

Watu wengi wenyeelimu au waajiriwa tuna fail kuingia kwenye biashara kwa sababu tuna overthink. Tunawaza mno, tuna run scenerios nyingi, mara nyingi either zina tukatisha tamaa au tuna poteza interest, unakuja kushtuka darasa la 7 anakupita kimaendeleo.

All the best aisee. Biashara ndo mpango mzima. So far sijutii kuacha kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafanya kazi gani?acha ufanye hiyohiyo kwa kujiajiri mwenyewe bila kutumia mahela yote hayo .

Core investment yako isiwe Pesa,wekeza ujuzi wako.ukiwekeza kwenye pesa hatari ya kutopata ni kubwa.Inakua inabadilika badilik kulingana na nyakati za kisiasa.
 
Wazo zuri ila utekelezaji ili kufikia lengo ndo kazi, watu waliofanikiwa kwa kujiajiri walianza taratibu na kupitia changamoto kadhaa kabla ya kusimama, hivyo achana kwanza na picha ya kufanikiwa baada ya kujiajiri, jipange kwanza , fanya utafiti wa hicho cha kujiajiri na anza taratibu na ;ikiwezekama anza kabla ya kuacha kazi
 
1_Ukikopa dhamana ya mkopo ni nini? Mshahara au nyumba? Au una mtu wa kukudhamini?
2_Je biashara unayopanga kuanzisha itaweza faida ya kutosha kulipa kodi za TRA,Leseni ya biashara,ushuru,pango la chumba cha biashara na gharama nyingine?Maswali haya ni muhimu ujiulize.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni hela kubwa sna kama ukijipanga vizuri unachomoka na unaacha kazi hiyo ya mateso isiyo kuvusha mahala. It seems kazi yako ni hand to mouth. Binafsi nilikua kama ww nikaamua kujitoa mhanga nikaacha kwa mtaji huo. Maisha yangu leo kila niliokua nao kazn wananilia

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio umuongoze apite ulipopita
 
UKIKOPA na KUACHA KAZI huo mkopo utaulipaje? Si unatafuta kuolewa wewe?
Fanya hivi kama unakopa kwa kutumia mshahara hilo ni ruksa. Hiyo pesa iwekeze kwenye biashara. Ukifanikiwa kuendesha hiyo biashara baada ya mwaka mmoja bila kuyumba yumba ndipo ufikirie kuacha kazi. Kujiajiri sio rahisi kama watu wanavyosema...
Mtumishi wa serikali anakopa kwa kutumia mshahara mkuu.
Maswali mengine majibu yake yapo kwenye post yangu humo humo
 
mkuuu subir kwanza mkulu ataleta mambo mazur kwa watumishi 2 unaweza ukaacha afu badae biashara zkagoma afu nako mkulu ndo katema mambo mazur kwa watumishi kwaiyo vumilia tu mkuu
 
Swala hapa ni kua Biashara unayotaka kuifanya bado hujaijua ni Biashara gani, pili hujajua Changamoto zake etc,
What if ukope ufanye hiyo Biashara then igome??
 
Mkuu kazi mbaya ukiwa nayoooo..... Husiache kazi mkuu... tafuta njia mbadala za kukuongezea kipato lakini sikushauri kuacha kazi!!!! Raisi mwenyewe na kazi yake ya Uraisi ana miradi yake binafsi ya kumuongezea kipata.. so who are you kutokuanzisha michongo yako ya pembeni maisha yasonge..! Umiza kichwa mzeeee aliesema ugumu wa maisha ndio kipimo cha Akili hakukosea!
 
mkuuu subir kwanza mkulu ataleta mambo mazur kwa watumishi 2 unaweza ukaacha afu badae biashara zkagoma afu nako mkulu ndo katema mambo mazur kwa watumishi kwaiyo vumilia tu mkuu

hahahahahah mzeee unamahope ya kizembeeeeee.... hahahahah ajira kweli utumwa haki ya nani...
 
Back
Top Bottom