ushauri: nataka nirudie mwaka kwa kudrop computer engineering niende civil

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Heshima kwenu wanajf!
Nasoma bachelor of computer engineering chuo kimoja hapa tz na mwezi wa kumi nategemea kuingia 2nd year!
Mwanzoni niliipenda sana hii computer engineering (na nna matokeo mazuri sana sababu semister ya kwanza somo la mwisho nilikuwa na B tena moja tu) japo kwa sasa mazingira yake tanzania hayaridhishi sana maana ukiangalia hata wanafunzi wengi field wanakosa na pia masomo yake na kazi zake baadae hazina tofauti sana na za IT na computer science ambazo kuna utitiri mwingi sana wa vyuo wanavyotoa hizo kozi za IT na comp. Science!(so kuna watu wengi sana)
Kiukweli nikiingalia civil naona kama ina future ndefu japo siijui kiundani saaana!(ntaomba mnieleze ikoje i.e ajira, uwezo wa kujiajiri, soko e.t.c)
wazo langu ni kurudia mwaka wa kwanza but by this time niwe nasoma civil!
Sasa naomba anayeelewa kuhusa yafuatayo naomba anielekeze pia!

I) Uongozi wa chuo watakubali?
II) Bumu litakuwaje? Au ndo heslb watanimwaga?(japo wakikubali kwa miaka 3 halafu ule wa mwisho nitafute mwenyewe nitakubali)
III) kwa mwenye ushauri kuhusu huu uamuzi kama ni sahihi au sio sahihi(according to yeye) ntaomba pia niupate ili nikae niangalie nijue kuwa mwezi wa kumi narudi na mawazo gani chuoni!

Ahsanteni!
 
Una mawazo mazuri sana, ila sijui taratibu za bodi ya mikopo, subili waelewa watakujuza, lazima unaposoma sasa hivi uwe na mission na vision.
 
Ndio tatizo la wajivuni wanapenda kwenda cit,te,ee,ep kwa coet ni ngumu sana kuhama kozi labda baba yako awe na cheo ccm,civil nayo majanga kuanzisha kampuni msing mkubwa nenda kasome sua au mati kilosa au ukishindwa nenda chuo cha nyuki manyara uungane na pinda.
 
Aah bra angalia sehemu ambayo unaweza kujiajiri mwenyewe na inanafasi kubwa ya kuwasiliana na customers mengine mm sijui masuala ya loan
 

Civil Engineering ni fani nzuri. ajira na soko lake ni pana.
 

Umejiuliza ni kwa nin unakua na hayo mawazo sasa ivi?? Kwanin haikua wakat unaanza mwaka wa kwanza?? Na je ukibadil koz unadhan utapata tena mkopo?? Na usipopata nyumban mnajiweza?? What if ukidrop mwaka na ukakosa nafas ya civil?? Look here brother hiyo ni koz nzur na nna was was hayo mawazo umeyapata toka kwa marafiki au ugum ulioupata pindi unasoma!!! Ambapo zote hizo sio sabab sahih za kuairisha mwaka!!! Chaguo ni lako mkuu ila kua makin na maamuz yako maana yatagharim future yako...
 
Kama upo UDSM sioni mantiki yakubadili fani na kuwa Civil Eng. Endelea tu na fani yako kwani soko ni kubwa jifanyishe bidii tu uweze kudesign systems..Kwenye kampuni za consulatancy unaingia kama service Engineer so komaa na shule tu..unless kama una problem nyingine e.g kudisco maana mawazo yako yanafanana na mtu aliyedisco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…