sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,001
Salaam wakuu,
Nimefanya kazi huku mjini kwa miaka10 saivi. Bado sina ndoa japo umri unaruhusu kufanya hivyo. Huku mjini sijafanya uwekezaji wamaana kutokani na changamoto za gharama za maisha kuwa juu.
Nahisi nalipa kodi kubwa kuliko watanzania wenzangu wakijijini kwani huku mjini kila ikianza siku lazima pesa itumike kwa mahitaji mbalimbali.
Katika siku zahivi karibuni nimejikuta nikitamani kurudi kijijini kwa wazazi wangu nikafanyie kazi huko kwani taasisi ninayoitumikia ina ofisi zake kule kijijini pia.
Kwa mtazamo wangu naona kuwa kwangu itakuwa rahisi kutoboa kimaisha kwani kijijini Kuna rasilimali nyingi muhimu ambazo naweza kuzibadilisha kuwa fedha. Kuna ardhi nzuri na maji yakutosha, vyote hivi nivya bure.
Je, kabla sijachukua uamuzi huu nijipange kwa changamoto zipi labda?
Au wazo hili litakua na faida kwangu kwa angalau asilimia 90?