Uchaguzi 2020 Ushauri NEC: Wekeni Sheria Mgombea atoe ahadi anazoweza kuzitekeleza miaka 5 tu

Uchaguzi 2020 Ushauri NEC: Wekeni Sheria Mgombea atoe ahadi anazoweza kuzitekeleza miaka 5 tu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Tunapokuja kupiga kura tunaingia mkataba wa miaka mitano na tunayempigia Kura. Mwisho wa miaka mitano tutapima aliyisema atafanya na Mapya atakayofanya tena.

Kwa nini nawaza hivi.
Kuna mbunge wa jimbo flani Yeye amekuwa anaahidi zahanati. Miaka 20 sasa ni mbunge lkn kila baada ya miaka mitano anajenga kidogo alafu anasema mnichague nimalizie. Mchezo huohuo hadi katoboa miaka 20.

Sasa hata kwa urais. Wanapaswa kufanya mambo makubwa mengi bila sio nje ya walichosema watafanya kwa miaka mitano. Au wayafanye baada ya kumaliza waliyosema watafanya.

Pia wasiseme naombeni kura nimalizie nilichoanzisha Bali naombeni kura nifanye yafuatayo miaka mitano ijayo kama nilivyofanya yafuatayo miaka mitano iliyopita.

NEC kuwabana kisheria hivi wagombea kutasaidia wao kujielekeza kwenye mkataba wetu tulioingia nao kwenye Box LA kura. Pia kutailetea heshima nchi kwa kupunguza siasa za ulaghai
 
Itapendeza Sana maana kila wakati wa uchaguzi wanakuja kutuambia "Najua hapa Kuna shida ya maji hivyo mkinipa kura nitashughulikia shida hizi" Mara waseme shida zenu nimezibeba nitazifanyia kazi, mara nawapenda sana sitawaangushusha, mara watupigie magoti. Ila baada tu ya kuchaguliwa wanajifanya miungu watu
 
Itapunguza usanii
 
Back
Top Bottom