Ushauri: Ng'ombe wa Maziwa na Maksai

Heaven Seeker

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2017
Posts
479
Reaction score
1,071
Heshima kwenu ndugu Wafugaji na Wakulima.

Kama mjuavyo, shughuli za Kilimo na Ufugaji ndizo kazi zetu za Asili tulizorithishwa tangu zama za Adam na Eva.


Sasa wakuu nisiwachoshe, mwenzenu nataka niwachukulie Wazee - Ng'ombe mmoja wa Maziwa mwenye mimba na Maksai wawili kwa ajili ya shughuli za Kilimo huko Mwanza. Lengo ni kupunguza kidogo utegemezi ili angalau kwa mwezi wawe wanajipatia vijisenti vya hapa na pale.

Naombeni ushauri mkuu kuhusu wapi naweza kuwapata kwa Mwanza. Itapendeza zaidi nikijua gharama zake pamoja na changamoto nazoweza kukumbana nazo.

Karibuni kwa ushauri Wakuu.
 
Ndugu Mungu akujaalie ufanikiwe ktk hilo maana kuwatunza wazazi ni jambo jema sana ktk maisha yetu, mtumainie Mungu nae atakuonyesha njia iliyo bora ktk kulifanikisha hilo. Wajali wazazi na kuwatunza maana nao walikutunza ktk njia iliyo njema, barikiwa sana ndugu.
 
Amina Mkuu. Huwa ni shauku yangu kuwaona Wazee wanakuwa na furaha kwa siku zao za hapa duniani zilizosalia.

Suala la uchumi wa Familia ni kichocheo kimojawapo ktk kusababisha hiyo furaha! Ni ngumu kufikia at the maximum level, lakini naamini kilicho ndani ya uwezo kina stahili kufanyika.

Binafsi huwa sijisikii vizuri endapo mie nitakuwa nalala sehemu nzuri na ninakula chakula kizuri, huku Wazee wakiugulia maumivu ya ufukara moyoni. Ni bora wao wapate kwanza kisha mie nikafuatia huko mbeleni.
 
Utukufu kwa Mungu juu, 🙏. Ibada mjema sana hii kuwatunza wazazi wetu, nakuombea Kwa Mungu lifanikiwe hilo kwa mapenzi yake mema.
 
Mkuu. Hawa Ng'ombe kwa hapa Bongo wanapatikana kweli?

..mkulima smartintiatives / shamba darasamkusi wanasema wanao ng'ombe wa aina nyingi ikiwemo Fleckvieh.

..pia wametoa namba zao za simu kuwa ni 0764915692 na 0713178868.

..yeyote atakayewasiliana nao aje kutupa mrejesho kuhusu huduma zao, kama ni nzuri, au la.

..sikiliza tangazo lao hapo chini.


cc balimar
 

Nakushauri uwanunulie ng’ombe chotara yani cross breed. Kwa uzoefu wangu, hawa ng’ombe wa kizungu wanahitaji uangalizi makini sasa kwa hali zetu, ni rahisi kuingia hasara kwani kupe ni adui namba moja.

Binafsi nimefuga chotara na wanamudu hali yetu ya mazingira vizuri tu huku maziwa pia nikipata kwa ufasaha.
 

..unaweza kutufafanulia ng'ombe wako ni chotara wa mbari gani?

..pia ng'ombe wa kizungu aliyekupa shida kumtunza alikuwa wa mbari gani na alikupa shida gani haswa.

..vipi kuhusu kiwango cha maziwa cha ng'ombe chotara? walikuwa wanakupatia maziwa kiasi gani?

..mwisho, tunaomba bei na mahali uliponunulia ng'ombe chotara.
 
..maelezo ya mfugaji aliyeko Kenya kuhusu ng'ombe aina ya Jersey.

..ng'ombe huyo anasifika kwa kutoa maziwa yenye "fat content" kubwa.




 





Hawa ng’ombe wangu ni chotara kama unavyowaona.
 

Attachments

  • IMG_1623.jpg
    249.1 KB · Views: 45
..wako vizuri.

..umechanganya mbegu gani?


..wanakupa maziwa ya kutosha?

Maziwa ya kutosha sana tu. Sema mimi niliwanunua mnada ni hivyo historia yao ya originality sina. Kwa sasa nimeamua wapandwe na wa kienyeji ili kuimarisha ustahimilivu yao, kwasababu ukiwaangalia kwa asilimia 85 ni wa kizungu so ukibalance, wanazaa 50/50 chotara. Hao wanakuwa ng’ombe wazuri sana.
 
Ahsante sana Mkuu. Unaweza kutusaidia kuwa wanatoa lita ngapi kwa siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…