Ushauri: Nichukue gari ipi kati ya hizi?

Nikuongezee maelezo----Umesema umewajengea wazazi kijijini, maana yake utakuwa unawatembelea at times.... Naamini kwa infrastructure zetu, na kwa budget yako; gari za Mjapan zinakufaa zaidi...
Nimekuwa na Rav 4 kwa takribani miaka 7 sasa, 2006 model---Nakuhakikishia hautojutia!
Now nimeichoka, natamani iharibike inilazimishe kuibadilisha, sioni dalili.
 
Kwa hiyo budget yako go for Kluger,Toyota Prado,RAV4,Vanguard au Suzuki escudo.

Na kama utanunua brand ya Toyota never usinunue kutoka beforward kwani huwa wanauza magari ya Toyota ambayo yameshatumika sana.Beforward ni wazuri kwenye brand nyingine ila siyo kwa Toyota.Huwa wanauza magari yaliyotumika sana ya Toyota kwa sababu demand ya magari ya Toyota ipo juu.
 
Toyota is ok. Lakini kwa harrier hapana mkuu. Tena ukinunua nyeusi ukiipaki mahali unaweza sahau yako ni ipi
Upo sahihi ni kweli ni mengi ila umejiuliza kwann ni tatizo yakiwa mengi?
Unless unakwepa vitu kama wizi wa spear au wewe ni mtu wa kukimbizana na fashion wingi wa harrier si kasoro ya msingi .
 
Asante sana kaka, nachukua ushauri wako mafuta si shida km itakua shida basi si-deserve kuwa na gari
 
M
Mtoa mada ina maana umejenga nyumba zote hizo ukiwa unakwea bodaboda? Kuna kama ka chai flani hivi. Unless hizo nyumba ziwe unga unga mwana ila mtu anayejenga nyumba mbili za kawaida hawezi kosa hata IST maana bei yake ni kama Tiles za nyumba moja tu
Mkuu asante kwa maoni yako...pia naheshimu mtazamo wako.
 
Yes gari kubwa kwa wakubwa
 
Hivi kutuelezea kuwa umejenga mjini na kijijini ina uhusiano gani na hitaji lako la gari?

wewe unadai ni mkubwa ila bado mshamba, acha ushamba halafu jiamini, haya sasa ndio nakushauri, nenda kanunue VW,achana na hizo toys ulizoorodhesha hapo.
Kueleza mafanikio sio dhambi mkuu.
Kwa taarifa yako washamba/maskini ndio huficha taarifa ya mambo yao.
 
Mtoa mada hongera kwanza kwa kupambana na mpaka kufikia ulipo...

Kwa kuwa umeamua kuwa na SUV chipi hapa ndio ushauri wangu....

Binafsi nimeshatumia RAV 4 2006. Ilikua gari nzuri na imara. Issue yake kubwa ni lile tairi la nyuma ukiendesha sana rough roa inaulegeza ule mlango.

So sipendelei tairi la spair kukaa nyuma.

RAV 4 ya 2008-2010 ni nzuri tairi imeingizwa ndani na gari ina muonekano mzuri. Pia kutokana na bajeti yako kuwa mwisho 40m basi hizo zitakufaa....

Don't go for other brand out of toyota na nissan (mimi nilikuja kuopt for Dualis coz of budget).....

Go for TOYOTA RAV 4 2008-2010

Kuhusu site ya kuchagua ni moyo wako tu wa uvumilivu kutafuta mtandaoni..... Wote wana magari mazuri ila uwe mvumilivu na utenge muda wako ku search mtandaoni....

If you don't mind na kuondokana na usumbufu kuna vijana wanafanya hiyo kazi siku hizi. Unawalipa wanakuagizia mpk kufanya clearance na usajili..... (Nilitumia option hiyo baada ya kuchoka kutafuta mtandaoni).....

Good lucky
 
Yes kwa za zamani. Ni roho ya paka. Kuna ndugu yangu alinunua extrail new model ina namba D . saivi iko nyanga nyanga. Rav 4 namba c mpaka sasa inadunda
 
Mimi ushauri wangu chukua Rolls Royce ila uwaambie kabisa wakuwekee matairi mapya.
 
Sasa mkuu mtu akiniagizia gari nitakuwa na uhakika gani na ubora wa gari hiyo?Si anaweza kunichagulia ambayo imechakaa sana?Si anaweza kunichagulia ambayo imeenda kilomita nyingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…