Mkuu PCB ni combination ambayo naiheshimu sana kutokana na kusoma karibu masomo yote ya sayansi, actually ni PCB na M - au siku hizi some la hesabu alifundishwi tena kama subsidiary ukweli hakuna cha subsidiary wala nini unasoma hesabu kweli kweli.
Ushauri wangu ni kwamba si vigumu kusoma Physics, Chemistry na hesabau kwa kuwa masomo hayo yote yana formula i.e mathematical intensive save Organic Chemistry, kibembe kiko kwenye some la Biolojia, hilo mkuu unapashwa kusoma kama mtu anaye soma somo la Historia, nikukalili tu hakuna jinsi.
Ujikite sana kufanya mazoezi kwa kujibu maswali ya past papers, wana kawaida ya kurudia rudia maswali wanabadilisha kidogo hapa na pale lakini ukiangalia kwa makini na yale yale tu, don't you slack katika kufanya mazoezi mara kwa mara hasa somo la Biolojia, kitu kingine uwe makini sana kwenye somo la practicals za mwisho mwisho kabla hamjafanya mtihani wa mwisho, mara nyingi walimu huwa na kawaida ya kuwapa practicals ambazo wanajua zitakuwa kwenye mtiani wa mwisho i.e kumaliza form six lakini awambii sasa husipokuwa makini ukasepa kwenda kusikiliza miziki ya Bongo/Diamond utaharibikiwa - U have been warned mkuu so take care. Goodluck.