Mkuu unaweza kujenga lakini nikwambie kitu kimoja, moja ya kitu ninachokijutia ni kutumia pesa kujenga nyumba katika hatua za mwanzo za maisha yangu, ningeambiwa nirudie maamuzi kwa kiwango cha pesa nilizotumia ningenunua kiwanja nikakiwekea alama alafu pesa nyingine nikanunue mashine mbali mbali, return ya nyumba ni ndogo sana ukilinganisha na pesa ya ujenzi. Alafu ukijenga kwa kutumia mafundi wasio wasomi hawawezi kukadiria gharama, ukianza kujenga ndio utasikia mara hiki mara kile.Utakuta mtu anapata kodi ya laki nne au tano kwa mwezi nyumba kaijenga kwa millioni sabini mpaka mia.Yaani hapo pesa itarudi baada ya miaka kumi na tano. Million sabini mpe muhindi au mchina uone baada ya miaka mitatu atakua wapi?Ninamshukuru mtu mmoja nilipotaka kununua aina fulani ya gari yangu ya kwanza alinishauri kutokana na pesa zenyewe za manati ninunue gari ndogo pesa nyingine ninunue mashine au kitu cha kuniingizia pesa zaidi. In real world some assets are not real assets are liabilities.