uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
Habari wadau naombeni msaada au ushauri.
Mimi sio mzoefu na mambo ya kesi na wala sijawahi kusimama kizimbani. Kuna mtu aliniomba nimsaidie kuna sehemu wanakopesha pesa bila dhamana yoyote yenye thamani isipokuwa mdhamini mmoja so akanambia ana shida na yeye amedhamini watu wengi pale kwahiyo hawawezi kumkopesha hivyo nikamkopee pesa yeye aongeze mtaji kwenye biashara yake, nikamkopea akaanza kurejesha
Siku ya kwanza mpaka akakimbia tukamtafuta tutamkosa sasa mkopeshaji ananidai mimi na mimi ndo niliekopa na pesa ya kumlipa sina.
Niliongea nae nimlipe kidogo kidogo akagoma hivyo amepeleka madai mahakamani, nimeitwa kesho tarehe 18 sijui naanzia wapi na hata kujielezea mahakamani sijawahi
Naombeni msaada wenu wa ushauri nifanyeje au msaada wa sheria naepuka vipi hii ili iwe nafuu kwangu.
Nenda kifua mbele hawawezi kukufanya kitu ila Kama unayosema ni ukweli, utalipa hata buku buku kwa mwezi!
Anakutisha tu na mahakama, Hakuna wauwaji kule!
Ingawa sielewi:
1. Unachukuliaje mtu mkopo?
2. Umeweka Dhamana vitu vyako?