Ushauri: Nimeagiza Valeur ndogo nimeletewa Viceroy na nina buku 5 cash. Mhudumu ni pisi kali niliyokuja kuilia misele niombe namba

Toa namba nije na askari waliovaa sare tukubebe
Nikibebwa mzobe babu si nitakua nimeharibu bora kuandikisha simu asee. Manjagu wenyewe hawaaminiki skuiz wanaweza kukuchuna ngozi na asiwepo wa kujua ulikopotelea. Wananjaa ya wahalifu siwaamini
 
Ipo wapi hiyo pub nipo hapa buguruni.. ukinijibu nakuja fasta hapo na boda nakuokoa kwa kukulipia na manzi tunang'oa..
 
Toa namba nije na askari waliovaa sare tukubebe
Haha,
Sasa hiyo pesa ya kununua hao askari si umrushie tu maana anayohitaji ni pungufu ya 10k tuu.

Halafu, kituo cha polisi unaingia bure ila unatoka na mpunga, na kwa kuwa hana ataozea humo😂

Ila tuwe wakweli, nyeg zinatesa sana vijana. Unaendaje bar na 5k kisa manzi, afu unaagiza na pombe kabisa!! Huyo demu utaweza gharama zake?!!! Maana kuchakata siyo bure
 
Kuna dem ukimuona tu moyo unakwambia usinuache hata kama huna hela. Ndo kilichonikuta.

Kuna msanii bongofleva kaingia hapa, naona jamaa kachill kwa pembeni na hajaagiza chochote. Ngoja nimsalimie ka vipi nisome mazingira ya kumuelezea
 
Unaendaje kuomba namba ya mhudumu halafu ni bar na mfukoni una 5K?

Kijana mbona unajitengenezea future ngumu sana?, mfukoni una 5K unataka pombe na mwanamke...
Leo nilikua nataka namba tu,
Mkuu mimi sio mtu wa shida za kushundwa kutoka na manzi, kuna challenge napitia ila zitaisha sasa nimeona niwe na namba mambo yakikaa sawa ndo nitamvuruga
 
Agiza kunywaji kingine kunywa kidogo andika kama unaongea na simu.. bill utakuja kulipa kesho
 
Huyu Msanii nae hajaagiza mtungi, naona kaletewa wali nyama tu. Anakula huku anachati kala kipensi
 
Agiza kunywaji kingine kunywa kidogo andika kama unaongea na simu.. bill utakuja kulipa kesho
Hii naona inaweza kunitoa, japo nawaza sana nikistukiwa. Pub moya mabaunsa naona kama wanausongo na kazi balaa
 
kunywa ukishalewa fanya furugu kuwa mbogo usishikike huku ukipiga kelele kuwa umebadilishiwa kinywaji!! timbwili liwe zito ukizubaa utaacha nguo hapo shauri yako..🤣
 
Hhaha, wejamaa me nataka kuonekana smart boy ning’ow mtoto wa kimanga huyu. Tulia kuna mwana kaja nimekaa nae, ila sasa kaagiza maji tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…