Ushauri: Nimeagiza Valeur ndogo nimeletewa Viceroy na nina buku 5 cash. Mhudumu ni pisi kali niliyokuja kuilia misele niombe namba

Ushauri: Nimeagiza Valeur ndogo nimeletewa Viceroy na nina buku 5 cash. Mhudumu ni pisi kali niliyokuja kuilia misele niombe namba

Natokaje hapa, ndo ushauri ninaohitaji.
Hapa jirani kuna pub mpya imefunguliwa mwezi sasa, kuna pisi za hatari …. kuna hii moja juzi nilikuja ikanichekeachekea leo nilikuja mahsusu kwa ajili ya kuomba namba nikasema nizuge na Valeur ndogo nina buku tano tu. Sa kaleta Viceroy ndogo na nimechungulia menu hapa bei yake ni 10,000.

Sikujua, kanifungulia na nimeshapiga puff zangu kadhaa hapa ndo nashtuka. Serious, nahtaji ushauri wanangu. Sina issue na namba kabisa nishachanganyikiwa, nataka namna ya kutoka tu. Sina kitu kabisa
Ipo wapi hiyo pub nipo hapa buguruni.. ukinijibu nakuja fasta hapo na boda nakuokoa kwa kukulipia na manzi tunang'oa..
 
Toa namba nije na askari waliovaa sare tukubebe
Haha,
Sasa hiyo pesa ya kununua hao askari si umrushie tu maana anayohitaji ni pungufu ya 10k tuu.

Halafu, kituo cha polisi unaingia bure ila unatoka na mpunga, na kwa kuwa hana ataozea humo😂

Ila tuwe wakweli, nyeg zinatesa sana vijana. Unaendaje bar na 5k kisa manzi, afu unaagiza na pombe kabisa!! Huyo demu utaweza gharama zake?!!! Maana kuchakata siyo bure
 
Kuna dem ukimuona tu moyo unakwambia usinuache hata kama huna hela. Ndo kilichonikuta.

Kuna msanii bongofleva kaingia hapa, naona jamaa kachill kwa pembeni na hajaagiza chochote. Ngoja nimsalimie ka vipi nisome mazingira ya kumuelezea
 
Unaendaje kuomba namba ya mhudumu halafu ni bar na mfukoni una 5K?

Kijana mbona unajitengenezea future ngumu sana?, mfukoni una 5K unataka pombe na mwanamke...
Leo nilikua nataka namba tu,
Mkuu mimi sio mtu wa shida za kushundwa kutoka na manzi, kuna challenge napitia ila zitaisha sasa nimeona niwe na namba mambo yakikaa sawa ndo nitamvuruga
 
Agiza kunywaji kingine kunywa kidogo andika kama unaongea na simu.. bill utakuja kulipa kesho
 
Huyu Msanii nae hajaagiza mtungi, naona kaletewa wali nyama tu. Anakula huku anachati kala kipensi
 
Agiza kunywaji kingine kunywa kidogo andika kama unaongea na simu.. bill utakuja kulipa kesho
Hii naona inaweza kunitoa, japo nawaza sana nikistukiwa. Pub moya mabaunsa naona kama wanausongo na kazi balaa
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    366.5 KB · Views: 4
kunywa ukishalewa fanya furugu kuwa mbogo usishikike huku ukipiga kelele kuwa umebadilishiwa kinywaji!! timbwili liwe zito ukizubaa utaacha nguo hapo shauri yako..🤣
 
Hhaha, wejamaa me nataka kuonekana smart boy ning’ow mtoto wa kimanga huyu. Tulia kuna mwana kaja nimekaa nae, ila sasa kaagiza maji tu
 
Back
Top Bottom