Ushauri: Nimegundulika kuwa na High Blood Pressure. Je, nifanyeje kuhimili hali hii?

Ushauri: Nimegundulika kuwa na High Blood Pressure. Je, nifanyeje kuhimili hali hii?

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
4,700
Reaction score
1,087
Habari wadau,

Jana nimepata wakati mgumu sana ambao sijawahi kushuhudia kabla, pale nilipofika nyumbani kwangu nikiwa salama salmini,lakini cha kushangaza hali ilibadilika ghafla na kuwa nusu kifo.

Nilipigwa na giza nene ambalo sikujua limetoka wapi nikaanza kuhisi kizunguzungu na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hayajawi kunipata!

Nilivumilia mpaka asubuhi ya leo tarehe 15/07 ndipo nilipowahi hospital na baada ya kufanyiwa vipimo vyote nimegundulika nina tatizo la BP ya kupanda, Daktari ameniambia hata hivyo ni bahati kufika asubuhi nikiwa hai, nimeshtuka sana.

Je, wadau nifanye nini ku-control hili tatizo? Na chanzo chake huwa ni nini?

Nawasilisha
 
Domy

MziziMkavu tafadhalipita huku!!! sina utaalamu wa afya mkuu, ila pole sana japo huu uzi ungepekwa kule madokta kulee!! Pole sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
Domy

Nenda hospital
Utapewa ushauri na vipimo muhimu kufahamu pressure kubwa imeathiri vipi viungo vya muhimu mwilini mwako
matibabu ni dawa,mazoezi na kuzingatia masharti ya chakula bora(wanga kidogo,mboga mboga kwa wingi,matunda kwa wingi na kupunguza mafuta na chumvi ktk chakula,punguza kilevi kama unatumia)
 
Last edited by a moderator:
Pole ,Nini ushauri wa daktari kutokana na hali hiyo..pia nakushauri tembelea jukwaa la Doctors
 
Pole, endelea kufuatilia ushauri wa daktari na dawa alizokuandikia. HBP yaweza kusababishwa na factors nyingi sana... So ili kujua ya kwako imesababishwa na nini, fanya vipimo na utagundua source. Otherwise Mungu akupe uzima na afya.
 
umri tafadhali lakini ni muhimu sana kuzingatia aina ya maisha ambayo hayakupi stress pili kama unatumia vitu kama sigara na pombe ni muda wa kiviweka mbali kwa sasa, tumia sana vitunguu saumu anza na vipunje viwili viwili mpaka vitatatu ukiona shica unaweza kuanza nia kimoja kimoja mara tatu asubuhi mchana na jioni. Pata muda wa kumpumzika na ni vizuri kutamfuta daktari bigwa anakuwa anakuangalia. Lakini haya ni magonjwa yanayotokana na aina ya maisha ambayo sio rafiki kwa mwili, ulaji usizingatia mlo kamili matunda, protein na hamirojo na wanga ni vyema ujipatie mlo kamili kila siku.
 
Nenda hospital
Utapewa ushauri na vipimo muhimu kufahamu pressure kubwa imeathiri vipi viungo vya muhimu mwilini mwako
matibabu ni dawa,mazoezi na kuzingatia masharti ya chakula bora(wanga kidogo,mboga mboga kwa wingi,matunda kwa wingi na kupunguza mafuta na chumvi ktk chakula,punguza kilevi kama unatumia)

Asante mkuu,vipimo wamechukua lakini nimeambiwa nirudi tena kesho kwa ushauri zaidi!
 
Kama ulienda hospital hukupewa ushauri huko kwani?.anyway..kama umegundulika una pressure ya juu(sijajua ilikuwa juu kias gan kutoka kiwango cha kawaida).ushauri ni kupunguza stress.kupunguza matumiz ya chumvi(muhimu sana )kutovuta sigara.kupunguza pombe..kufanya mazoez..kama pressure haiko juu sana hivyo wakat mwingine hutosha kuiweka sawa..ila kama iko juu sana dawa pia ni muhimu..sikuzote za maisha yako pamoja na hiyo lifestyle hapo juu..ni muhimu kwenda hospital na kufanya uchunguzi wa awali wa afya kwa jumla juu ya baadhi ya vipimo muhimu kwa mgonjwa wa pressure..zingatia pia kupima mara kwa mara..so nenda hospital upate elimu zaidi juu ya ugonjwa wenyew
 
Wakati fulani nilipatwa na tatizo kama hilo, daktari alinishauri yafuatayo:
1. Pata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala
2. Kunywa maji mengi ya kutosha.
3. Have fun ili kupunguza stress.
4. Kama una mwili mkubwa punguza uzito.
5. Fanya jogging, angalia vipindi vya vichekesho, jaribu kuwa na furaha muda mwingi.
6. Punguza muda unaotumia kufanya kazi ili muda mwingine uutumie kupumzika na ku-have fun.
7. Fanya mambo ambayo moyo wako unafurahia kuyafanya na unapoyafanya mwili unaburudika eg, romance, jigijigi, kuimba, kucheza michezo/muziki, nk.
Note: Iwapo hayo hayatakusaidia (mimi yalinisaidia sana) mwone daktari akupe dawa za kusaidia kushusha bp. Kumbuka kwamba ukianza kushusha bp kwa vidonge ndo utakuwa mtu wa vidonge siku zote.
 
Duh pole sana, hasa Dk anaposema umevuka usiku kwa bahati nasibu unajiona marehemu hivi hivi. Hisia ambazo binadamu hapendi kuzisikia japo ndio ukweli.
 
Kwanza punguza unene, acha mambo ya nyama choma, punguza kula chakula chenye chumvi na mafuta, uwe unakunywa maji mengi + kula matunda kama vile matango au matikiti maji, mazoezi.muhimu , usiwe unakasirika kasirika ( kuwa na furaha a.k.a raha jipe mwenyewe)
cha msingi cheza na diet sana pia punguza uzito
 
High Blood Pressure ni kunzia 140/90 na kuendelea, tukifahamu ya kwao imepanda kwa kiasi gani inakuwa rahisi ku plan management.


Pia ni vizuri tukafahamu chanzo, whether it is a primary or secondary Hypertension.


Pole.
 
Back
Top Bottom