Ushauri: Nimeokota wallet yenye Tsh. 50,000 pamoja na risiti za miamala ya pesa nyingi nahofia kurudisha nahisi naweza bambikiwa kesi

Tenda wema nenda zako usingoje shukran. Mwenye kutenda mema atalipwa kwa kutendewa mema
 
Universe imekupa hela ya chai na wewe unataka kurudisha? Haya.
😀😀😀
Ilishawahi kunitokea zamani, tena nipo ofisini mastory ya pesa za majini. Sasa kutoka nje naenda washroom nikaiona bahasha ina elfu 10 nyingi niliingia wenge la kufa mtu. Niliiokota bahasha huku natetemeka.

Siku nyingine nipo Posta soko la kisutu nakatisha barabara nikaiona dola 50 na shilingi 9000 sikuwa na wenge aisee ile hela niliikota 🤣🤣🤣
 
Chukua hiyo 50k hiyo wallet tupa mbali afu sepa
 
Ukifunge mwenyewe kamba mikononi na ujipeleke kwenye kituo cha polisi kilichopo karibu nawe
 
Kwa nini akubambikie kesi kwani hizo risiti za hiyo miamala ya 45m na 10m zina majina yako? Ndio aseme hela zimeenda kwenye akaunti zako? Acha woga riport kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe. Tena huenda akakupatia donge nono kuliko hiyo 50K unayotaka kuipiga. Pengine hizo risiti zina umuhimu kwake kuliko hata hiyo 50K iliyoko kwenye hiyo pochi uliyoiokota
 
Nenda polisi Mkuu waambie wampigie simu muhusika aje kuchukua vitu vyake achukulie hapo polisi. Ila polisi usiwaachie wenyewe hiyo wallet na wao ni binadamu kama kweli una nia ya kumrudishia basi wampe muhusika ukiwepo
 
Potezea tu
 
Nenda polisi Mkuu waambie wampigie simu muhusika aje kuchukua vitu vyake achukulie hapo polisi. Ila polisi usiwaachie wenyewe hiyo wallet na wao ni binadamu kama kweli una nia ya kumrudishia basi wampe muhusika ukiwepo
Yaani ajipeleke polisi unachukulia simple vp kama huyo aliepoteza alikufa au aliuwawa
kesi hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…