USHAURI: Nimepata Milioni 10 cash, sijui cha kufanya

Ila nakushaur tu usinunue hiace used.
Hizo idea nyingine ziko vizur
 
Namba 5 acha usijaribu ni kucheza na shilingi chooni.bodaboda nayo acha.Kwa uzoefu Wangu katu usifanye biashara ambayo wwe ushiriki yaani unaajiri mtu mwingine ndio akuletee Pesa mfano daladala bodaboda utamfaidisha yeye watu si waaminifu.Pia usiiweke kwenye kilimo kilimo ni kamari betting,fanya biashara utakayokuwa unauza au shika hela mwenyewe yaani uwepo mda wote
 
1.Umewahi kufanya chochote katika hvyo, kama mwajiriwa au ulifanya ukafeli?
2. Je ni Kipi kati ya hivyo kimejaa moyoni zaidi( ukipendacho)
3. Una mradi mwingine au ajira nyingine ukitoa hizo deal mpya unazotaka kuongeza kutokana na kupata hela?
 
mimi nilizipata kama hizo 2015, nikafungua ofisi za miamala, m pesa, tigpesa, a money etc,

Sasa hivi nipo mbali sana. Nimezalisha mara 6 ya hizo
umefungua ofisi ngapi? Mpesa, Tigopesa yapaswa kuwa back-up business alongside other good business
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…