USHAURI: Nimepata Milioni 10 cash, sijui cha kufanya

USHAURI: Nimepata Milioni 10 cash, sijui cha kufanya

Ila nakushaur tu usinunue hiace used.
Hizo idea nyingine ziko vizur
 
Wanabodi,

Katika angaika angaika yangu, nimefanikiwa kupata Milioni 10 (kumi) taslimu. Kiukweli sijawahi kupata pesa kama hii kwa mkupuo maishani mwangu pamoja na kwamba nina 42 years now. Ni miujiza.

Sitaki niicheleweshe maana matatizo ni mengi sana mtaani.

Supu ya Mbweha huliwa ikiwa ya moto.

Naombeni ushauri wa biashara ya kufanya ambayo itanisaidia kwenye maisha (SIYO SEKTA YA KILIMO maana ninalima tayari).

Nipo Korogwe Mjini hapa Tanga.

Nimewaza haya machache kwa haraka haraka:-

1. Kufungua Duka la Dawa baridi za binadamu

2. Kununua bodaboda 6

3. Kufungua hardware (Duka la Vifaa vya Ujenzi / Umeme)

4. Kufungua duka la Pembejeo za Kilimo (Madawa ya Kilimo / Mifugo n.k )

5. Kununua Hiace used

6. Kufungua duka la vipodozi

Asante wadau
Namba 5 acha usijaribu ni kucheza na shilingi chooni.bodaboda nayo acha.Kwa uzoefu Wangu katu usifanye biashara ambayo wwe ushiriki yaani unaajiri mtu mwingine ndio akuletee Pesa mfano daladala bodaboda utamfaidisha yeye watu si waaminifu.Pia usiiweke kwenye kilimo kilimo ni kamari betting,fanya biashara utakayokuwa unauza au shika hela mwenyewe yaani uwepo mda wote
 
1.Umewahi kufanya chochote katika hvyo, kama mwajiriwa au ulifanya ukafeli?
2. Je ni Kipi kati ya hivyo kimejaa moyoni zaidi( ukipendacho)
3. Una mradi mwingine au ajira nyingine ukitoa hizo deal mpya unazotaka kuongeza kutokana na kupata hela?
 
mimi nilizipata kama hizo 2015, nikafungua ofisi za miamala, m pesa, tigpesa, a money etc,

Sasa hivi nipo mbali sana. Nimezalisha mara 6 ya hizo
umefungua ofisi ngapi? Mpesa, Tigopesa yapaswa kuwa back-up business alongside other good business
 
Back
Top Bottom