USHAURI: Nimepata Milioni 10 cash, sijui cha kufanya

USHAURI: Nimepata Milioni 10 cash, sijui cha kufanya

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Wanabodi,

Katika angaika angaika yangu, nimefanikiwa kupata Milioni 10 (kumi) taslimu. Kiukweli sijawahi kupata pesa kama hii kwa mkupuo maishani mwangu pamoja na kwamba nina 42 years now. Ni miujiza.

Sitaki niicheleweshe maana matatizo ni mengi sana mtaani.

Supu ya Mbweha huliwa ikiwa ya moto.

Naombeni ushauri wa biashara ya kufanya ambayo itanisaidia kwenye maisha (SIYO SEKTA YA KILIMO maana ninalima tayari).

Nipo Korogwe Mjini hapa Tanga.

Nimewaza haya machache kwa haraka haraka:-

1. Kufungua Duka la Dawa baridi za binadamu

2. Kununua bodaboda 6

3. Kufungua hardware (Duka la Vifaa vya Ujenzi / Umeme)

4. Kufungua duka la Pembejeo za Kilimo (Madawa ya Kilimo / Mifugo n.k )

5. Kununua Hiace used

6. Kufungua duka la vipodozi

Asante wadau
 
Hongera sana mkuu. Na mimi ningependa sana kupata elimu kwa wazoefu. Tuwasubiri waje.
 
Kwa kuwa wewe ni mkulima chukua hiyo option namba 4,,
 
Wazo zuri
Ni rahisi kusimamia pia
Nenda na namba tatu maana unaweza kuanza na item chache kama Cement, gypsum board, gypsum powder, sample za tiles (ukipata mteja utachukua kwa wenzio) nk.
 
mimi nilizipata kama hizo 2015, nikafungua ofisi za miamala, m pesa, tigpesa, a money etc,

Sasa hivi nipo mbali sana. Nimezalisha mara 6 ya hizo
asante mkuu.

Mchakato kisajili line unagharimu sh ngapi na viambata vyake ni vipi?
 
Nenda na namba tatu maana unaweza kuanza na item chache kama Cement, gypsum board, gypsum powder, sample za tiles (ukipata mteja utachukua kwa wenzio) nk.
Asante kwa ushaur mkuu
 
Hivi punde,
NAKUPA MWONGOZO.

IKIWA KUTAKUWA NA USIMAMIZI MZURI NA WA KARIBU,
BIASHARA AMBAZO HAUTOJUTIA HAPO NI NAMBA 1 NA 3.

HIZO ZINGINE LAZIMA UJE KULIA!!!!
 
mimi nilizipata kama hizo 2015, nikafungua ofisi za miamala, m pesa, tigpesa, a money etc,

Sasa hivi nipo mbali sana. Nimezalisha mara 6 ya hizo
CHANGAMOTO YA MIAMALA NI ISHU YA USALAMA,
YAANI VIBAKA WANAKUTAMANI KILA ANGLE- WANAWEZA KUKULIA TIMING WAKAKUBEBEA HADI GUN!!!!

NA IKITOKEA UMEPIGWA NA MATAPELI AU WEZI-
UNAWEZA KUPIGWA MTAJI WOTE!!!
 
Hongera Sana..

Namba tatu ndiyo sahihi..uwe tu na usimamizi mzuri..
 
asante mkuu.

Mchakato kisajili line unagharimu sh ngapi na viambata vyake ni vipi?
laini ni buree, ila kinacho-matter ni location. Tafuta chimbo lenye raia wengi sana wapita njia, inaweza kuwa stendi, vyuon, sokon etc
 
Back
Top Bottom