Ushauri: Nina mil 150 niwekeze katika nini?

Hivi kuna mtu mwenye hizo hela afu hajui afanye nini?
Au mmeuza nyumba ya urithi?
UPO SAHIHI MKUU....HUWEZI KUWA NA PESA HIZO HALAFU HUJUI CHA KUFANYIA UNATEGEMEA WATU WAKUUMIZIE KICHWA NINI CHAKUFANYA..PESA PEKEE SIO MAFANIKIO YA BIASHARA..HUMU ATAPEWA MAWAZO MEPESI..KIKUBWA YEYE AJE NA WAZO HALAFU WATU WAMSAIDIE KUBORESHA AU KAMA KUNA WATU WANA UZOEFU WA HIZO BIASHARA WATAMFUNGUA..HATA HAO WANAOJIITA CONSULTANT WATAMLIA MPUNGA TU..MAANA KAMA WAO WANA HIZO IDEAS ZA BIASHARA ZA KUWAPA WATU PIA WAO WANGEKUWA WAMESHAZIFANYA AU WANAFANYA.
 
Nimeipenda
 
Nunua bonds nmb, pia malengo account zitakupa faida hadi utakapotoa hela
 
Kalime matikiti maji,zitaongezeka Mara 10,solo lake ujerumani
 
Hi wapendwa kwa rehma zake mwenyezi Mungu, nimepata haka kamzigo naomba ushauri ili kesho yangu iwe na kheri niwekeze katk biashara gani na mtaji huu

asanteni kwa maoni
Inategemea wewe unataka kupata faida kubwa zaidi au ya kawaida tu
Ili kupata faida kubwa obviously inatakiwa kufanya biashara zenye more risks kama za usafirishaj abiria au mizigo

Ila kama unahitaji faida ndogo lakin ya muda mrefu zaid bas fanya biashara kama kujenga nyumba kwa ajili ya upangishaji
 
Jenga Godown kubwa Morogoro au ukumbi wa harusi wa kisasa... Kwenye mikoa inayo chipukia Moro Iringa Dom etc..
 
Hi wapendwa kwa rehma zake mwenyezi Mungu, nimepata haka kamzigo naomba ushauri ili kesho yangu iwe na kheri niwekeze katk biashara gani na mtaji huu

asanteni kwa maoni
mie sina ushauri ila nakuomba mkuu hiyo rehema ya Mungu tugawane sote
mi naomba ajira tu maana gvt imeshindwa kutuajiri ila na wazo zuri pia ni vyema ukanipm.
 
Me nakushauri wekeza katika fixed deposit utapata 21,000,000 kama retun ambapo ukiongea nao vizuri utapata 1,750,000 kila mwezi hiyo ni retun tuu apo nazungumzia return ya 14% na unaweza pia chukua hiyo 21 milion up front ukitaka for 1 year
Mkuu...ningekuwa na uwezo wa KUONGEA na Bosi wa Tanzania,

Ningemshauri akuweke walau katika JOPO la washauri katika maswala ya Uchumi.

Umetoa USHAURI mzuri sana.
Fedha ya jamaa itakuwa katika MIKONO salama.
 
Nimepata kihala hii fedha ndugu yangu. niliwahi post hapa biashara yangu mchina kaja alikuwa anahitaji lile eneo coz lilikuwa karibu na town katoa hela.
Mkuu karibu uwekeze kwenye housing sector.. Tujenge budget homes...kuna mipesa ya kumwaga
 
fungua chama cha siasa unaona Mbowe anavyozitumua ruzuku bila wasa wasi wowote
 
mie sikupi ushauri ila nakupa tahadhari: usikurupuke, hakikisha una information (taarifa) za kutosha na za uhakika kabla ya kuwekeza.

wengi wanaotoa ushauri hapa, hawajawahi ata kuwekeza. wamesikia stori tu huko mtaani na wao wanaanza kushauri watu hizo stori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…