Ushauri: Nina milioni 6 lakini sijui nifanye biashara gani

Tuambie Bei kwa dozen
 
Wewe mtu wa2 unasema hv una idea na hii busn? Malipo yakoje n
Wewe mtu wa2 unasema hv una idea na hii busn? Malipo yakoje nk
Unaweza kuingia humo, mimi nimo humo kwa kama wiki tatu sasa. Ila nikupe angalizo kidogo. Ni kuwa utahitaji uwe na kama 8 milioni ili uiweke Bajaj yako barabarani yaani bei ya kununulia zina range kutoka 7,350,000/= hadi 7,500,000/=. Mimi niliipata kwa 7,400,000/=. Ongeza hapo Bima Kubwa (Sh.576,000/=), ongeza LATRA (22,000/=), ongeza TRA MAPATO (Sh.100,000/=) kwa mwaka wa fedha na gharama nyinine kama kujengea turubai, ngao n.k. 8mi/= na zaidi kidogo.

Baada ya hapo sasa una njia mbili za kuiendesha hiyo Bajaj yako kibiashara. Aidha umpe dereva KWA MKATABA, huyu akuletee Sh.20,000/=kwa wiki kwa miezi 24 au 26, kadri mtakavyokubaliana. Baada ya huo muda, Bajaj inakuwa ya dereva. AU umpe dereva bila mkataba kama huo hapo juu, yeye akuletee kila siku kati ya Sh.10,000/= na Sh.12,000/= kwa muda wote wa uhai wa Bajaj yako. Kuna some details nimeziacha kwa sababu ya muda kama vile kuhusu matengenezo na bima baada ya mwaka wa kwanza n.k. Twende sasa kwenye maswali ukizingatia uzoefu wangu wa wiki kama mbili hivi za barabarani.
 
Hakuna faida mkuu kama kwa siku bajaj 10-12k bora nibet tu.
 
Biashara nyingine ni biashara kichaa yaani unaweka Mil 8 alafu upate elfu 12 kwa siku?

Afadhali kidogo ukomae mwenyewe barabarani ila sio kumpa mtu akuletee elfu 12
 
Biashara ya Mchele na tikiti zitakusumbua kwa sasa.

Bajaj fine dereva uwe mwenyewe bt how comes unaweka 8M thn usubiri 25k per day ni kuzika ela tu itakuchukua miaka 2 na zaidi kuirudsha 8M.

Weka ela kwenye biashara ya kuuza solar vijijini kwa pesa iyo mtaji tosha
 
Niliwahi sema..unanunua bajaj kipande kwa siku 15 _20 ..sijui ni akili ya wapi hii!
 
Niliwahi sema..unanunua bajaj kipande kwa siku 15 _20 ..sijui ni akili ya wapi hii!
 
Kamanda bajaji wapi? M8

Nimetoka juzi tu kuulizia bajaji inaenda 7.5million na Bima mpaka 7.3million unachukua bila Bima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…