Ushauri: Nina Milioni 700, nizifanyie nini?

Ushauri: Nina Milioni 700, nizifanyie nini?

jimmymziray

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
816
Reaction score
515
Habari wana jamvi, ni matumaini yangu kwa uwezo wa yeye tumtumainiaye wote ni wazima wa afya.

Ama baada ya salamu, kama jinsi thread inavyojieleza wandugu nina suala nahitaji mawazo na ushauri wenu, ingawa sina hakika kama wachangiaji watakaochangia watanipa ushauri unaofaa au la.

Kwa utashi nilionao, naweza kuchukua yale ambayo nitaona yananifaa, na kwa yale ambayo hayatonifaa nitaweza kuyaachia humu humu jamvini.

Wana ndugu, mimi nimerithi mali na pesa taslim, ambazo kulingana na mkanganyiko na sintofahamu kutoka kwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki, nililazimika kuziuza zile mali zote ili kuziba mianya ya utapeli na dhuluma ambazo niliziona.

Kwa ujumla nimepata shilingi milion mia saba na laki saba (774,533,212) nilikuwa Mwanza imebidi nihamie Dar, nimepanga chumba.

Kwa wenye uzoefu; je, nifanyie nini hizi fedha?
 
Ningekuwa wewe ningejenga ghorofa ama nyumba za kupangisha Dar then natulia tuli kwa pesa hiyo unapata nyumba nzuri sana 14 ambazo unapangisha kwa laki5 unakuwa unapata 7 mil kila mwezi wakikulipa kwa miezi 6 una uwezo wa kuingiza 42 mil. Hizo ndo utaanza kufanyia biashara.
 
Hakika kama ni kweli una hiyo hela na upo dDr, hutadumu nayo zaidi ya siku 60. Watakupiga uishie kujinyonga!

Nakushauri urudi kanda ya ziwa nenda hata Geita ukajenge nyumba hata za wapangaji wa daraja la kati. Tumia milioni 500 kufanya huo uwekezaji. Jenga mdogo mdogo lau nyumba mbili mbili zikikamilika una pause kidogo unaanzisha tena.

Pia tafuta viwanja viwili vilivyo pimwa mkoani Dodoma jenga nyumba za angalau m70@ zitapata wapangaji na hata ukikwama huko mbeleni utauza kwa bei nzuri na kubaki kwenye form tu.

Usikurupuke kuanzisha biashara usiyo na uzoefu nayo utaanguka tu. Usikumkopeshe mtu hiyo hela hatarejesha.

Ni mara 100 kaiwekeze UTT kama huwezi kufanyia kazi. Chukua m700 weka UTT wakati ukiwa unasoma ramani nini cha kufanya, nenda dom kapange hata chumba tu unazuga hata kwa kupiga trip za bajaj huku unasoma ramani.

Pesa ya mirathi haidumu uwe makini sana itaisha fasta make hujaitolea jasho na hujui mzee alikaza vipi.
 
Kuwa makini sasa. Matapeli na wale uliowaogopa kukufanyia figisu bado wanakuwinda. Tulia, jifunze upate maarifa nini utafanyia.

Biashara zote zina risk, tofauti ni ukubwa wa hizo risks kwa hiyo cha muhimu ni kujifunza namna ya kuishi na hizo risks utakapowekeza. Kila la heri.
 
Nawalaumu sana wazazi wetu, kweli mzazi wa kuweza kukuachia urithi wa milioni 700 hakukuachia ujuzi wowote ambao ungeundeleza, wazazi tuwafundishe watoto wetu uwekezaji na biashara tokea wakiwa wadogo.
Wazazi wote hapa duniani wakiwafundisha watoto wao kuhusu uwekezaji na biashara-ndio itakuwa dunia gani hiyo, kwenye maisha kuna mgawanyo wa majukumu watu wote hawawezi kuwa investors au wafanyabishara.

Ndio maana katika post yangu hapo juu nimemwambia lazima tujuwe baadhi ya vitu kuhusu yeye ambavyo hajavieleza.
 
Wazazi wote hapa duniani wakiwafundisha watoto wao kuhusu uwekezaji na biashara-ndio itakuwa dunia gani hiyo,kwenye maisha kuna mgawanyo wa majukumu watu wote hawawezi kuwa investors au wafanyabishara.

Ndio maana katika post yangu hapo juu nimemwambia lazima tujuwe baadhi ya vitu kuhusu yeye ambavyo hajavieleza
Sio kila unachofundishwa lazima ukitumie, fungua ubongo huo.
 
Back
Top Bottom