Ushauri: Nina milioni sita nahitaji kuwekeza katika ufugaji

Ushauri: Nina milioni sita nahitaji kuwekeza katika ufugaji

Mpaka hapo umeshafeli, kabla ya kuchukua pesa inabidi mipango yote na taarifa zote za unachoenda kufanya ziwe tayari, na hapo umeshakusanya taarifa zote muhimu.

Sasa ndugu hizo pesa zinawezapotea pasipo cha maana kwasababu utafanya vitu ambavyo haviko katika mpango na mpangilio.
Akili fupi
 
Salaam wakuu!

Baada ya kuhangaika sana nimefanikiwa kupata milioni 6 ya mkopo bank, sasa nilikuwa nahitaji kuwekeza katika ufugaji, eneo la kufugia ninalo tayari lenye ukubwa wa heka 30 na ni eneo la mashambani kidogo.

Kwa eneo nilipo kwa ujenzi naweza tumia tofali za kuchoma kwa ujenzi kwa kuwa zinapatikana na pesa niliyonayo nahitaji kuitumia kwa ajili ya ujenzi wa kibanda cha mlinzi, mabanda ya mifugo na ununuzi wa mifugo.

Msaada na nini nifuge kwa kurudisha pesa haraka.
Tafuta ngombe wa kienyeji ndama wa Bei ndogo ili Kila mwaka uwe unavuna na kuuza utafurahi mkuu
 
Hio pesa tayari umefeli kabla hujaanza, Cha msingi elekeza hio ela kwenye biashara ambayo tayari ipo na inaendelea, Kama huna biashara ni ngumu kwa hela hio ya mkopo, Ikiwezekana rudisha pesa yote ili uondokane na strees za marejesho Anza upya kwa sababu eneo unalo kubwa tu...Anza na mbuzi wa mkopo au ng'ombe wa mkopo
 
Mkuu bado hujachelewa, ila kuwa makini na matumizi ya hiyo pesa angalau 80% ipandikizwe kwenye mifugo moja kwa moja! Kadri mradi utakavyokuwa unalipa ndivyo utakuwa unaboresha na kupanua miundo mbinu ya kufugia! Pia ng'ombe wa maziwa wanaweza kukulipa!
 
Fuata maelekexo haya
Jambo la kwanza uwepo wewe karibu ili kuweza kufwatilia hadi mradi usimame. Hiyo kitu haitaki mtu mwenye haraka. Sio unakaa tabata mradi bagamoyo lazma upigwe.


Jambo la pili kama unafuga tafuta mbegu bora na itunze vizuri. Kama ni ngombe basi tafuta wa kutoa maziwa ya kutosha na mbegu ya kisasa kabisa. Pia tumia mbolea na ulime bustani. Ni rahisi kuuza bidhaa za maziwa na hizo mboga mboga kwa pamoja.

Tatu, fahamu vya kutosha kitu unachotaka kufanya na weka gharama za wataalamu. Pengine ikaongeza gharama kidogo lakini itakuepusha na gharama kubwa baadae ikiwa kuna jambo utakosea. Kama ni kilimo pima udongo na pata ushauri zao gani linafaa na kwa namna gani utafaidika.
Fuga ngurue
 
Ni mradi mzuri sana. Tatizo tu ni imani. Ni mzuri kujifunzia kuliko hata kuku.
Daa INGEKUWA sio iman mkuu kwa pesa yako na mazingira uliyo yaanda ingekufaa sana.. Ila sio mbaya mirango ya kutokea ni mingi utapata njia nyine tu ..
 
Back
Top Bottom