Ushauri: Nina million 1.5 nataka kufungua saloon au ninunue bodaboda

NURDIN.HAMIS

Member
Joined
Mar 9, 2013
Posts
79
Reaction score
5
Kwa hiyo milioni 1.5 naweza kufungua kisaloon cha kawaida au ninunue bodaboda naombeni ushauri wenu wanajamii kipi ni bora zaidi kukifanya maana hela nyenyewe ndio hiyo hiyo naitegemea initoe.
 
Nunua bodaboda ila usimamie mwenyewe. Saloon at least milioni 3 ukianzia na gharama ya Pango.
 
Nunua bodaboda.....Mimi ninamiliki vyote hiyo mil 1.5 haitoshi kwa saloon, maana hapo ni bei ya pango tu....bodaboda simamia mwenyewe
 
Kwa hiyo milioni 1.5 naweza kufungua kisaloon cha kawaida au ninunue bodaboda naombeni ushauri wenu wanajamii kipi ni bora zaidi kukifanya maana hela nyenyewe ndio hiyo hiyo naitegemea initoe..
Kuna utaratibu umeibuka wa uendeshaji wa bodaboda na mimi naamini ni bora zaidi.
Unanunua bodaboda na unamkabidhi dereva kwa makubaliano ya kuwa arudishe 10000 kila siku kwa miezi kumi na mbili na baada ya hapo inakuwa yake.
Utapata wastani wa milioni tatu na kitu kwa mwaka na hata ukitoa gharama bado utabaki na faida.
Unakuwa umetengeneza faida lakini pia umemsaida kujitegemea dereva wako.
 
Kwenye hayo makubaliano matengenezo/service ya pikipiki nani anahusika...??

Shukrani.
 
Kwenye hayo makubaliano matengenezo/service ya pikipiki nani anahusika...??

Shukrani.
Ni juu yako mwenye pikipiki.Ila nimeshudia pikipiki ikiwa imemaliza mwaka ikiwa bado kama mpya kwani wanatunza mno.Tafuta mtu anayeyajua maisha na aliyekuwa na malengo usiwape wavuta bangi.
 
Kwa hiyo milioni 1.5 naweza kufungua kisaloon cha kawaida au ninunue bodaboda naombeni ushauri wenu wanajamii kipi ni bora zaidi kukifanya maana hela nyenyewe ndio hiyo hiyo naitegemea initoe..

Nunua bodaboda ikiwa wewe mwenyewe unaendesha,lakini zingatia sheria za barabara maana haichelewi kuleta umaskini kwenye family
 
Siku hizi wengi hesabu hii inawashinda.Mtagombana kila siku
Bora akupe 50,000 kwa wiki kama wanavyofanya wengi na bado inakuwa yako.Ikifika mwaka unamaamuzi yako mwenyewe aidha kuuza kununua mpya au kutumia hiyo hiyo.La sivyo utakuwa unafanyakazi ya zeze.
Pikipiki kama Boxer inawezo wa Kudum kwa ubora wake zaidi ya miaka miwili,sasa kwa hesabu ya kumuachia ikifika mwaka basi Madereva Taxi nao wangefanikiwa kwa hili.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wenu ndg. Zangu mmenifungua ubongo naamini nimepata wapi pa kuanzia asanteni sana..
 
Ni juu yako mwenye pikipiki.Ila nimeshudia pikipiki ikiwa imemaliza mwaka ikiwa bado kama mpya kwani wanatunza mno.Tafuta mtu anayeyajua maisha na aliyekuwa na malengo usiwape wavuta bangi.

mkuu hiyo njia nimeipenda..nitaimplement aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…