yah and ni mwaka huu mwezi wa kwanza ndugu yangu nliingia na akaunti moja nikapambana ila baadae kwa upande wangu nikaona sitawezana nayo bora nifanye ishu zingine..sijaconclude kwamba ni utapeli lakini maana pia nlitembeza kahawa zao zile 4 hatari nikauza kwa watu japo wengine walikuwa wanazikataa wanasema ni za kichina (si unajua wabongo tukiwa hatuna hela tunavyobwabwaja) mpaka nikatamani nijifunze jinsi ya kutengeneza kahawa zangu mwenyewe original yani nijifunze jinsi ya kukaanga na processing zote za kahawa hadi niliwaza kununua zile mashine zao special za kupackage kahawa kwa jinsi nlipata changamoto kuwashawishi kununua zile kahawa..kuhusu kuweka watu kulia na kushoto nlipata tabu sana na jinsi ambavyo mimi sio mtu muongeaji na convincing power sanaa sikuwahi kuingiza mtu kabisa..
all in all nashukuru changamoto nlizopata zimenifungua akili kwa upande mwingine na nimejifunza vingi sana in general kuhusu bussines na kuhusu maisha pia....siwezi kukushauri sanaa lakini langu moja tu..Fanya utafiti zaidi wa kitu kabla ya kukianza usije kujuta baadae ndugu . sikutishii bali ni ushauri tuu..haimaanishi kwamba mimi nlifeli na wewe ndo utafeli but also haimaanishi kila mtu anaweza kufanikiwa kwenye hii biashara...