Ushauri: Nipo ktk hatua za mwisho kufungua chuo cha kutoa mafunzo (short courses) ya computer

Ushauri: Nipo ktk hatua za mwisho kufungua chuo cha kutoa mafunzo (short courses) ya computer

mozilla

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2013
Posts
770
Reaction score
1,222
Wakuu wasalaam,
Ktk majukwaa hapa JF yanayojenga na kufundisha hili ni moja wapo kama sio linaloongoza. Big up all Business & Economic forum members.
Sasa nirudi ktk mada, mimi ni kijana wa miaka 26-27, ni muhitimu wa chuo, nilisomea masomo ya IT, wengine upenda kuita ICT. Wakuu kulingana na changamoto mbalimbali za ajira ktk nchi yetu nimependelea kujiajiri ila nisitoke nj’e ya taaluma yangu.
Kwa sasa nipo ktk hatua za mwisho kufungua chuo cha kutoa mafunzo mbalimbali ya computer, I will base only on short courses such as micro computer applications, graphic design, English courses, etc.
Kwa sehemu kubwa nimetimiza vigezo vya VETA walivyokuwa wanaitaji mm kuwa navyo na natarajia mwezi ujao (april) VETA watakuja kunikagua ili wakiona nimekidhi vigezo wanipatie registration ya kutoa mafunzo ya computer.

Nimeshafanikisha yafuatayo:
  • Nishasajiri jina la chuo BRELA
  • Nishakata TIN #
  • Nishakata business license ya IT Consultant
  • Nishalipia jengo kodi ya miaka 2
  • Nishaanda madarasa 2 (teaching room)
  • Nina computer 7
Na mengineyo yanayoitajika.

Changamoto zinazonikabili:
  • Naitaji computer 3 (vigezo vya VETA wanataka atleast uwe na 10 computers)
  • Na baadhi ya vitu vidogo vidogo ambavyo vinaitaji pesa.

Dhumuni langu:
Naombeni ushauri wenu wana JF ktk maeneo haya:
  • Taasisi zipi (government &non government institutions) zinazoweza kunisaidia udhamini ili niweze fanikisha changamoto zilizobaki?
  • Changamoto zipi nitegemee kukutana nazo ktk biashara hii?

NB - Ofisi ipo pugu kajiungeni junction of kisarawe and chanika, ilala-dsm.
 
Sina Ushauri,Lakini itoshe Kusema tu kwamba UMETHUBUTU na UTASHINDA tu!!
Ukivuka viunzi hivyo tu hakika baada ya Miaka si zaidi ya Minne utakuwa Moja Kati Ya Watu wenye Wallet Nene hapa Dar es salaam!!

All the Best!!
 
Kaka hongera kwa kuwa umeshafika mbali sana, changamoto zilizo baki si kikwazo kwako kuanza business husika, maana mambo ya msingi kwa nature ya business umeshafanya. PILI nakupongeza kwa KUTHUBUTU kitu ambacho ni kigumu kwa graduate wengi hapa nchini. Tujiulize kama wote tunahitaji kuajiriwa then AKINA nani watatengeneza NEW job opportunities? nani watakuwa ma-GM, CEO nk? You have done your part brother, miaka 5 ijayo UTAAJIRI SANA!! mawe bank statement itakuwa inasoma vema!
SASA uhitaji wako na changamoto and /or Risks unahitaji au ulihitaji kuzijua/ku- analyze mapema katika BUSINESS PLAN YAKO, ambayo kimsingi kama inge andaliwa vema/kitaalamu na wewe ukaifuata basi kinacho kusumbua sasa kisingingekuwepo! So go back to your BUSINESS PLAN, if you dont have Prepare one, IF you need external Consultant find one, humu JF wapo kibao, TRY BINOCRATS......, or try http://www.kimiconsultancy.blogspot.com/ (mimi huyo) na wengine kibao. Unajua kila discipline ina watu wake, pia ni mhimu kuwatumia na ndivyo ilivyo kwa ofisi kutegemeana.
PAMOJA kila mtu katika fani na uwezo wake akifanya hivyo, vijana tutatoka japo si katika mindset ya utajiri!!!! tuwasiliane kwa mengi zaidi au tembelea blog hiyo.
 
Back
Top Bottom