Ushauri: Niweke fedha benki kwenye fixed account au ninunue hisa?

Ushauri: Niweke fedha benki kwenye fixed account au ninunue hisa?

kamikaze tz

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2017
Posts
232
Reaction score
174
Habari wakuu, naomba mwenye ujuzi na mambo ya fedha anisaidie.

Kuweka fedha benk katika akaunti ya muda maalum(fixed account) au kununua hisa kipi kinaweza kuwa bora zaidi kwa malengo. Ushauri wenu unahitajika
 
Ngoja wajuzi wa maswala ya kifedha waje watujuze, wengi tunaitaka hii elimu
 
Mimi siyo mjuzi wa uchumi na fedha lakini nafikiri kuwa kama utaihitaji hiyo pesa tena ktk kipindi kifupi, weka katika akaunti ya muda maalum. Kama haitahitajika katika kipindi kifupi, nunua hisa.
 
Habari wakuu, naomba mwenye ujuzi na mambo ya fedha anisaidie.

Kuweka fedha benk katika akaunti ya muda maalum(fixed account) au kununua hisa kipi kinaweza kuwa bora zaidi kwa malengo. Ushauri wenu unahitajika
Ukinunua hisa ni jambo jema ila kwa trend ya stability ya makampuni ilivyo mie ninaona heri uweke fixed deposit ila kwenye bank kubwa zinazoaminika maana kwenye hisa ni pata potea kwa sasa
 
Fanya forex, weka lot size 0. 01 fungua lot kama kumi hivi..............ukihitaji pesa yako unaclose order vizuri tu

Hii biashara ya forex ipo vipi mkuu, ukweli kwangu ni kitu kipya hiki
 
Hii biashara ya forex ipo vipi mkuu, ukweli kwangu ni kitu kipya hiki
Forex
Ni biashara ya kuuza na kununua pesa kwa kifupi.........

INA SHERIA ZAKE............. Pesa ambazo unaweza tu kuziweka benki kisha ukizitoa wanazikata........... Unaweza kuzibadilisha kuwa kwenye USD, JPY, EUR etc kisha ukaziuza kulingana na demand....... With higher discpline of money management zinaweza zaa faida kubwa zaidi.

a0565883b7387e955c660df6763d6ab8.jpg

ONA HAPO USD 50 ndani ya saa 1imezaa USD 15............. Yaani laki 1 na 11 ya TZ, imezaa elfu 32 ndani ya saa 1........... What the business?
 
Inategemeana na mtaji ulionao na level yako ya maisha kiuchumi,
1. Fixed account ni nzur kama ww ni maskini yaan mtaji mdogo! Level 3 ,yaaan kuanzia million 5 mpaka 200 millions,
2. Hisa ni nzur kwa investors level 1 and 2yaani wenye mitaji ya kuanzia million 200 mpaka billions!
Ni mwehu pekee anayekimbilia kununua hisa na mtaji chini ya million 5, huku hana hata kiwanja cha 1million, anaishi nyumba ya kupanga, hana kitega uchumi, anaishi na maden juu!
Kununua hisa na kukodolea gawio na jaa kali likukomboe kimasha sio ujanja ni ufalaa!!
 
Hii biashara ya forex ipo vipi mkuu, ukweli kwangu ni kitu kipya hiki
Tumia simu yako google kitu forex.............. Tumia search engine ya Jamii forum angalia kitu forex.
Prons na cons zimeelezewa humo....

Ni kazi yako kuujua ukweli.
 
Aisee nunua kiwanja utakiuxa utakapo kuwa na uhitaji na pesa yako mimi nimenunua hisa benki ya walimu tangu 2015 mpaka leo sijapata gawio, na kuna sehem niliacha kununua uwanja kwa kipindi hicho kwa thamani ya pesa niliowekeza ningekinunua kwa sasa ningekuwa na nusu ya thamani ya fedha nilio idhika.
 
Habari wakuu, naomba mwenye ujuzi na mambo ya fedha anisaidie.

Kuweka fedha benk katika akaunti ya muda maalum(fixed account) au kununua hisa kipi kinaweza kuwa bora zaidi kwa malengo. Ushauri wenu unahitajika
Inategemea unaiweka kwa ajili gani. Kama unataka hiyo fedha ikupatie faida inategemea na kiwango unachoweka fixed deposit. Average rate ya fixed deposit ni 16%. Inategemea unaweka shilingi ngapi ongeza asilimi 16 ndiyo faida utakayopata. Kuhusu hisa faida utapata kama utasubiri hisa zipande bei ndipo uuze. Sasa soko letu halijachangamka sana hivyo nako vigumu kupata faida kubwa. faida kubwa pia inategemea umenunua hisa ngapi na kama znapanda bei kila wakati. gawio la hisa huwa si kubwa. Kununua wakati bei iko chini na kuuza wakati bei imepanda ndiyo kunafaida katika hisa. Kuna mtu alisema kununua fedha za kigeni kuna faida sana. Kwa mfano ukinunua US dollar leo na ukauza mwaka kesho au baada ya miaka miwili utapata faida kubwa.
 
Somo lako zuri sana nimelielewa kidogo, ila hapo kwenye 16% ya faida, je hii ni kwa mda gani? Nina maanisha ni faida ya kila mwezi au mwaka, au kwa kipindi chote utakachokuwa umeweka?
 
Back
Top Bottom