Ushauri: Noti za tsh 1000 na 2000 zibadlishwe material ya utengenezaji huwa zinachoka sana katika mzunguko

Ushauri: Noti za tsh 1000 na 2000 zibadlishwe material ya utengenezaji huwa zinachoka sana katika mzunguko

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Salama humu.

Sijui ni lini hizi noti zilianza kutengenezwa na kuanza kutumika, naona ni muda mrefu sana umepita. Na ni muda sasa muafaka wa kupata noti mpya hasa hizi za tsh 1000 na 2000.

Unajua hela ya noti kwa nchi ni kama nembo ya Taifa. Zinawakilisha nchi na wageni mbalimbali wanazitumia.

Sasa hizi noti zinapochoka huwa zinakuwa katika hali hoi bin taabani hata kuzishika unaogopa unaona kama muda wowote inaweza kuchanika. Zina mzunguko mkubwa sana wa matumizi hasa huku kwetu underground tofauti na noti za tsh 5000 na 10000.

Kwa mimi naona ni muda muafaka sasa kuzibadilisha na kuwe na material imara ya kuzitengeneza kama noti za tsh 5000 na 10000.

Tuna wageni mbalimbali wanafika nchini kwetu hasa watalii,sasa wanapokutana na noti imechoka namna hii haileti taswira nzuri.

La pili ni kuwa kuna haja sasa ya noti zetu ziwe na picha ya waasisi wa taifa letu.Naona tu hizi picha zimewekwa kwenye pesa za coin sijui kiswahili chake 'coin'

Humu kwenye coin hizi picha za waasisi wetu lakini hazionekani vizuri na hata maandishi yake kuyasoma uwe na macho yenye lens kali kuweza kuyasoma.
Umuhimu wa wa hizi picha ni kwa ajili ya vijana wetu na vizazi vyetu vya sasa na vijavyo kuweza kuwajua waasisi wa Taifa letu. Picha hizi na maandishi zikikaa kwenye noti zitaonekana vizuri na mtu ataweza kusoma vizuri maandishi.

Kwa ushauri wangu noti ya tsh 10000 iwe na picha ya Mwalimu Julia's K. Nyerere na noti ya 5000 iwe na picha ya rais Aman A.Karume rais wa kwanza wa Zanzibar.

Sasa tukija kwenye noti za tsh 1000 na 2000 mi nashauri ziwekwe picha ya Mama.Nani kama mama,hakuna kama mama.Mama Samia raisi wa kwanza Mama kwa Taifa letu la Tanzania.

Rais Mpole na mnyeyekevu anaewapenda wananchi wake.Na ninahisi ana mitano tena mwakani.(hapo nimechomekea tu.)Tanzania tumebahatika kupata Rais wa kwanza mwanamke,basi ingependeza tuwe na picha ya mama kwa noti hizi mbili

Noti zetu zimekaa muda mrefu sana hazijabadilishwa ni muda muafaka sasa kutumia point hizo juu kufanya mabadiliko.
 
Noti za 1,000 zinachoka sana haraka kwa sababu zinatumika sana na kupita mikononi mwa watu wengi.
Na hata 2,000 inachoka haraka kuliko noti ya 5,000.
Pia noti ya 5,000 inachoka haraka kuliko noti ya 10,000.
 
Thamani ya noti inapokuwa ndogo na mzunguko wake unakuwa mkubwa halikadhalika uchakavu ni haraka sababu inatumika na watu wengi sana. Ndio maana elfu 10 na elfu 5 hazichakai haraka.
 
Na sisi hatutaki tukae nazo sana mkononi. Inatakiwa ziwe zinachakaa haraka ili serikali ione umuhimu wa kuboresha mazingira ya kukuza uchumi.
 
Back
Top Bottom