Ushauri; nyumba ndogo imeathirika mi mzima

Ushauri; nyumba ndogo imeathirika mi mzima

Joined
Oct 9, 2010
Posts
13
Reaction score
3
Habari!

Mi ni kijana mwenye mke na mtoto mmoja, nina mpz nje ya ndoa yangu ambaye anakaa kwao. nimekuwa na uhusiano nae kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa; sijawahi kwenda nae kupima licha ya yeye kudai mara ya mwisho alipima mwaka 2007 na alikuwa safi lakini mimi huwa napima mara kwa mara.

hivi karibuni alikuwa mbali nami kwa masomo ingawa mawasiliano yalikuwepo kama kawaida na nilikuwa namtania kuwa hata kama naibiwa basi tumieni kondom, utani huo ulionekana kumkera hata kufikia kusema akiridi kabla ya kukutana tupime kwanza nikamkubalia.
amerudi na jana tukaenda kupima alikuwa ananipigia mara kwa mara kuniuliza tunaenda saa ngapi?

tulipofika eneo la tukio kama kawaida tulipewa ushauri nasaa na kuulizwa maswali kama kwa nin mriamua kuonana kimwili kabla ya kupimwa binafsi nilijibu kutokana na afya yake niliamini hana maambukizi (ni binti mnzuri kwa muonekano, hips za kuvutia na ---- lakutosha ni raha hata kuongozana nae) na yeye alisema aliniamini.

tukatolewa damu ingawa ilikuwa tofauti kidogo na nivyowahi kupima kabla, kabla walikuwa wanatoa damu kidoleni kama wanavyopima malaria ila sasa walinitoa hapo wanapotoa damu kama unataka kumuongezea damu mtu.

baada ya muda tuliitwa kupewa majibu na mambo yalikuwa hivi
baada ya maneno ya daktari aliendelea kutuuliza maswali kama itaonekana mwenzako ameathirika (nilimtambulisha kama mke wangu) utafanyaje nikajibu nitaendelea kuwa nae na nitatumia kondomu kwake ila yeye alijibu ana uhakika yupo vizuri; mi nikadakia nakumwambia usimchagulie docta jibu.
baadae daktari akaniambia nipo vizuri nakumwambia mwenzangu samahani kwa majibu hayo nitakoyokupa vipimo vinaonesha umeathirika. sikuamini na bado siamini

daktari alienda mbali zaidi kwa kutuonesha kuwa baada ya kumpima kwa kipimo cha kwanza akampima kwa mara ya pili, tatu na baadae akaamua kubadilisha kipimo akatumie kingine (alituonesha) lakini majibu bado ni yale yale.

Mapokea ya majibu ya mwenzangu
hakushtuka sana kitu kilichonishangaza alianza kulia baada ya dk 20 kupita
haamini matokeo ana taka kurudia kupima, aliendelea na kulia huku majuto ya kiwa kwa kiasi kidogo ila alikuwa mara kwa mara akiomba nisimuache na mimi nirimhaidi kuto muacha.

nilitumia muda mwingi kumnyamazisha ingawa hakutulia kwa asilimia mia, na baadae nilimpeleka kwao ambapo wazazi wake walikuwa wameondoka na yeye alibaki na wadogo zake, tulipofika kwao aliendelea kulia waliniuliza analia nini nikawajibu tumekorofishana lkn namwambia yameisha hataki kuelewa akawa anajibu kuwa mi mwongo na alitaka kusema ukweli nikamkataza na mara akawasha simu yake akitaka kumpigia simu mamake nikamnyang'anya.

alikuwa na kadi ya harusi ya mamake aliniambia ataenda kwenye sherehe na baadae alienda (mambo haya yote yalianza saa kumi na mbili jioni) alikuwa huko nilikuwa namfuatilia kwa kumpigia simu alikuwa haoneshi kuwa na wasi wasi sana ila aliomba nisimuache, na asubuhi ya leo ameenda kunisani kama kawaida.

Ninachohisi
Aidha alikuwa anajua ameathirika au alikuwa anajua ametembea na mtu aliyeathirika hivyo alikuwa na uhakika wa zaidi ya asilimia 50 kuwa ameathirika kwa sababu.
  1. Alitaka kumlazimisha daktari kutoa majibu kama haja athirika (rule out the doctor)
  2. hakupokea majibu kwa mshtuko sana.
  3. anaomba kuto achana na mimi badala ya kufikiria zaidi kuathirika kwake
  4. ameweza kwenda kwenye sherehe ya harusi just after an hour (nilipenda aende kwa ajili ya kupoteza mawazo) lakini sikutegemea akubali au iwe rahisi kwake
  5. ameweza kwenda kanisani leo

Nataka
  1. Nimpeleke hospitali nyingine akapime tena na hata kama majibu yataendelea kuwa kama yalivyo sasa basi apewe ushauri nasaha ili aondokane na mawazo ya kuathirika ni mwisho wa maisha na kuwa huru kimawazo.
  2. niendelee kuwa nae karibu kwa muda fulani then nitampotezea (ushauri unahitajika kutoka kwako msomaji)

Naomba ushauri kuhusu hali hiyo ikiwemo uhusiano wetu wa kimapenz.i ili kumuondoa mawazo nilimwambia nitaendelea kufanya mapenzi nae ila kwa kondomu sio kama ilipokuwa kuwa awali ambapo kondomu ilikuwa haitumiki.

ndigu zangu ukimwi upo tuwe makini na wapenzi wetu tusipime kwa macho huyo ambaye namzungumzia ukimwona alivyoshiba huwezi amini kuwa ameathirika.

naomba kama huna cha kuchangia pita tu utani singefurahia sana
 
pole sana ila ningemshauru huyo dada aanze kutumia VIRUTUBISHO vya kinga kabla kinga yake haijaanza kupungua NA kuanza kuugua. Ni wengi wametumia NA wanaishi kwa furaha.
0713507487
0767507487
0782898210
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1371984893448.jpg
    uploadfromtaptalk1371984893448.jpg
    6.2 KB · Views: 333
The possibility of an HIV free generation begins with you.

Kuwa na nyumba ndogo sio ujanja ndugu yangu, yaani ni bora upige nyeto kama umeshindwa kuvumilia K ya wife tu
 
Poleni.


Mkuu huna haja ya kupanic maradhi ni
kawaida kwa binadamu ila hata akipima
tena usimwache kwakuwa huenda akafa
haraka utakapomtenga.


Jaribu kuwa nae tu ila zana zitumike.
 
kawaida nyumba ndogo zote huingiwa na wengi, SHARED. Akili kichwani.
 
dah! hilo ni onyo mkuu...tubu afu mpende kw dhati mke wako...nasema mpende kwa dhati coz kama unampenda utamlinda kitendo cha kwenda kavu nje ni kuhatalisha maisha na future ya familia yako...achana na huyo nyumba ndogo mara moja na baki na mkeo pekee...
 
dah! hilo ni onyo mkuu...tubu afu mpende kw dhati mke wako...nasema mpende kwa dhati coz kama unampenda utamlinda kitendo cha kwenda kavu nje ni kuhatalisha maisha na future ya familia yako...achana na huyo nyumba ndogo mara moja na baki na mkeo pekee...
asante
 
wataalamu anaweza kufanya nae mpz na kondomu na asipate ukimwi?
busherere inaweza isisimame
 
mungu ameshakuepusha.najua unamuonea huruma huyo nyumba ndogo yako.jee vipi kuhusu mke wako?huna watoto?humfikirii mke wako?achana nae huyo dada,hiyo iwe kama fundisho.si ushukuru mungu umepata second chance,maana na wewe ungempelekea mkeo jee?fikiria familia yako,kama una huruma nae kuwa karibu ila sio kimapenzi.ooh utumie condom,usithubutu tena.mwambie umeamua kuwa katika ndoa yako,maswala ya mapenzi wewe na yeye tena basi.maybe alikuwa na mt5u wakati wewe uko mbali.sasa bado unataka bado uiendeleze chain?
 
Hehehe eti utani haufurahii. Muombe ushauri mkeo. Afu wewe si wamekuambia urudi baada ya miezi 3?
 
Back
Top Bottom