Ushauri: Oda za wateja zimezidi mtaji nilionao

Ushauri: Oda za wateja zimezidi mtaji nilionao

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Niende kwenye mada mojakwamoja Nimestack wakuu mimi najishughulisha na kusupply vifaa mbalimbali.

Sasa toka mwezi October nilianza kufanya usambazaji wa bidhaa kwa wateja ila hadi kufika mwezi huu oda zimekuwa nyingi kuzidi mtaji na teyari nimepokea oda mpya na nimehadi kupeleka bidhaa kwa wakati kwa wateja.

Sina vyanzo vingi vya kupata mkopo hili ndio linaniumiza akili.

Naomba Ushauri
1. Nawaza niwataarifu wateja kuwa sitaweza kudeliver bidhaa zao tena sababu ya mtaji na je si nitawapoteza alafu itakuwa haina maana ya hiki ninachofanya biaashara haitakuwa.

2. Wapi naweza kupata pesa ili nibust mtaji na niendelee kusabaza bidhaa kama kawaida kwa wateja wangu..

Naombeni ushauri wenu wakuu..
 
Kama wewe ni kampuni na unaofanya nao kazi wako registered pasipo chenga chenga. Nenda benki fukuzia mikopo ya kitenda. Utawasambazia ila payments zikifanyika benki watachukua chao.

Kama wote ni unga unga kukwepa kodi, njia kajisalimishe kwa agents wako anayeku supply mueleze kila kitu atajua anakusaidia vipi. Ikiwa mkakubaliana yeye ndio apeleke. Itabidi utumie resource zako kufikisha mzigo na kuhakikisha unalinda wateja wako.

Mwisho fanya kazi ndani ya uwezo wako. Kuzidi uwezo kutapeleka kufanya kazi chini ya kiwango, kufanya kazi pasipo tahadhari. Matokeo yake utajikuta kwenye kuongezeka kwa cost, na madeni na mwisho kuuuuuuuufa
 
“Hakuna kitu kibaya kama kuanzisha biashara kupata order kubwa kuliko ulivyotegemea halafu ukashindwa kuitimiza, utatamani upasuke” ushauri nlipewa na mtu kabla sijaanza biashara

Suluhisho chukua bidhaa kwa competitor fulfill hizo orders hakikisha unaweka value zako ili usijiharibie reputation. Hii ni kama umeshindana na supplier na umekosa funding
 
covid 19 Kama bidhaa yako ni unique unayo wewe tu, hapo ndio matatizo mengine hayo🤣... hope haujawaaidi hadi delivery date
 
Mkuu ungesema unahitaji mkopo kias gani na utaweka dhamana ya kitu gani.
 
covid 19 Kama bidhaa yako ni unique unayo wewe tu, hapo ndio matatizo mengine hayo🤣... hope haujawaaidi hadi delivery date
Ni very unique ndio maana nawaza ingekuwa kama nyingine ningetoa deal kwa suppliers wengine ila ni unique na nataka kulinda code maana naona kuna features mbèleni kwa hii kitu inakubalika sana..
Na ujinga niliofanya nilitoa date delivery ili kuonekana naenda na muda..😅
 
Tafuta partnering, sishauri mkopo. Share a percentage in agreement pia tumia social media kutangaza tender yako.
Ndio najaribu kufanyoa kazi hili hata kuleta hapa nia moja wapo ni kama nitapa partner itasaidia..
 
Mkuu ungesema unahitaji mkopo kias gani na utaweka dhamana ya kitu gani.
Mkopo yes dhaman ni wateja maana ni taasisi zinzoaminika so na hawajawah kunisumbua kwenye malipo..
 
Mkopo yes dhaman ni wateja maana ni taasisi zinzoaminika so na hawajawah kunisumbua kwenye malipo..
Sasa Mkuu ingependeza ukaweka mpangilio mzuri endapo Mtu akihitaji kushare na wewe au kukupa mkopo ni kias gani unahitaji!!?
 
Niende kwenye mada mojakwamoja Nimestack wakuu mimi najishughulisha na kusupply vifaa mbalimbali.

Sasa toka mwezi October nilianza kufanya usambazaji wa bidhaa kwa wateja ila hadi kufika mwezi huu oda zimekuwa nyingi kuzidi mtaji na teyari nimepokea oda mpya na nimehadi kupeleka bidhaa kwa wakati kwa wateja.

Sina vyanzo vingi vya kupata mkopo hili ndio linaniumiza akili.

Naomba Ushauri
1. Nawaza niwataarifu wateja kuwa sitaweza kudeliver bidhaa zao tena sababu ya mtaji na je si nitawapoteza alafu itakuwa haina maana ya hiki ninachofanya biaashara haitakuwa.

2. Wapi naweza kupata pesa ili nibust mtaji na niendelee kusabaza bidhaa kama kawaida kwa wateja wangu..

Naombeni ushauri wenu wakuu..
Nenda Benki kachukue mkopo haraka sana. Biashhara huwa ni wateja
 
Back
Top Bottom