Ushauri: Pesa zimeisha kimaajabu

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
591
Reaction score
1,001
Salaam wakuu, niende kwenye tatizo langu. Kwenye harakati zangu zakujenga nchi, juzi tar23 may nikafanikiwa kulipwa na bosi wangu ujira unaotokana na jasho langu.

Nilipanga kufanya matumizi kadhaa nakubakiwa na akiba Kama kanuni zinavyotutaka ku save. Cha ajabu leo nimekaa na kadaftari na calculator ili nipitie matumizi yote nilofanya. Katika hesabu hizo nimegundua 104k haipo na haijatumika kabisa.

Nipo hapa kitandani kichwa kinagonga naombeni Ushauri labda kuna namna zakimiujiza huwa zinajitokeza kwenye issues Kama hizi.

Nawasilisha
 
Umelipia zile bia mkuu
 
Laki na elfu nne kudadadeki. Ukimpata aliyekuibia nakushauri mbake
 
Ulitakiwa utoe hata buku 5 tu kumshukuru Mungu.Bila hivyo tukikupa Bilioni 1 tutakukuta uvuguni mwa kitanda.
 
Hamna sangoma humu
Jaribu Mlingitini Bwagamoyo
 
Cha ajabu Leo nimekaa na kadaftari na calculator ili nipitie matumizi yote nilofanya.
Ulitakiwa kutumia 'Kadaftari' na calculator kabla hujaanza matumizi ya fedha yako, Hili ndio funzo unapaswa kulishika kuanzia sasa.
Kama kanuni zinavyotutaka ku save.
Kanuni inakutaka ku_save kiasi cha pato lako kabla ya matumizi, na sio baada ya matumizi.
 
wahumi wamekuzidi nguvu, unaibiwa na warogi
 
Nenda kwa Mwamposa faster. Zitarudi zote siku hiyohiyo! Tena na nyongeza juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…