Da Asia
JF-Expert Member
- Sep 25, 2011
- 731
- 819
tunaishi mikoa tofauti, naamini tunapendana, japo kuonana kwetu ni mara chache sana. kutokana na umbali na majukumu. sote ni watu wazima, aliwahi kuoa, akazaa watoto, it didnt work wakaachana. na mimi hali kadhalika. tulikubaliana kuoana kama tukiona mahusiano yanakwenda vizuri. japo mimi nilimwambia nisingependa tuoane halafu tuendelee kuishi mikoa tofauti, sio maisha ninayoyataka kwa umri wangu. nimeshaishi mwenyewe kiasi cha kutosha.
sote ni waajiriwa japo mimi kipato changu kimezidi cha kwake, hainipi tabu kwa sababu katika mahusiano huangalii kipato, kikubwa na maelewano. analalamikia kipato chake kila wakati kua hakitoshi hasa kusomesha watoto wake ambao bado wako shule, na pia kugawa inakua kazi, vile watoto wanasoma mkoa mwingine. tukakubaliana aache kazi aje tukae pamoja nilipo mimi ambapo ndipo na watoto wake walipo. tukawa tumeshapanga tayari nini atafanya. akatoa notice kazini kwake, lakini wakataa wakadai watamuongeza mshahara maana aliwaambia mshahara hautoshi. kweli akaongezewa mshahara, si kiasi kikubwa japo naona yeye karidhika na mipango ya kuhama haipo tena.
kwa hivyo kila tulichopanga kufanya tukiwa pamoja imekua ndoto maana sioni kama kuna dalili ya mtu kuja tena. nimekua muwazi kwake, na kumwambia kua, sitaweza kumsubiri tena maana siko tayari kuishi mwenyewe. nina miradi ambayo nilitaka yeye akiacha kazi asimamie na kufufua mingine na kuiweka sawa wakati anatafuta kitu chake mwenyewe cha kufanya, maana siku zote amekua akidai asingependa kujibwetesha kwenye miradi ambayo ni ya kwake. ila yuko tayari tuanzishe ya kwetu. sijui hili lina maana gani. maana mwisho wa siku ni vitu vyetu. hana imani tena na mimi maana anahisi nitamuacha na mimi nimemwambia he needs to make up his mind maana hatuwezi kuishi hivi tunavyoishi. kwa sasa maelewano si mazuri sana sababu ya hili tatizo ambalo ufumbuzi muafaka hatuna.
wana JF, naomba mniambie nani mwenye kosa hapa. mimi au yeye au wote wawili. au tutaishi hivi for how long. tuna miaka miwili sasa tangu tuwe kwenye mahusiano.
Mimi sioni mwandishi mzuri, lakini nina imani mmenielewa.