Ushauri: Rais Samia zuia mazao kwenda nje ya nchi, njaa inalinyemelea Taifa

Mishenyi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
464
Reaction score
748
Mh. Ukiachilia mbali mfumuko wa bei wa ajabu kuwahi kutokea,,,nakuomba zuia mazao kwenda nje ya nchi ulinisuru Taifa na njaa,,mvua zimegoma kunyesha mahindi na mpunga vimeanza kupandishwa bei kiholela.Mh.nakuomba simama na wananchi angalau kwa hili njaa itakuletea mgogoro mkubwa katika utawala wako najua hutafurahia kusikia watu wanasaga pumba iwe ndo chakula chao!!!

Chonde chonde waziri wa kilimo,biashara nk kama mnapita humu fikisheni taarifa hii haraka kuwanisuru wananchi,,,Chakula ni jambo linalogusa usalama wa Taifa letu ikiwezekana weka bei elekezi ya mazao isiyomuumiza mkulima wala mlaji,,,Zuia mazao kwenda nje tafadhali

Mfumuko wa bei mmeshindwa lkn hili najua mnaweza
 
Nchi inanyemelewa na njaa kali kutokana na mvua kushindwa kunyesha kwa wakati. Maeneo mengi ya nchi ni makame. Nashauri Serikali izuie kuuza mahindi nje ili chakula kibaki ndani kudhibiti mfumuko wa bei katika mazao unaoanza kujitokeza. Mh. Rais usikubali na hili likushinde wananchi wako wakafa na njaa.

Ikiwezekana panga bei elekezi isiyomuumiza mkulima wala mlaji, wananchi wanateseka na mfumuko wa bei msiwaongezee tena pigo la njaa tafadhali.
 
Kwanini usimshauri anunue chakula tokea nchi zenye ziada?
 
Ujinga.

Serikali inunue mazao kwa bei ya soko.

Yaani eka zangu 30 za maharage nizilime kwa shida na kutumia nguvu kumwagilia ili niuze kwa faida zizuiwe kuuzwa nje ili mtu aliyekaa ofisini na AC asife njaa?

Tuna Ardhi kila mtu ajilimie kisehemu chake asife njaa, sio kushinda mjini halafu mkulima awe masikini ili msife njaa.
 
Sawa akili zako zinakutosha mwenyewe
 
Ujinga.

Serikali inunue mazao kwa bei ya soko.

Yaani eka zangu 30 za maharage nizilime kwa shida na kutumia nguvu kumwagilia ili niuze kwa faida zizuiwe kuuzwa nje ili mtu aliyekaa ofisini na AC asife njaa?

Tuna Ardhi kila mtu ajilimie kisehemu chake asife njaa, sio kushinda mjini halafu mkulima awe masikini ili msife njaa.
Mbona unalalamika mabati na nondo nk kupanda bei kwanini usikae kimya!! Tunategemeana katika kuishi!! Vipi na wewe mwenye shule akikupandishia ada x2 utapenda,Mseto ukiuzwa 10000 dozi utapenda!!? Hatuwezi kuishi tutakavyo itakuwa vurugu na hiyo huzusha vita,kaangalie mataifa yanayopigana mengi serikali zao zimeshindwa kudhibiti mambo kila mtu anapanga unyama dhidi ya mwenzie kama wewe unavyopanga unyama dhidi ya mtu aliyepo ofisini kumuuzia debe la mahindi 25,000 wakati unajua hajawahi ongezwa mshahara miaka 7 sasa
 
Kilimo ni biashara sawa na ajira au biashara yako hapo ulipo, IHESHIMU kwa kupendekeza serikali iache forces za demand and supply ziwe in control.
[/QUkila kitu lzm kiwe under control other ni vurugu zinazoweza pelekea vita kama nchi zingine ambazo kila kitu kimekosa governor
 
Hapana wananchi wana shida nyingi hasa mfumuko wa bei katika bidhaa nyingime sasa ukiruhusu hata chakula kuwa ghali itakuwa shida sana

Nani amewapangia bei wauza bidhaa kariakoo au kuamua wauze wapi? Jaribu kulima ndo utajua kwamba jamaa wanateseka sana. Kwanza wengi wao wanalima kwa tabu sana, waacheni nao wafaidi. Serikali haijawasaidia kwa chochote kabisa.
 
Mbona unalalamika mabati na nondo nk kupanda bei kwanini usikae kimya!! Tunategemeana katika kuishi!! Vipi na wewe mwenye shule akikupandishia ada x2 utapenda,Mseto ukiuzwa 10000 dozi utapenda!!? Hatuwezi kuishi tutakavyo itakuwa vurugu na hiyo huzusha vita,kaangalie mataifa yanayopigana mengi serikali zao zimeshindwa kudhibiti mambo kila mtu anapanga unyama dhidi ya mwenzie kama wewe unavyopanga unyama dhidi ya mtu aliyepo ofisini kumuuzia debe la mahindi 25,000 wakati unajua hajawahi ongezwa mshahara miaka 7 sasa
Mabati yakipanda bei yakawa na faida wazalishaji wanaongezeka yanakuwa mengi demand inashuka supply inaongezeka bei inashuka, hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa... Serikali inatakiwa iache forces za demand na supply zifanye kazi, inatakiwa kuingilia kati kama kuna watu kwa makusudi wanaficha bidhaa ili zipande bei na si vinginevyo.

Suala la mshahara ni suala binafsi na linategemeana na umuhimu wa mfanyakazi husika kwa mwajiri wake, kama hautoshi ni jukumu la mfanyakazi kuchukua hatua kwa kufanya kazi inayomlipa. Kuna sekta ziliongezwa mishahara kutokana na umuhimu wao.
 
Nani amewapangia bei wauza bidhaa kariakoo au kuamua wauze wapi? Jaribu kulima ndo utajua kwamba jamaa wanateseka sana. Kwanza wengi wao wanalima kwa tabu sana, waacheni nao wafaidi. Serikali haijawasaidia kwa chochote kabisa.
Ukiwa wewe kama rais hutachelewa kupinduliwa kwa kiacha kila mtu apange atakavyo hasa kwa vitu muhimu kama chakula,,,mtu unaweza kuacha kujenga ila huwezi kuacha kula,,,Nakujuza chakula ndio Usalama wa Taifa ndugu
 
Kwa nini wakulima tu ndo wapangiwe??
 
Mh. Ukiachilia mbali mfumuko wa bei wa ajabu kuwahi kutokea,,,nakuomba zuia mazao kwenda nje ya nchi ulinisuru Taifa na njaa,,mvua zimegoma kunyesha mahindi na mpunga vimeanza kupandishwa bei kiholela.Mh.nakuomba simama na wananchi angalau kwa hili njaa itakuletea mgogoro mkubwa katika utawala wako najua hutafurahia kusikia watu wanasaga pumba iwe ndo chakula chao!!!

Chonde chonde waziri wa kilimo,biashara nk kama mnapita humu fikisheni taarifa hii haraka kuwanisuru wananchi,,,Chakula ni jambo linalogusa usalama wa Taifa letu ikiwezekana weka bei elekezi ya mazao isiyomuumiza mkulima wala mlaji,,,Zuia mazao kwenda nje tafadhali

Mfumuko wa bei mmeshindwa lkn hili najua mnaweza

Hii ni njia ya kijima na fikra za kijima. Kwanza watu wanaouziwa nje si watu? Binadamu wote ni ndugu na sawa.

Wacha watu wafanye mambo kwa uhuru wao.

Huwezi lalamika mvua wakati Tanzania ni nchi pekee iliyozungukwa na maji ya kudumu.
 
Wafugaji walikesha na kuomba mvua kwa Mungu kuokoa mifugo yao iliokuwa inakufa kwa kukosa maji na malisho,

Wachoma mkaa na wafyatua matofali nao wanakesha na kuomba kwa Mungu asilete mvua kwani mvua inakwamisha kazi zao kufanyika hatamae wanakosa pesa zakuendesha Manisha yao.

Sijui Mungu asikilize lipi.

Wakulima wanaomba kwa sekali mipaka iwe wazi ili nafaka ipande bei wapate faida,
Raia nao wanalalamika kwa serikali mipaka ifungwe nafaka bei ishuke ili kuondoa uwezekano wa wimbi la bei za mazao kupanda wananchi hawana pesa.

Sijui kama wewe ndio muhusika wakutatua hizi changamoto utafanye?
 
Mabati yakipanda bei yakawa na faida wazalishaji wanaongezeka yanakuwa mengi demand inashuka supply inaongezeka bei inashuka, hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa... Serikali inatakiwa iache forces za demand na supply zifanye kazi, inatakiwa kuingilia kati kama kuna watu kwa makusudi wanaficha bidhaa ili zipande bei na si vinginevyo.

Suala la mshahara ni suala binafsi na umuhimu wa mfanyakaI husika, kama hautoshi ni jukumu la mfanyakazi kuchukua hatua kwa kufanya kazi inayomlipa. Kuna sekta ziliongezwa mishahara kutokana na umuhimu wao.
Demand and supply huwa theory isiyosimamiwa vzr!!! Mara nyingi wafanyabiashara ndio wanaosababisha demand kuwa kubwa kwa kuficha bidhaa na kukosa humanity,,kama ambavyo wewe unataka mtu apandishiwe bei ya chakula kisa eti serikali haijakusaidia kulima,,Ni vyema serikali ikasimami Wewe upate faida na mlaji asiumie pia
 
Wafugaji walikesha na kuomba mvua kwa Mungu kuokoa mifugo yao iliokuwa inakufa kwa kukosa maji na malisho,

Wachoma mkaa na wafyatua matanuli nao wanakesha na kuomba kwa Mungu asilete mvua kwani mvua inakwamisha kazi zao kufanyika hatamae wanakosa pesa zakuendesha Manisha yao.

Sijui Mungu asikilize lipi.

Wakulima wanaomba kwa sekali mipaka iwe wazi ili nafaka ipande bei wapate faida,
Raia nao wanalalamika kwa serikali mipaka ifungwe nafaka bei ishuke ili kuondoa uwezekano wa wimbi la bei za mazao kupanda wananchi hawana pesa.

Sikui kama wewe ndio muhusika wakutatua hizi changamoto utafanye?
Ndo maana Suleimani aliomba hekima
 
Demand and supply huwa theory isiyosimamiwa vzr!!! Mara nyingi wafanyabiashara ndio wanaosababisha demand kuwa kubwa kwa kuficha bidhaa na kukosa humanity,,kama ambavyo wewe unataka mtu apandishiwe bei ya chakula kisa eti serikali haijakusaidia kulima,,Ni vyema serikali ikasimami Wewe upate faida na mlaji asiumie pia
Unanilisha maneno. Sijasema bei ya chakula ipandishwe kumnufaisha mkulima, nimesema soko huria liachwe na serikali inunue bidhaa kwa bei ya soko na si kuzuia bidhaa ili bei ishuke.

Elewa maana ya soko huru, Demand and Supply haipaswi kuingiliwa na serikali au mfanya biashara. Mfanyabiashara anayeficha bidhaa kwa kushirikiana na wenzake ili bei ipande anafanya kosa, na serikali inapozuia soko ili bei ishuke inafanya kosa.
 
Back
Top Bottom