Ushauri: Rais Samia zuia mazao kwenda nje ya nchi, njaa inalinyemelea Taifa

Lima vya kwako afu uzuiwe usipeleke nje ndipo uone raha yake.
Si soko huria ama. Si unatafuta hela unazo una wasiwasi gani kwani utakula hela zako.
Yaani mtu alime umpangie auze wapi sio ujamaa huu ,
 
Ukiwa wewe kama rais hutachelewa kupinduliwa kwa kiacha kila mtu apange atakavyo hasa kwa vitu muhimu kama chakula,,,mtu unaweza kuacha kujenga ila huwezi kuacha kula,,,Nakujuza chakula ndio Usalama wa Taifa ndugu
Nunua weka ndani. Mie huwa napenda drought moja ama calamity matata itokee ili watu wajue shida ni Nini. Kuna watanzania wengi Sana hawajui shida ni nini
 
Fikira za ajabu na za kijinga kabisa, hivi ni lini tutaacha kuwatumia wakulima Kama punching bag?

Mwaka juzi, Jana na huu wakati mavuno yalipokuwa makubwa mlimsaidia vp mkulima kutokana na kukosa soko na Bei ya mazao kudorora? Badala ya kufikiria namna bora ya kuwainua wakulima wetu kwa kupata masoko nje na kuweza kupata Bei nzuri, ili wapate faida zaidi nakuinuka, sie tunawaza kuzuia wasipate masoko na Bei ya mazao isipande!!!. Very pathetic.
 
Hii ni njia ya kijima na fikra za kijima. Kwanza watu wanaouziwa nje si watu? Binadamu wote ni ndugu na sawa.

Wacha watu wafanye mambo kwa uhuru wao.

Huwezi lalamika mvua wakati Tanzania ni nchi pekee iliyozungukwa na maji ya kudumu.
Unafanya kazi taasisi gani we fisadi!! Nyie ndo mnafanya rais achukiwe we unadhani hali hii isipodhibitiwa rais ataeleweka machoni pa wtz!!? Njaa itamfanya apinduliwe kilaini sana,,Chakula ni Usalama wa Taifa nasisitiza mkulima asimamiwe asipate hasara na mlaji asiumizwe
 
Kitu rahisi ni kusimamia mkulima apate na mlaji asiumizwe alafu kumbuka wananchi weng wanalimia tumbo(subsistance farming) hivyo kulingana na shida za kitamzania hujikuta wameuza kila kitu kwa wafanyabiashara(walanguzi) alafu baadae wanaenda kulanguliwa kwa bei kubwa isiyomithirika
 
Kama nilivyosema, kilimo ni biashara ila tatizo wakulima wengi hawalimi kibiashara ndo maana wanalima tu bila kutengeneza au kulijua soko la bidhaa zao. Sasa hapo mlanguzi ndo anapoingia.

Unajua kazi ya serikali kuu ni kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia wake na kuhakikisha kuna mazingira mazuri kwa raia wake kufanya kazi na biashara......

Hizi kazi zingine tunaipa serikali sababu ni uvivu tu na kutojielewa. Jembe lako, Mbolea yako, Shamba lako, nguvu kazi zako, mazao yako, unauza kwa ridhaa yako ila unataka serikali ipambane kuhakikisha unapata faida. Tukielewa somo la soko huru, Watanzania wakulima watafaidika sana na biashara ya kilimo.
 

Njia na fikra kwa ujumla wake ni zakijima. Na mvua isiponyesha miaka 3 utafanya je kwa fikra za kijima namna hii utaendelea kuzuia kitu kisichokuwepo?
 
Kumbe wewe shida yako ni Rais, na sio chakula?

Acha kuwapangia wanaume matumizi ya mazao ya jasho lao. Kama unaogopa njaa, nenda ukalime vya kwako!
 
nyie wenye kadi zenu mtapona tutakufa njaa sisi wa upinzani
 
Mbolea imepanda bei, halafu tuanze kupangiana bei eti kisa kuna njaa...kila mtu ashinde mechi zake !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…