USHAURI: Rais teua Wakurugenzi wa Halmashauri, Halmashauri zinakufa huku

USHAURI: Rais teua Wakurugenzi wa Halmashauri, Halmashauri zinakufa huku

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2015
Posts
637
Reaction score
663
Tangu upite uteuzi wa Wakuu wa Mikoa hakuna kinachofanyika huku kwenye Halnashauri.

Kauri yako uliyoitoa wakati unawaapisha wakuu wa mikoa ya kwamba " zege halilali ,hii itaenda hadi chini" umesababisha viongozi hao ku-relux na kutofanya kazi.

Wapo wanaosema mama unaingiza watu wako ,hivyo unaondoa ulio wakuta wota kwenye nafasi hizo .Hii imesababisha watu kukata tamaa na kuacha kufanya kazi za usimamizi wa miradi, mapato na shughuli nyingine za kila Siku

Tangu uteuzi wa wakuu wa mikoa, kutendo cha kuingiza safu Mpya zaidi ya 50% imewaogopesha sana .

Kinachoweza kufanyika kwa sasa ili kuzinusuru hizi Halmashauri ni kufanya uteuzi wa nafasi hizo, ili kazi ziendelee. Huku mambo mengi yamesimama miradi ya vituo vya Afya ,Sequip zahanati ambazo zimepokea fedha mwaka uliopita ni kama zimesahaulika na hazijakamilika.

Kwa upande wa Mazahanati ambayo umeyapa fedha mwaka uliopita ndio kabisa ni kama yametekelezwa nchi nzima.

Fedha nyingi unashusha huku chini lakini zimejazana tu kwenye maakaunt ya Halmashauri ni kama wanakuhujumu kwa makusudi.

Spidi ya utendaji kazi na morari kwa viongozi hao ni kama imepungua mno, inahitajika kuingiza nguvu mpya itakayoanza upya.
 
Kama kiongozi ana maono katika utumishi wake hawezi kutishwa na mabadiliko ya uteuzi. Tatizo viongozi wengi hawana maono. Na bila maono, watu wanaangamia (without vision, people perish)
 
Na hii ni kweli wamekaa mguu mmoja nje mmoja ndani hawajui watabaki au watatenguliwa. Ila kwa ambae tayari anajua shughuli za kufanya akitoka hapo alipo hana wasiwasi.
 
Hofu ya kutumbuliwa sio ya mchezo mchezo, isikie kwa wenzako. Hasahasa kama hujajipanga kifedha kuishi nje ya ajira 😂😂😂😂. Sisi majobless tushazoea.



Unakaa roho juujuu unarefresh page ya ikulu mawasiliano kila baada ya dakika 5 😂😂😂
 
Unakut mkurugenz ashakopa pesa ndef na akabakiwa 1.1m kama take home, anaish kwa posho na stahk nyingine halafu umtangazie utumbuz? Lazm apanic!

Wakurugenzi msipanic wala kuwa wanyonge. Kapitieni masomo ya kikatoliki ya jpili ya nyuma huko, siku 14 nyvma
 
Nchi ikiongozwa na mwanamke nothing going on ,kuna mkoa kuanzia RC,DC,DED,RPC,Diwani,mtendaji, wote wanawake ni umbeaaaaa
 
Chawa wa wanaosubiria uteuzi naona mko kazini
 
Back
Top Bottom