Ushauri: Rwanda iache kufadhili waasi wa M23, Wakongo wameshachoka sasa

Ushauri: Rwanda iache kufadhili waasi wa M23, Wakongo wameshachoka sasa

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kuna maandamano kila mahali ya kupinga kitendo cha Rwanda kuwafadhili waasi wa M23 wanaoleta machafuka yasio isha huko DRC.

Wakongo wamechoka, Tanzania tumechoka, Afrika mashariki imechoka, Africa imechoka, na hata dunia imeshachoka. Waache sasa.

Na sisi Tanzania tujiulize, silaha nzito nzito za waasi wa M23 zinapitia bandari ipi? Ya Dar es salaam au ya Mombasa? Au ni kiwanja kipi cha ndege na ni shirika lipi la ndege linalowapelekea silaha huko mpakani na Rwanda?

Na kwanini M23 kila wanapozidiwa huwa wanakimbilia Rwanda na kupewa hifadhi kama wakimbizi ?, hii ina maana gani kwa nchi moja kukomaa kuleta machafuko kwenye nchi jirani, miaka nenda, miaka rudi? Kwani madini ya mashariki ya DRC si ni mali ya Wakongo wenyewe?

Kwanini wasiachwe wenyewe waamue nani wa kumuuzia leseni za uchimbaji madini? Kwanini Rwanda amiliki kinu kikubwa cha kuchenjulia dhahabu Afrika mashariki na kati wakati hana hata mgodi mkoja wa dhahabu.

Je, M23 wakikimbilia Rwanda wafuatwe huko huko au waachwe ili wajipange na wakishapewa silaha warudi tena msituni?

B8E64E56-BDAA-488F-967F-C6F2F56634DC.jpeg

===========================
Update: 19/11/2022

===========================
Update: 23/12/2022

Then wao Rwandees watakula wapi? Hizi conflicts zinawekwa makusudi kabisa ili kuleta mwanya wa mataifa ya nje kuchukua rasilimali za wakongo, once ukikubali kuingiliwa na mgeni ndani kwako lazima haya yatokee
Kama ni kutajirika kwa madini ya DRC basi Rwanda ameshatajirika sana, wawaache na Wakongoman nao japo wapumie, hata kam ni kwa muda wa miaka 10 tu, wapumzishwe jamani, nao ni binadam wale, waachwe wafaidi nchi yao.
 
Waache kufadhili hao waasi, halafu watapata wapi madini ya kuuza nje ya nchi!
 
Waache kufadhili hao waasi, halafu watapata wapi madini ya kuuza nje ya nchi!
Kwani kila mtu si ana rasilimali zake alizojaaliwa na Mungu? Mbona sisi Tanzania hatuna mafuta ila hatuvamii Uganda kisa wana mafuta?

Kila mtu aridhike na chake na apambane na hali yake, hii tabia ya kuvamia watu ili kupora rasilimali tumuachie US, ila tusivamiane sisi kwa sisi, tuwe na mshikamano.
 
Rwanda Wana kivutio cha makubiri ya vita ya kimbari. Aisee kweli Rwanda kavurugwa.
 
Kwani kila mtu si ana rasilimali zake alizojaaliwa na Mungu? Mbona sisi Tanzania hatuna mafuta ila hatuvamii Uganda kisa wana mafuta? Kila mtu aridhike na chake na apambane na hali yake, hii tabia ya kuvamia watu ili kupora rasilimali tumuachie US, ila tusivamiane sisi kwa sisi.., tuwe na mshikamano...
Kagame hana madini mengi kivile! Hivyo ameona atumie fursa ya kuzubaa kwa Wakongoman, kuvuna raslimali zao.

Maana hata Wachina na Mabeberu wengine wamejazana huko Congo kwa miaka nenda, wakibeba matani na matani ya raslimali na kuzipeleka kwao.

I wish na sisi Watanzania tutaanzisha masoko ya kununua madini kwenye mipaka na Congo mfano kule Kigoma, ili tuyanunue hayo madini kwa bei ya chini, na kwenda kuuza kwa bei ya juu kwenye siko la dunia.
 
Kagame hana madini mengi kivile! Hivyo ameona atumie fursa ya kuzubaa kwa Wakongoman, kuvuna raslimali zao...
Kitu kibaya sana ni kufadhili kikundi cha majambazi ili kuleta machafuko kwenye nchi jirani, ni kitu kibaya sana, biashara ya madini si kosa, kosa ni kufinance machafuko ili upate hayo madini bure badala ya kuyanunua toka kwa waKongo wenyewe.
 
Aise! Kumbe ndo unavofikilia hivo? Uliwahi jiuliza hao M23 ni kina nani? Wanapigania nini? Rejea kidogo historia ya nchi za Afrika mashariki tu,ndo uanze habari hizo za reja reja. Unapodai Rwanda ndo inawapa support, siraha zinazotumiwa huko kwenye uwanja wa vita zinatoka wapi? Uliwahi angalau jiuliza kuhusu hilo?!
 
Maswali meeengi, sema wewe unachojua ili tukijadili. Aache kusapoti waasi, period.
 
FRANCIS DA DON jeshi la Congo linaandikisha vijana wa kupambana na M23 nenda kajuinge huko.
Mali za Congo zinaibwa na kila mtu anaekwenda Congo kwa mgongo wa kulinda amani.
Viongozi wa Congo wa jeshi na serikali wanaiba.
Monusco wanaiba.
Un wanaiba.
Zimbabwe wanaiba.
Ug wanaiba.
Rwanda wanaiba.
US,China n,k wanaiba.
Kenya nao wanaenda kuiba.

shida ipo kwanza kwa wacongo wenyewe kabla ya kumnyooshea kidole Kagame.
kiboko ya M23 ndani ya jeshi la Congo alikua ni Kanali Mamadou Mustafa Ndala lakini wacongo wenyewe walimuuwa askari kinara wa kuliongoza jeshi kupambana na M23, tangia hapo M23 wakakosa kikwazo cha kuwazuia kusonga mbele.
 
Ile genocide ya 1994 ya Rwanda ndio iliyosababisha Wahutu wakimbilie DRC na kuunda kundi la kupigana dhidi ya Watutsi

Ila wananchi wa drc nao walipoona hivyo na serikali yao ilivyo hovyo wakatengeneza makundi kibao ya kupigana
Ndipo napo Paka akatengeneza March 23 kupigana na hao wahutu
Wakulaaniwa ni hao wanaopitisha silaha mchana kweupe kwenye bandari zetu kwa nguvu ya matajiri wazungu wauza silaha

Sio mataifa bali wafanyabiashara ya silaha
Lazima mizigo yao ichunguzwe sana maana naona Kenyatta na Pk wanakumbatiana majuzi ila wa kuelewa anaelewa silaha zinapitia wapi

Vita hazitaisha kama huwezi kudhibiti silaha
 
Drc ingekatwa tu maana ni kubwa sana jeshi lake haliwezi kuwamudu hao kwani wafadhili wengi ni wauza silaha kwani kuna sehemu jeshi lao haliwezi kutoka likienda huko bali watakufa au watajiunga na vikundi vingine

Yaani kama una hela ndefu unaweza kuunda kikosi chako na huku ukijihami na huku unaiba madini
Hivyo ndivyo wanafanya

M23 hawapo huko kupigana na Wahutu hapana bali wapo kwa masilahi mapana zaidi
Adhibitiwe huyo PAKA
 
Sawa, ila waasi wa M23 wakomeshwe mara moja, na anaewafadhili ashughulikiwe!
 
Sawa, ila waasi wa M23 wakomeshwe, na anaewapa support (Kagame) ashughulikiwe as a matter of continental emergency!
 
Drc ingekatwa tu maana ni kubwa sana jeshi lake haliwezi kuwamudu hao kwani wafadhili wengi ni wauza silaha kwani kuna sehemu jeshi lao haliwezi kutoka likienda huko bali watakufa au watajiunga na vikundi vingine

Yaani kama una hela ndefu unaweza kuunda kikosi chako na huku ukijihami na huku unaiba madini
Hivyo ndivyo wanafanya

M23 hawapo huko kupigana na Wahutu hapana bali wapo kwa masilahi mapana zaidi
Adhibitiwe huyo PAKA
Kuna mtu alitaka DRC imegwe vipande ilihali watu wanapambana kuiunganisha Afrika, nilimtukana vibaya sana. hivi China au Russia au India, ni kubwa au ndogo compared to DRC? Mbona ni super powers na zipo?
 
Sawa, ila waasi wa M23 wakomeshwe mara moja, na anaewafadhili ashughulikiwe!
huwezi kuwashughulikia M23 ukafanikiwa PK akiwa anamiliki powers,,,,never.nipo nimekaa palee[emoji117][emoji907].
ukikata mizizi umeuwa mti,matawi,matunda na kilakitu.
anza kwanza kung'oa mizizi jombaa.
 
Wakikimbilia Rwanda inabidi wafuatwe huko huko!
 
Back
Top Bottom