Ushauri: Serikali ifanye haya ili nchi ijitosheleze unga wa ngano

Ushauri: Serikali ifanye haya ili nchi ijitosheleze unga wa ngano

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Leo kulikuwa na Press conference baina ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha na Waandishi wa Habari.

Maelezo kuhusu upungufu wa ngano ulielezwa vyema na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kusema kuwa mahitaji yetu ya ngano ni tani 800,000 kwa mwaka na sisi tunazalisha tani 100,000 kwa mwaka na hivyo kuwa na upungufu wa tani 700,000.

Mhe. Waziri wa Fedha alieleza kuwa bajeti ijayo Serikali imetenga fedha nyingi na zitaelekezwa kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kilimo.

Napenda nitoe hoja kuhusu suala la ngano.
Katika miaka ya 1970s Serikali ilitenga maelfu ya ekari katika Wilaya ya Hanang kwa ajili ya kilimo cha ngano ikijulikana kama HANANG' WHEAT COMPLEX na ilikuwa ikishirikiana na Serikali ya Canada.

Mashamba haya bado yapo japo yalibinafsishwa na kuuzwa kwa wahindi ingawaje hakuna kinachoendelea.

Ninaishauri Serikali iyarudishe mashamba haya na kumpa Mwekezaji mwenye maono kama Mzee Seif wa Kagera Sugar ili hapo baadaye Serikali iweze kujitosheleza na suala la ngano.

Serikali ikiwa Serious na masuala ya kilimo nchi itajisholeza kwa chakula.
 
Hata mimi hili jambo linanishangaza sana, kuna jamaa yangu analima shayiri Karatu anawauzia Serengeti breweries.

Sijui tumelaaniwa na nini, hao Warusi na Ukraine wanalimaje? Wanatumia majini?
 
... mafuta ya kula tumeambiwa mahitaji ya nchi kwa mwaka ni tani 700,000 uzalishaji wa ndani ni tani 30,000 kiasi kinachoagizwa kutoka nje ni tani 670,000! Very interesting kwa kweli; siamini CCM imetufikisha hapa!
 
Hizo data huwa ni za uongo. Maana toka mimi ni mdogo nasikia tani laki sita. Mpaka leo nasikia ni hizohizo laki sita. Maana yake watu hawaongezeki. Je mafuta hayauzwi nchi za jirani?
 
issue siyo mashamba tu, je zimefanyika researches za kutosha kuhusu kilimo cha zao hilo hapa nchini kwetu ili kuwezesha kilimo hcho kufanyika kwa tija?
 
Leo kulikuwa na Press conference baina ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Waziri wa Fedha na Waandishi wa Habari.

Maelezo kuhusu upungufu wa ngano ulielezwa vyema na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kusema kuwa mahitaji yetu ya ngano ni tani 800,000 kwa mwaka na sisi tunazalisha tani 100,000 kwa mwaka na hivyo kuwa na upungufu wa tani 700,000.

Mhe. Waziri wa Fedha alieleza kuwa bajeti ijayo Serikali imetenga fedha nyingi na zitaelekezwa kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kilimo.

Napenda nitoe hoja kuhusu suala la ngano.
Katika miaka ya 1970s Serikali ilitenga maelfu ya ekari katika Wilaya ya Hanang kwa ajili ya kilimo cha ngano ikijulikana kama HANANG' WHEAT COMPLEX na ilikuwa ikishirikiana na Serikali ya Canada.

Mashamba haya bado yapo japo yalibinafsishwa na kuuzwa kwa wahindi ingawaje hakuna kinachoendelea.

Ninaishauri Serikali iyarudishe mashamba haya na kumpa Mwekezaji mwenye maono kama Mzee Seif wa Kagera Sugar ili hapo baadaye Serikali iweze kujitosheleza na suala la ngano.

Serikali ikiwa Serious na masuala ya kilimo nchi itajisholeza kwa chakula.
jamaa kuna gap wameishaliona hapo wanatafuta justification
 
Majaruba mengi ya mpunga baada ya kuvuna mpunga huwa yanakaa wazi. Nimejaribu kukaa maeneo ya karatu na mbulu wanakolima ngano nikagundua kuwa ngano inalimwa mvua zikiwa chache au zimeshapita. Sasa najiuliza yale majaruba ya mpunga kanda ya ziwa na kule ruvu na katavi na mpanda kule baada ya kuutoa mpunga wao wakulima kwa nn utafiti usianze mara moja ukawekwa ngano kuliko majarabu ya kilosa na ifakara kukaa empty yakisubiri msimu ujao wa zao la mpunga??????
Nawaza tuuu. I am standing to be corrected mimi sio mtaalamu wa kilimo.
 
Majaruba mengi ya mpunga baada ya kuvuna mpunga huwa yanakaa wazi. Nimejaribu kukaa maeneo ya karatu na mbulu wanakolima ngano nikagundua kuwa ngano inalimwa mvua zikiwa chache au zimeshapita. Sasa najiuliza yale majaruba ya mpunga kanda ya ziwa na kule ruvu na katavi na mpanda kule baada ya kuutoa mpunga wao wakulima kwa nn utafiti usianze mara moja ukawekwa mpunga kuliko majarabu ya kilosa na ifakara kukaa empty yakisubiri msimu ujao wa zao la mpunga??????
Nawaza tuuu. I am standing to be corrected mimi sio mtaalamu wa kilimo.
kwa uzoefu nao ngano inalimwa maeneo ya baridi
labda wa SUA watujuze hili badala kulisha panya wa kutegua mabomu tu
 
Serikali pia imepuuza sana kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha umwagiliaji kinatakiwa kufanyika mwaka mzima.
 
Mashamba ya HANANG' WHEAT COMPLEX bado yapo na yalikuwa yanatumiwa kwa kulima ngano. Kwa hesabu ya haraka ni hekta karibu 100,000. Mashamba yametelekezwa a Serikali iko kimya.
 
Serikali haina mpango wowote WA muda mrefu kwenye kilimo wao kila mwaka wanakuja na ngonjera zile zile mwkaa Jana mmepewa pesa za kovid nyie mkaamua kwenda kujengea madarasa inashangaza kwakweli alafu mtu anatoka mbele anasema mkopo WA masharti nafuu kuliko mingine ya nyuma wakati upeleke kwenye secta za kiuchumi ili mkopo urudi ww unaenda kuifukia chini
 
... mafuta ya kula tumeambiwa mahitaji ya nchi kwa mwaka ni tani 700,000 uzalishaji wa ndani ni tani 30,000 kiasi kinachoagizwa kutoka nje ni tani 670,000! Very interesting kwa kweli; siamini CCM imetufikisha hapa!

[emoji37] hatari sana
 
Back
Top Bottom