USHAURI: Serikali itoe namba za NIDA kwa watoto

USHAURI: Serikali itoe namba za NIDA kwa watoto

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Habari za majukumu JF?

Kulingana na hali ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia, naishauri serikali iliangalie hili suala la NIDA lisiwe kwa watu wazima pekee.

Naiomba serikali iweke utaratibu maalum wa kutoa Usajili wa NIDA kwa kila mtoto anaeanza elimu ya msingi.

Hili litatusaidia mambo mengi sana;

- Kwanza litazuia udanganyifu wa umri hapo mbeleni katika masuala mengi sana.

- Pili itatusaidia ku track location ya wazazi/walezi wa mtoto endapo mtoto atapotea kwa namna yoyote ile.

- Itarahisisha pia katika zoezi zima la ongezeko la idadi ya watu maana kila mwaka watoto wataingizwa kwenye mfumo.

- Kadhalika serikali itatambua idadi kamili ya raia wake katika level ya under Secondary na Primary bila usumbufu wowote hivyo itakua rahisi kupeleka maendeleo sehemu mbalimbali.

NB: Mifumo ya simu itumike kuwasajili ili iwe rahisi zaidi.

Karibuni kwa maoni.
 
Sio darasa la kwanza ,ukizaliwa tu unakuwa na number yako ya nida..ukifika 18yrs una update taarifa na kupigwa picha...
 
Yeah hii ni sawa kabisa, mtu apate number tangu akiwa kichanga, alafu mambo ya kitambulisho baadae
 
Back
Top Bottom