Ushauri: Serikali iwapigie magoti wafanyabiashara wa mafuta

Ushauri: Serikali iwapigie magoti wafanyabiashara wa mafuta

Hapana aisee, yaani Serikali ipigie magoti wafanya biashara wahujumu uchumi?.

Serikali ni chombo chenye taasisi zote za usalama na jeshi vinavyoweza kujua kila kitu.

Piga ban, filisi na wengine peleka jela, Hakuna nchi iliwahi kuendelea kwa kubembeleza wezi, wajinga na wavivu.
Haya si ndiyo alikuwa anafanya Magufuli akawa anapingwa sana kwa jina la Demokrasia!
 
Biteko kawekewa mtego na wahuni, ngoja tuone.
 
Kwa ujinga wao wa kuwakumbatia wafanyabiashara na kuwageuza miungu watu, wanaweza kweli kuwapigia magoti, kwasababu ni serikali ya mjinga ndio imewafanya hao wafanyabiashara waiendeshe wanavyotaka.

Nchi imekosa uongozi kabisa, tatizo alilotengeneza mjinga kwa kuwaruhusu wajanja wale kwa urefu wa kamba zao, ajabu anataka Biteko akalitatue, kama akishindwa amtumbue kisingizio ameshindwa kazi, wakati yeye mjinga asiyejitambua ndie chanzo cha matatizo yote.
Wewe mbona unahangaika sana na rais? Biteko hata hajakabidhiwa ofisi tayari unasema mama anataka amtumbuwe hivi wewe kichwani upo sawa kweli?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Wafanyabiashara wameshika nchi. Wanaweza kupanga nini wafanye wakati gani. Wanaweza kupata taarifa nyeti za serikali. Wale wa mafuta wamejua bei inaenda kupanda. Kwa hiyo wameficha mafuta ili waje wapige hela.

Lakini wanafanya hivyo mbele ya mamlaka za nchi, na pengine chini ya ulinzi wa mamlaka. Who knows.

Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake. Wanaona kama DPW kaweza kwani wao washindwe wana nini?

Kama ni hivyo, basi mama awapigie magoti ili kuleta ahueni. Nchi itaanguka hii jamani. Hawa watu wana nguvu, waulizwe wanataka wapigiwe magoti hadharani au kifichoni.

Enzi za Magufuli huwezi kufanya huu ujinga. Kuficha mafuta ni kuhujumu uchumi. Utapewa kesi wewe na wajukuu zako. Lakini hizi ni enzi za mama
Africa ya Kati jeshi limejidhihirisha kuwa ni la wananchi wamekataa upumbavu wa wanasiasa kuyumbisha nchi jinsi watakavyo kwa sababu za kijinga na kipumbavu,tumebaki ss Tanzania nchi ambayo wanajeshi ni vipofu na hawana ndugu ktk Taifa hili.
 
Back
Top Bottom