Ushauri: Serikali kupitia TRA iwakamate wananchi wanaotoka kununua vitu bila risiti

Kama nimetoka kwenye duka la hardware nimebeba mzigo wa mil.2 nimekamatwa nikapigwa faini hata mil.1 huo ujenzi si utakuwa mwakani tena.
 
Duh aisee kwa mwendo huu tutafika kweli. Badala ya kusema labda serikali itazame namna ya kuongeza malipo kwa njia ya mifumo kama bank kupitia debit cards, mobile money na zinginezo ili taarifa zote ziwe electronically, wewe unaongea mashudu gani sijui hapa.
 
Hiyo Mbona imefanyika Sana kariakoo kipindi cha mwanzo cha Jiwe lakini wafanyibiashara nao wakajiongeza ikafia mbali
 
Serikali inatakiwa ipunguze Kiwango cha VAT kwa ujumla ili wananchi tuweze kudai risiti na wafanyabishara wasione tabu kuzitoa hizo risiti.
 
Elimu ya kutosha kwanza. Nakubaliana na wewe.

Kuanza kukamata tu hovyo haitasaidia. Wengine watoto, wengine wageni, wengine hawajui kusoma wala kuandika, etc. Sanasana italeta taharuki tu. Mahabusu yenyewe ya kuweka watu ndani zipo wapi?

Hata hizo risiti unazopewa sasa, unaweza kujua kama genuine ama la?

Nakubaliana na wazo lako la kugawa hizo mashine bure kabisa lakini kusiwe na makato. Iwe ni mali ya TRA. Ikiharibika unawarudishia, wanakupa nyingine. Mfanyabiashara asitoe hata senti kupewa hiyo mashine.
Actually hilo la efd system kuwa na rekodi za mauzo na manunuzi ya mlipakodi ni the best thing likiweza kufanikiwa.

Yaani TRA akija kwangu mfanyabiashara anioneshe mauzo na manunuzi yangu. Ukinunua bidhaa anayetoa risiti ni lazima aweke TIN yako. Kwa sasa hivi utaratibu ni wa hovyo kabisa .....yaani unaenda sheli kununua mafuta (hata kwa bidhaa nyingine), lakini risiti unayopewa haina uhusiano wowote na utambulisho wa gari lako wala wewe uliyelipia. Hii ni area TRA wanaweza Ku address na ikaleta incentive zaidi kwa wafanyabiashara kutumia machine za efd.

Tatizo jingine linahusiana na hili ni la risiti kufutika baada ya muda. Hii sio sawa. TRA walitizame tena. Kwa teknolijia ya sasa hili halipaswi kutokea.
 
Mbongo unambembeleza hivyo ataenda? Mimi niliwahi kuleta uzi humu kuwa tumsaidie mama Samia kwa kuwa Sasa hivi kariakoo suala.la risiti ya EFD ni Kama halipo Tena.

Nikashambuliwa Sana na watu humu, sikujua kuwa watu hawapendi kulipa kodi
Acha serikali iendelee kutubembeleza kulipa kodi ili tuone tutafika wapi. Kwa mbali naona tumeanza kuwaomba IMF watusaidie kugharamia SGR na Nyerere dam construction. Kodi ilipwe kwa hiari, tusilazimishane. Ni udikteta na ukandamizaji wa haki za binadamu kulazimishana kulipa kodi.

Viva JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inachekesha kwa kweli. Kumbana mfanyabiaahara ni kumkandamiza ila kumbana mteja si kumkandamiza. Awamu hii tutaona vituko vingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ushamba tu wa Mwendazake na haturudi huko. Kuchukua risiti ni HIARI ya mtu world wide.

Nimefanya shopping worldwide iwe SA, Kenya, UK, Italy hata Asia. Pale ninapotaka ku claim VAT Airport ndipo ninafai risiti.

Huyu Mwendazake baada ya kuwa frustrate Big taxpayers akakosa makusanyo. Kwa hiyo akataka akakusanye kwenye ma petrol stations, maduka ya nguo, restaurants na hadi kwa mama Ntilies.

EDF machine na risiti siyo dawa ya kuzuia wakwepa Kodi. Pamoja na hizo EDF machines wafanyabiashara walikuwa wanakwepa tu.

Ushauri kwa TRA weka misingi rafiki ya watu kulipa Kodi including viwango vya chini. Jadilini na wafanyabiashara Ni vitu gani vinawakwaza na namna bora ya kulipa Kodi. Hangaikeni na BIG TAX Payers, waacheni hawa wadogo wakue then muje mukusanye wakishakuwa wame grow
 
Hatuwezi kutumia SGR na Stiglers project kama msukumo wa kukusanya Kodi.

Kama mradi haukufanyiwa feasibility study sawasawa ambayo inaonyesha utapata wapi fedha za ku-finance ujenzi, tusihamishie mzigo kwa wananchi kuwabambika kodi za kidwanzi.

Mwendazake alianzisha miradi mikubwa kwa pupa bila kupima uwezo wa nchi kugharamia ujenzi.
 
Kwahiyo hai wananchi ndo watakuwa wakiwasilisha mahesabu ya Kodi tra?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza hayo marisiti yanachafua mazingira watafute njia risiti itoke kidigitali
 
uko sahihi lakini ungekuwa sahihi zaidi kama ungeshauri zaidi elimu itolewe kwa walipa kodi,hizo gharama za vikosi kazi zingeelekezwa kwenye kutoa elimu faida ingekuwa kubwa zaidi
 
Unafikiri kuna nyenzo za kutosha kuwakabili watanzania toka saa kumi alfajiri hadi saa nane usiku?
 
Nchi ina maafisa tehama kibao waliosoma ndani na nje ya nchi, hamuajiri, hamuwapi nafasi kuonesha uwezo mmekalia mbinu za enzi za ujima tu, TRA ndio anayetoa loophole ya watu kukwepa kodi, wakiona yanawashinda wanaanzisha taskforce na sheria kandamizi.
 
... huu nao mtihani!

Kwani ni huo tu? Hivi EFD inajali gharama za mzigo mwuuzaji anauouza?

Tuacheni ushabiki kwenye mambo ya msingi yanayolalamikiwa na waathirika.
 
Naamini Suluhu atapata muongozo wa Uhuru kuhusu jinsi wao wanafanya na kufanikiwa ukusanyaji kodi bila uonevu au makundi flani kubebeshwa mzigo mkubwa wa kodi.
 
Hivi mkuu sheria inasemaje kama nimekopa dukani! je nitapelewa risiti siku nikilipa au napewa kabla ya kulipa?
 
Wamachinga wanatoa risiti?
Wauza-genge nao?
Huo ni wimbo uliochuja tangu juzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…