Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kaka zangu.....
Hebu kabla hatujalala tuambiane kakitu.
Kuna wanawake Mungu amewapa tu akili nyingi. Yaani naturally tu ana akili sana, ana mawazo ya mbali sana, ana upeo mkubwa, amekomaa kichwani, yuko serious na maisha, yuko very calculative na akikushauri ukamsikiliza unatoboa. Wengine wa aina hii wanakuaga viongozi au wakuu kwenye maeneo fulani. Most of them are very strong minded. Focus yao ni maendeleo zaidi. Wako tough pia kwa sababu zinacharge sana.
Anaweza kuwa na umri mdogo lakini akili yake na hekima yake haifanani na umri wake. Ni Mungu amemuumba hivyo. Anaweza kuwa na madhaifu ya hapa na pale kama binadamu mwingine yeyote lakini kichwa chake kimechangamka. Saa zingine ni kama anaweza kuwa anakuzidi akili hivi ukimuangalia mambo yake japo huwezi ku-admit. Unajikaza kiume🤣 of which inaeleweka. Hatukulaumu, mfumo dume unatesa wengi. Anaweza kukutandika maswali na kukufikirisha mpaka ukafikiri sijui uko kwenye mtihani gani lakini lengo lake ni kujenga.
Sasa ikitokea unaye wa design hii kama mke fanya hivi;
1) Kubali kwamba mwanamke uliyeoa sio kilaza na ana akili nyingi na kukubali sio udhaifu. Ni hekima na inaonyesha ukomavu na inaonyesha unajiamini na unajua nafasi yako kama Baba na kama Mume haiwezi kubadilika hata kama mke ana akili kiasi gani.
2)Mpokee kwa shukrani kama zawadi yako kutoka kwa Mungu. Badala ya kumuona mjuaji, Muone ni asset. Mfanye rafiki na mshauri wako wa karibu. Hiyo ni rasilimali Mungu amekupa kaka.
3)Ona kwamba Mungu amekupendelea sana kukupa aina hiyo ya mwanamke kwa sababu wanaume wenzio wanatamani wangepata wa hivyo na hawana. Mtunze, mlee kama lulu yako ya thamani ili aishi miaka mingi akusaidie ufanikiwe sana.
4)Akili zake zisikutishe na kukufanya ujisikie kilaza. Wala usimuone tishio. Baraka kwenye familia zinaweza kuja kupitia mke, mume au wote wawili kwa pamoja. Kuwa positive, mfurahie, mpe nafsi na zitumie akili zake kukuletea wewe na familia faida. Kama umeshamjua ni mzuri kwenye jambo fulani usijitutumue kwamba unaweza sababu ni mwanaume wakati kiukweli yeye anaweza kuliko wewe. Weka EGO chini, Mpe nafasi yeye anayekiwezea afanye, utakuja kunishukuru.
5) Mpende sana. Usimkandamize, wala usiruhusu insecurities zikakupa hasira na husda ukaanza kumminya na kumbana. Wanawake wa hivi wakipendwaga na wakajua wanapendwa aisee they go extra mile. She will burst her head to support and strategically plan things ili wewe utoboe. Hakuna mwanamke asiyeweza kushuka na kunyenyekea kwa mwanaume anayemdekeza na kumuonyesha upendo. Tunakuaga wadogo kwa aina hiyo ya wanaume.
Lakini ukiwa jeuri na kumuumiza na kutokumthamini na kutokumsikiliza, atakuona unatumbukia shimoni hapo na njia ya kukuokoa anaiona na atakuacha. Hataitumia akili yake kukusaidia. Atanyamaza akuache na ego yako uharibikiwe.
Muwe na siku njema.