Ushauri tafadhali juu ya uchumba huu

Alkelokas

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2012
Posts
203
Reaction score
103
Habari wanajukwaa.

Mimi ni kijana wa kiume nina mchumba ambaye tulikubaliana tuanze kuishi kama mme na mke mwezi wa 12 mwaka jana.Lakini kulitokea tatizo kidogo amabapo dada ake alikuwa anaumwa nayeye akawa ndio mtu wa kumsaidia pale nyumbani alikoolewa dada yake.Hivyo nikaamua kumpa mda apate nafuu mgonjwa,Lakini alipopona akaanza kusogeza mda akakidai hadi mwezi wa 3,nikimuuliza sababu anadai nisubiri pasipo sababu za msingi.

Nawakati huo nilishatoa kishika uchumba kwao,hata hiyvo mama yake amekuwa akimwambia aendoke nyumbani na aje kwangu,lakini amekuwa mtu wa kuahidi siku fulani naja,ikitimia hafiki na kutoa sababu kama anaumwa.Nimejaribu kumwambia kama haupo tatari kwa sasa ama umepata mwingine naomnba nikwache uwe huru, ufanye unavopenda.

Yeye huniambia nasema hivi labda nimepata mwingine wakati sivyo,siku inayofata anadai si umeamua nakurudishia hizo pesa zako ukitaka. Nikamwambia niwewe ukirudisha ama usirudishe hamna shida.Baadae anaanza kusema basi nipe wiki nakuja kabla haijatimia anaanza sababu ila mama anaenda kesho kuuguza bibi huko siwezi kuondoka home. Lakini nikapeleleza ikawa kweli hadi leo hajarudi lakini sioni kama kuna sababu ya msingi,hivi kwa hali hii kuna changu hapa.

Ushauri please.
 
Anza mkakati wa kupata mwingine hapo hamna kitu. Anaona aibu kukuambia moja kwa moja kwamba anza mbele. Soma alama za nyakati kijana.
 
Mie naona hamna love hapo between you two,wewe uko eager kuvuta ndani ule vitu,wkt mwenzio anaquestion km kweli unampenda ama unataka kumtumia tu as sex machine.......mfano ni hapo alipotingisha kiberiti eti arudishe posa na wewe ukamjibu ni juu yake arudishe ama la,simply humpendi huyo.msichana and she is confused.......wote chapeni lapa...
 
Hivi kutoa kishika uchumba inamaanisha mwanaume anaweza kuishi na mwanamke?

Maana naona kama jamaa kakomaa na kishika uchumba as if ni mahari...


Hebu nisaidie kushangaa............
Ukweli ni kwamba huyo mwanamke kashashtuka kua hapo hamna ndoa.....na ndio anatafuta pa kuchomokea. Hivi kishika uchumba si inaweza ikawa elfu 10,000/- au 20,000/- au????
 
Mmmh vipi unaomba muanze kuishi kama mke na mume kwasababu tu umelipa mahari.....mahari haikupi hiyo rights. Mimi naona bado hajakuwa tayari...usinganganize.

Mpe time...
 
Jichunguze kwanza wewe mwenyewe,inawezekana nawe n tatizo pia.ila kama wewe hauna tatizo basi kunawalakin mahali
 
Jamani Kishika Uchumba Si Tiketi Yakuchukua Binti Wawatu Uishi Nae, Nafikiri Binti Hakuamini Ndo Maana Anasita Kuja, Yani Kisa Umetoa Posa! Aje Akupikie, Akufulie, Usafi Kwaujumla, Bado Abebe Namimba Bila Ndoa, Kesho Ukiona Mwingine Uanze Kumponda Binti Wawatu Bure, Kama Unampenda Funga Nae Ndoa Kwanza Ndo Aje Kupika Nakupakua
 
Mimi sina tatizo kwan nilimpeleka hata nyumbani kumtambulisha na ilifana kweli sa sielewi, anasumbua nini, hata hivo nmemwonya kuwa naoa mwingine anadai hata nikioa lazima nae aje tu.sa nashndwa kumwelewa ana maana gan.
 
Kinachoniudhi nlikuwa nipo wazi sana kiasi kwamba mtaani kote wanafahamu hii relation, kiukweli natamani kufanya uamuzi mgumu lakni nahisi kama nishajitia dosari isitoshe tumefanya mengi kama kununua vyombo na kuvihifadhi mwenyewe kwa mshenga.
 
Niliwahi kusikia wakisema....
Shimo la panya halizibwi kwa mkate
 
Huwezi lazimisha kuishi na mtu eti kisa kishika uchumba,ningekuwa mie mwenyewe ningekataa.maana unaweza ukaishi na njemba ukaja shtuka umri umeenda hamna ndoa wala mahali,anza proess za ndoa ili ajue kama kuna ndoa kati yenu.ila nahisi kama unalazimisha sana hayo mahusiano?.
 
Sijamlazimisha kisa kishika uchumba coz mahusiano ni ya mda mrefu tu nayeye ndiye aliyependekeza kama nipo siriasi nitoe kishika uchumba.na kuhusu kumwoa tulipanga nae.
 

Habari za ndoa hatukupanga tulichokubaliana ni kuoana kwa staili hii ya kumove herself from their home.
 
Alkelokas

Nahisi upo kwenye wakati mgumu hadi nimekuonea huruma.wewe ni mwanaume na inabidi ujikaze kiume au labda nikuazime roho yangu maana mie msichana ila na roho ngumu hatari.

Usimlazimishe mtu kitu ambacho hakitaki huwa mala nyingi tuna kero kulazimishwa kufanya kitu ambacho hukipendi,jiandae kwanza kwa ajiri ya mahari na harusi,huyo mkeo mtarajiwa jaribu kuongea naye kistaarabu tena mpeleke sehemu nzuri ambayo mlishawahi kwenda na akapafurahia au mpeleke sehemu yeyote nzuri na tulivu kwa ajiri ya maongezi yenu ya maandalizi ya ndoa na mahusiano yenu.

Jaribu kujishusha na umweleze umuhimu wake kwako endapo utamkosa,mpe zawadi special na umwambie ya kwamba unampenda sana na hutaki umkose kwenye maisha yako,kwa wakati huu uliopo usipende kumlazimisha kitu huyo msichana na jaribu kuwa chini yake hadi pale adhima yako ya ndoa itakapo timia mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…