Ushauri tafadhali kabla sijazirejesha hizi 10mil benki

Ushauri tafadhali kabla sijazirejesha hizi 10mil benki

kama wewe sio mfanyabiashara.. na hujawai kufanya biashara yeyote maishani mwako.

mimi nakushauri peleka hizo hela bank kafute deni lako lote kama ulivyowaza.

biashara ni risk na ili zifanikiwe zinahitaji experience. sasa wewe experience hauna na bado hutaki hasara hata iweje...

peleka bank tu mkuu nenda kafute deni..

watu watakushauri na pm nyingiii.. ili wafaidike tu wao... hakuna mfanyabiashara wa kumfaidisha mwenzake... kabla yeye hajafaidika
Hali ya uchumi haiko vizuri kwa mtu mmoja mmoja(uchumi wa taifa uko fresh) sasa upepo wa biashara umebadilika sana.naomba rudisha mkopo wa watu sababu wewe huna uzoefu wa biashara inaweza kukucost kwa kipindi hiki na baadae ukashindwa kurudisha mkopo. Vumilia hali ikae sawa baada ya miezi kadhaa hata ukienda kukopa tena utakopeshwa sababu wewe ni mteja mzuri na muaminifu kwa historia yako ya kurudisha mkopo kwa wakati.
rudisha mkopo utafungwa

TAFADHALI WASIKILIZE HAWA
 
Afanyeje?.. Maana nimejaribu kusoma, hata kwa kugeuzageuza nimeshindwa kukuelewa ulichoshauri.
Mwenye deni kaelewa,we mnazi unaelewaje unadhani?wacha nipite [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Nilikopa 15mil katika tasisi moja ya kifedha kama miaka 3 iliopita nikaomba wanikate makato makubwa ili nilipe kwa muda mfupi it was like 493000 kwa mwezi.
Sasa haya makato ni makubwa mno nimefanya mishe nimepata kama 10mil hv lengo langu nikafute hilo deni coz naamin balance yangu huko bank haiwezi kuzidi hyo pesa kwa muda walionika hzo pesa .
Sasa naomba ushahuri wowote wa kujenga kabla sijarudisha huu mpunga
Hivi siwezi zungusha kwa namna yeyote huu mpunga ukazaa ili unipunguzie machungu kidogo wadau au nizidabo ili maisha yaendelee?
Note
Me sio mfanya biashara na sina uzoefu wowote wa jambo hilo



Kama hujawai kufanya biashara nakushauri rudisha hizoo hela bank.


Hiki kipindi ni kipindi hatari sana kwa biashara.
Ukichangia tena wewe si mzoefu.
 
Nilikopa 15mil katika tasisi moja ya kifedha kama miaka 3 iliopita nikaomba wanikate makato makubwa ili nilipe kwa muda mfupi it was like 493000 kwa mwezi.
Sasa haya makato ni makubwa mno nimefanya mishe nimepata kama 10mil hv lengo langu nikafute hilo deni coz naamin balance yangu huko bank haiwezi kuzidi hyo pesa kwa muda walionika hzo pesa .
Sasa naomba ushahuri wowote wa kujenga kabla sijarudisha huu mpunga
Hivi siwezi zungusha kwa namna yeyote huu mpunga ukazaa ili unipunguzie machungu kidogo wadau au nizidabo ili maisha yaendelee?
Note
Me sio mfanya biashara na sina uzoefu wowote wa jambo hilo
kma ww ni mwajiriwa na ratiba zako za kazi hazi eleweki nakushauri usijiingize kwenye Biashara yeyote! yaani utajuta tu maana biashara inahitaji usimamizi mkubwa sana hasa hasa pale inaanza kwa sababu cost zote za uendeshaji zinakuwa zinatoka kwenye mtaji huo huo. ila kma ratiba yako iko vzur ndio nitaanzia hapo
 
Kwanza tuanzie kwenye hizo M15 ulizokopa ulizifanyia nini? Ulinunulia gari, ulijengea au ulizilia bata?
Nilianza mambo ya ujenzi lakini sikufika pale pahala nilitarajia mkuu.
 
Ni kweli mkuu. . biashara inahitaji experience lakini je ukikaa tu hiv jiv unahis experience utaitoa wapi? ?
Pia hela bila kuirisk huwez kupata nyingine kwa mfani mtu unanunua basi leo kesho linapata ajali, riski ni kawaida tu kwenye biashara
(Nimefanya biashara kidogo now ni muajiriwa)

Sasa mkuu lazima uangalia na mazingira uliyopo ni biashara ipi inatoka, pia lazima iwe biashara ambayo utaweza kuisimamia mwenyewe yaan isiwe na muingiliano na kazi zako. .
Kwa mfano hapo biashara ya mobile phone accesories inalipa sanaaaa. Na katika kuwekeza haizid 5 milion. Maana yangu ni kwamba unafungua duka la wastan la phone accesories then hiyo tano unaweka akiba au unafanyia kingine
Naongelea phone accesory ka kua ndio biashara niliowah kufanya na ninaifahamu vizuri na hata machimbo ya bidhaa zake nayajua, sjawai kufanya biashara tofaut na hiyo. .
Sasa hii biashara inategemea upo maeneo gan/mazingira gan mkuu.
Mkuu na hali hii ya sasa hiyo biashara bado iko pouwa, maana nyingine huku zimedorora kama vip tuhamie huko
 
ukitaka kupata ushauri ulio-endesha shule, lazima ueleze interest rate ya huo mkopo, ueleze pia kama ukirudisha kabla ya muda uliokubaliana na benki watakata asilimia ngapi. Hapo sasa ndio nitakushauri urudishe lumpsum au ununue kiwanja kama bado.
 
Watu tunakurupuka sana, biashara huwezi kufanya bila kuwa na uzoefu wa aina ya biashara unayotaka kufanya. Mfano., unataka kuwa mama ntilie lazima uwe umepitia hiyo shughuli hata kwa kuajiliwa.

Kalipe deni uwe huru, ukijiingiza tu sehemu husio ijua basi umeliwa, na deni utaendelea nalo kama kawaida. Unaujua mchezo wa kekundu na kehusi? Umeshaona yule mchezeshaji anavyoongea na mate haya mkauki? Umeshaona macho yake yanavyo kuangalia na yanavyo uangalia mchezo? Umeshaona mikono yake ilivyo faster zaidi ya 4G ya tigo? Huo ndio uzoefu.
 
Mkuu me nafanya biashara, Upepo sio mzuri kabisaaa, labda ngada but biashara halali unatakiwa uwe mvumilivu Sana.
Anyways ukiamua biashara Tafuta sehemu nzuri yenye mzunguko want watu fungua restaurant Safi tuu, but make sure unakuwa mwenyewe otherwise utafeli.
Biashara y'a Mkaa pia iko Safi but uwe tayari kukimbizana Na maliasili
Ni hayo tuu
 
Back
Top Bottom