Mkuu,
Sina uhakika kama tayari ushanunua gari, ila kwa hayo magari uliyoyalist, ushauri wangu ni kama ifuatavyo:
Toyota Vitz
Ni nzuri kwa utumiaji wa mafuta. Spea zipo ila bei mbaya. Sio gari imara sana kwa kifupi. Kama una hela ya kununua spea kwa gharama, ni gari nzuri.
Duet
Hili sikushauri hata kidogo. Lina 3 pistons. Hii engine inasumbua na kuna wakati inaweza kuleta mlio fulani kwenye engine (kawaida ya 3 pistons engine) ambao kuurekebisha ni ngumu (au haiwezekani kabisa). Utaangaika tu kwa mafundi.
Utumiaji wake wa mafuta ni mzuri, ila engine ni kimeo.
Allex
Hii sijawahi kuigusa, hivyo sina uzoefu wa spea wala uimara wake. Haina tofauti na toyota RunX, zote zinatumia engine sawa (inategemea na model lakini)
RunX
Hii ni Corolla Runx. Ni nzuri, ila sina uhakika na ubora wa engine wala upatikanaji wa spea. Ila, kama ilivyo kawaida, gari mpya spea zake ni ngumu kidogo kupata na bei huwa juu. Hii inawezekana kwa Allex na RunX, ingawa sina uhakika.
Pia, kama unatazamia kununua Allex au RunX, angalia pia na IST. Zote zinatumia Engine sawa, na bei zake zinakaribiana sana, lakini zipo juu. FOB ya chini ni around USD 3,600 (kwa gari nzuri)
Suzuki SWIFT
Achana na hii gari mkuu. Spea ni ngumu kupata.
Inatumia mafuta vizuri, na ni gari nzuri. Ishu itakupata kwenye spea tu.
Bottom line:
Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, engine ndogo ya Toyota 4E-FE ni engine bomba sana, imetulia na spea ni bei chee kila kona. Inatumika kwenye Toyota Starlet na Raum (na model nyingine nyingi tu)
Toyota Starlet ni model ya nyuma kidogo, ni nzuri, ila Raum ni ya mpya zaidi ya Starlet.
Kama unataka gari ndogo, spea zinazopatikana ki urahisi na bei nafuu, Toyota Raum is among the best options out there.
Ila, kama wewe sio mtunzaji mzuri, mlango wa nyuma unaweza kuharibika mapema. But anyway, spea zipo na ni bei nafuu.
Kazi kwako.
Ramthods